Winamp Logo
SportsCast Cover
SportsCast Profile

SportsCast

Swahili, Sports, 1 season, 62 episodes, 1 day, 10 hours, 2 minutes
About
Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili mada mbalimbali zinazohusu mpira wa miguu. Tunaangazia uwekezaji, mbinu na historia mbalimbali za Soka.
Episode Artwork

Washambuliaji wawili, mawinga wenye kasi na namba 10

Kuna surprise kibao kwenye Ligi Kuu Tanzania bara ambazo tumeziona baada ya Game week mbili. Matumizi ya washambuliaji wawili Timu kuhamia back-four Mawinga wenye speed Singida Big Star Aziz Ki vs Chama Sikiliza episode hii kuyajua yote hayo kisha tupe maoni yako  
8/31/202228 minutes, 17 seconds
Episode Artwork

Chelsea ya Thomas Tuchel

Tangu amechukua mikoba ya kukinoa kikosi cha Chelsea, Tuchel amekuwa akihusudu mfumo wa mabeki watatu kuliko ule wa mabaki wanne ambao alikuwa akiutumia akiwa PSG. Clifford Sangai na Prosper Bartalomew wanajadili kwa kina falsafa za raia huyo wa Ujerumani. Miongoni mwa yaliyoongelewa ni kama Tuchel anaweza badili mfumo au atasalia na wa sasa? Kitendawili cha Havertz, Werner na Lukaku bila kusahau namna anavyotegemea Wingback wakati wa kufanya mashambulizi. Sikiliza zaidi Episode hii
6/3/202223 minutes, 24 seconds
Episode Artwork

Mwaka mmoja wa Nabi: Mbinu na Ufundi

Ni mwaka mmoja sasa tangu Nasreddine Nabi achukue mikoba ya kukinoa kikosi cha Yanga kutoka kwa Cedric Kaze ambaye kwa sasa ni msaidizi wake. Kuna mambo mengi ameyabadili katika kikosi hicho ambayo Clifford Sangai na Prosper Bartalomew wanayajadili katika episode hii. Kati ya hayo ni kumfanya kiungo Feisal Salum kucheza katika eneo la mbele zaidi kuliko alipokuwa akicheza hapo awali. Swala la muhimu zaidi ni nafasi ambayo wachezaji vijana waliopo Yanga wanapewa nafasi na Nabi. Sikiliza episode hii kisha tupe maoni yako.
5/6/202224 minutes, 22 seconds
Episode Artwork

Taifa Stars ya Kim Poulsen

Stars ya Kim ni tofauti na ya Etienne lakini kuna vitu vinaendana. Episode hii emejikita katika kuangazia falsafa za kocha Kim Poulsen anayekinoa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili hayo yote bila kusahau aina ya wachezaji ambao Kim hapendi kuwakosa kwenye timu. Je ni wachezaji gani hao? Sikiliza Episode hii hadi mwisho
4/6/202216 minutes, 33 seconds
Episode Artwork

Je, Carlo Ancelottii amebadilika?

Tangu miaka ya 90 wapenzi wa soka walianza kushuhudia kazi za Carlo Ancelotti ambaye ni raia wa Italia. Katika miaka yake yote kama kocha ameshuhudia mabadiliko mbalimbali katika soka barani Ulaya lakini amwezaje kudumu katika taaluma hiyo kwa kipindi kirefu? Clifford Sangai na Prosper Bartalomew wanajadiliana kuhusu falsafa, mbinu na ufundi wa kocha huyo ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Real Madrid kwa muhula wa pili. Kuna mengi sana tusiyoyajua kuhusu Ancelotti, sikiliza episode hii kisha utupe maoni yako.
3/22/202215 minutes, 21 seconds
Episode Artwork

Falsafa ya Marcelo Bielsa

Wengi huvutiwa na soka la timu anazofundisha kama Marseille, Lille na Leeds ambayo kwa sasa imemtimua. Kuna mengi ya kujifunza juu ya falsafa ya Marcelo Bielsa na hapo ndipo kunamfanya Clifford Sangai aketi chini na Prosper Bartalomew kujadili kwa kina mbinu na ufundi wa raia huyo wa Argentina. Tumeongelea aina yake ya ukabaji ambayo ni 'MAN TO MAN" tukiangazia kwa kina namna ilivyofaulu na kufeli hasa akiwa na Leeds United. Prosper alienda mbali zaidi kwa kulinganisha mbinu za Bielsa dhidi ya Gian Piero Gasperini ambaye anakinioa kikosi cha Atalanta kinachoshiriki ligi kuu ya nchini Italia maarufu kama Serie A. Sikiliza uchambuzi huu pia share na wengine zaidi.
3/8/202215 minutes, 51 seconds
Episode Artwork

Kwanini kiwango cha Lukaku kimeshuka?

Tangu Lukaku afanye mahojiano na Sky sports, amecheza mechi sita za Ligi Kuu bila kufunga bao. Clifford Sangai ameamua kukaa chini na Prosper Bartalomew kuangalia mwenendo wa mshambuliaji huyo wa Chelsea ambaye msimu uliopita alifunga mabao 24 na assists 11 akiwa na klabu ya Inter. Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni mifumo ya Chelsea, Inter Milan na timu ya taifa ya Ubelgiji. Prosper ameenda mbali zaidi kwa kuangalia aina ya pasi ambazo Lukaku anapokea pia maeneo anayokaa ili kupokea pasi. Episode hii imeelezea kila kitu kuhusu Romelu Lukaku.
2/22/202213 minutes, 9 seconds
Episode Artwork

Mikimbio ya Washambuliaji wa Simba SC

Bila shaka ulimsikia beki wa Mtibwa Sugar, Abdi Banda aliposema kwamba washambuliaji wa Simba ni rahisi kuwakaba. Je kauli hii inaukweli? Clifford Sangai amekutana na Prosper Bartalomew chini ya mti ili kuangazia na kuchambua kwa undani mikimbio ya washambuliaji wa Simba yaani Kagere, Mugalu na Bocco Usisite kushea na marafiki Episode hii Pia unaweza kupakua majarida yetu BURE kuhusu AFCON: https://sportscasttz.gumroad.com/l/stajt https://sportscasttz.gumroad.com/l/jbxud
2/1/202216 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Arsenal: 'Pattern' ya ushambuliaji

Hawakuanza msimu vizuri lakini hivi karibuni inaonekana kama gari limewaka.  Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia wapi Arsenal walikuwa wanakwama pamoja na vitu ambavyo Mikel Arteta ameviongeza ili kuongeza ubora katika safu ya ushambuliaji.  Tumegusia pia patnership ya Xhaka na Partey inavyowasaidia katika kufanya mashambulizi. Katika episode hii tumegusia mbinu za Mikel Arteta kwa undani zaidi, usisite kuisikiliza hadi mwisho. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
1/11/202219 minutes, 48 seconds
Episode Artwork

Kufeli na kufaulu kwa Viungo wa Simba na Yanga

Watani hawa wa jadi wametuonesha mambo mengi katika mechi mbili walizokutana, kuanzia maswala ya ufundi hadi mbinu za makocha wao na hapo ndipo Clifford Sangai anapojadiliana na Prosper Bartalomew kuhusu timu hizo. Tumeangazia eneo moja muhimu sana kwa timu zote mbili nalo ni Safu ya Viungo ambapo kila timu imeonesha ubora na madhaifu yake na kama yanaweza kusahihishwa. Unataka kujua madhaifu hayo basi sikiliza episode hii
12/14/202121 minutes, 27 seconds
Episode Artwork

Azam FC: Msimu mpya mambo yale yale

Msimu mpya huu, unaona mabadiliko yoyote ndani ya kikosi cha Azam FC? Swali hilo ndio limemfanya Clifford Sangai aketi chini pamoja na Prosper Bartalomew kujadili mambo mbalimbali hususani ya kimbinu katika kikosi cha Azam FC. Tumeangazia namna timu inavyojilinda hadi inavyoshambulia huku tukilinganisha na msimu uliopita. Hatujaangazia mechi za Ligi Kuu Tanzania bara tu bali michuano yote ambayo Azam FC imeshiriki. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
12/9/202122 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Manchester United Special

Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia kwa kina wapi Ole Gunnar Solskjær alikwama kimbinu, tumezichambua kwa kina mbinu za raia huyo wa Norway kwa kuzingatia washindani wake kimbinu. Pia tumegusia mambo ambayo kocha wa muda wa Manchester United, Michael Carrick ameyabadili katika kikosi hicho kwa muda mfupi aliopo. Wakati tunarekodi episode hii dili la Manchester United, Lokomotiv Moscow na Raph Ranginick limekamilika kwa asilimia kubwa hivyo unaweza ukasikiliza kumfahamu zaidi kocha huyo ikiwemo falsafa zake na yeye ni kocha wa aina gani, pia tutarajie nini kutoka kwake akiwa Manchester United. Unataka kujua wachezaji gani watafaidika na ujio wa Ranginick? Sikiliza episode hii.
11/29/202137 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Ligi Kuu Tanzania Bara: Mbinu na Ufundi Part 2

Huu ni mwendelezo wa pale tulipoishia katika episode iliyopita lakini mwendelezo huu ni wa kipekee zaidi. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuchambua mbinu na ufundi katika Ligi Kuu Tanzania Bara maarudu kama NBC Premiere League. Tumeangazia mwenendo wa timu nyingi zinapokutana na Yanga zimekuwa zikijaza wachezaji wengi katika eneo la kiungo (Midfield overload) je kuna faida yoyote inayotakana na mbinu hiyo? Kibwana Shomari ameanza kuonesha mabadiliko makubwa sana katika matumizi ya mguu wake wa kushoto, Prosper amechambua style ya uchezaji wake na namna alivyokuwa hatari dhidi ya wapinzani wake. Ibrahim Ajibu Migomba anaweza pata nafasi ya kudumu katika kikosi cha Simba kwa sasa? Sikiliza episode hii kisha utupe maoni yako. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
11/7/202130 minutes, 17 seconds
Episode Artwork

Ligi Kuu Tanzania Bara: Mbinu na Ufundi Part 1

Bado unaamini Ligi Kuu Tanzania bara haina mbinu? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili mbinu za makocha mbalimbali na ufundi wa wachezaji katika Ligi Kuu ya NBC. Je kocha wa Yanga ameshaonesha mfumo wake rasmi katika kikosi chake? Ipi ni nafasi inayomfaa Bwalya awapo uwanjani? Hayo ni kati ya maswali tuliyojadili bila kusahau ubora wa Chirwa na Lusajo na mabadiliko ya kimfumo katika kikosi cha Namungo. Bila shaka jina Abdul Sopu umewahi kulisikia katika story mbalimbali za michezo lakini unajua yeye ni Kiungo wa aina gani? Vipi kuhusu Ramadhan Chombo (Redondo)? Sikiliza episode hii Prosper amechambua kwa kina mambo yote hayo. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
10/22/202137 minutes
Episode Artwork

Mbinu zilizotrend katika ligi tano bora barani Ulaya. Part 2

Kila siku makocha katika vilabu mbalimbali barani Ulaya wamekuwa wakitafuta kila namna ya kuweka vikosi vyao sawa na kuhakikisha falsafa zao zinaonekana vizuri. Ili kuhakikisha hayo yote yanatimia basi tumekuwa tukishuhudia mbinu mbalimbali za soka na hapo ndipo Clifford Sangai anapoketi na Prosper Bartalomew kuchambua timu mbalimbali pamoja na mwenendo wa timu hizo. Tumeangazia mabadiliko aliyoyafanya Mikel Arteta katika kikosi chake cha Arsenal hali iliyopelekea yeye kuwa kocha bora wa mwezi. Pia tumeangazia jukumu analopewa Christiano Ronaldo katika kikosi cha Manchester United bila kusahau ubora wa Napoli chini ya Spalleti. Prosper ametufafanulia takwimu mbalimbali kama PPDA, High Turnovers, nk pamoja na umuhimu wake katika soka la kisasa. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
10/11/202138 minutes, 18 seconds
Episode Artwork

Martin Ødegaard ni suluhu kwa matatizo ya Arsenal?

Tuliwahi kuongelea kuhusu kukosekana kwa kiungo mshambuliaji katika kikosi cha Arsenal kwenye Podcast hii. Sasa Arsenal chini ya Arteta imemsajili kiungo Martin Ødegaard kutoka Real Madrid. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili kama Ødegaard ataleta ahueni katika eneo la kiungo mshambuliaji. Ødegaard aliweza kuwashawishi mashabiki kipindi yupo kwa mkopo? Takwimu zake zinasemaje klabuni hapo? Je ni chaguo muhimu kwa Arsenal?. Basi sikiliza episode hii. Tumeangazia pia kama Mikel Arteta anaweza kutumia tena mfumo wa 3-4-3 ambao ulimpa mafanikio kipindi anaichukua timu. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
9/23/202123 minutes, 41 seconds
Episode Artwork

Tofauti ya Joshua Kimmich na Trent Alexander-Arnold

"Kwanini umchezeshe beki bora wa kulia duniani katika nafasi ya kiungo?" - Jürgen Klopp Kumeibuka maswali mengi sana tangu kocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate alipomtumia beki wa kulia wa Liverpool Trent Alexander-Arnold kama kiungo katika mechi dhidi ya Andorra huku wengine wakijaribu kumfananisha beki huyo na Joshua Kimmich. Clifford Sangai amekaa chini na Prosper Bartalomew kuchambua kwa kina utofauti uliopo baina ya wachezaji wawili, tukiangazia hasa ubora na mapungufu yao katika nafasi mbalimbali wanazocheza. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
9/20/202117 minutes, 34 seconds
Episode Artwork

Soka Langu: Francis Baraza

Katika mfululizo huu mpya wa episodes za 'Soka Langu', tutaongelea maswala ya mbinu na aina ya soka la wachezaji pamoja na makocha mbalimbali. Clifford Sangai anakaa chini na Prosper Bartalomew pamoja na Francis Baraza, kocha wa timu ya Kagera Sugar kujadili aina na mbinu za soka ambazo amekuwa akizitumia. Baraza anatupitisha katika safari yake ya ukocha tangu akiwa katika klabu ya Biashara United akitufafanulia baadhi ya maamuzi ya kiufundi aliyowahi kuyafanya. Kocha huyo wa Kagera Sugar ametueleza kwanini anapendelea wachezaji ambao hawana majina pia amegusia matumizi ya mfumo wa 3-4-3. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
9/13/202149 minutes, 5 seconds
Episode Artwork

Mbinu zilizotrend katika ligi tano bora barani Ulaya. Part 1

SportsCast imekuandalia uchambuzi wa ligi kuu tano bora barani ulaya tukiangazia hasa mechi za awali kabla ya mapumziko kwa ajili ya timu za taifa (International Break) Kama kawaida Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kudadavua mbinu za makocha mbalimbali na Wachezaji walioonesha viwango katika hatua za awali. Tumegusia mbinu ya Manchester city ilivyofeli katika mechi za mwanzoni kabisa msimu huu. Pia tumeangalia kikosi cha Real Madrid chini ya Carlo Ancelloti kama kuna mabadiliko yoyote. Pia Prosper ametaja orodha ya makocha wanaopaswa kuangaliwa kwa umakini katika Ligi Kuu nchini Ufaransa, pia ameelezea ubora wa Jose Mourinho na Julian Naglesmann. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
9/4/202141 minutes
Episode Artwork

Je, Tottenham na Manchester City zinaweza kucheza bila mshambuliaji wa kati?

Pep Guardiola amekuwa na mtindo kwa kucheza bila mshambuliaji wa kati katika mechi nyingi. Nini sababu ya maamuzi hayo? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili kama timu inaweza cheza msimu mzima bila kuwa na mshambuliaji wa kati. Tumetumia klabu ya Tottenham Hotspur na Manchester City kama mfano tukiangazia mbinu za makocha wa klabu hizo. Umuhimu wa Harry Kane kwa Spurs hususani katika mawanda ya kiufundi umejadiliwa kwa kina katika episode hii. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
8/18/202124 minutes, 20 seconds
Episode Artwork

Namna Utatu wa PSG utakavyoweza kutimiza ndoto za Klabu hiyo

Timu zilizopata mafanikio zaidi zimekuwa zikitumia washambuliaji watatu eneo la mbele na mara nyingi mfumo unaotumika 4 3 3. Tumeshuhudia utatu wa BBC (Bale, Benzema na Christiano) katika klabu ya Real Madrid, pia utatu wa MSN (Messi, Suarez na Neymar) wakati wapo Barcelona, bila kusahau utatu wa Liverpool wenye Salah, Firmino na Mane. Lakini je nini siri ya Utatu wa timu hizi kuweza kupata mafanikio zaidi? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuuchambua utatu wa PSG (Mbappe, Messi na Neymar) na namna wanavyoweza kuja kutimiza malengo ya klabu. Klabu ya Paris Saint-Germain imetimiza miaka 51 tangu ianzishwe. Licha ya kutawala katika Ligi ya ndani, klabu hiyo haijwahi kutwaa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Nasi tumeamua kugusia watu kama Di Maria na Wijnaldum ambao wanaweza kuisaidia timu hiyo ili kuweza kuwa tishio zaidi Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
8/14/202134 minutes
Episode Artwork

Mwenendo wa Usajili katika Ligi Kuu Tanzania Bara

Kuna madhara au faida gani timu inaposajili wachezaji wengi kutoka katika taifa moja?,Je makocha wana mchango gani wakati wa dirisha la usajili kwenye vilabu vyetu? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew pamoja na Michael Mwebe kuangazia kwa undani mwenendo wa usajili katika Ligi Kuu Tanzania Bara ili kujibu maswali hayo hapo juu na mengine mengi. Tumeangazia kwanini vilabu vyetu vimekuwa vikitupia macho washambuliaji kutoka DR Congo na ubora wao wanaoungeza wawapo kwenye kikosi. Katika usajili kitengo cha Skauti ni muhimu sana lakini je klabu zetu zinachunguzaje wachezaji ili waweze kuwasajili? Michael Mwebe ametupa uzoefu wake. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09 Jiunge nasi katika mtandao wa Clubhouse: https://www.clubhouse.com/club/sportscast
8/8/20211 hour, 5 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

VPL: Mbinu zilizotawala katika msimu wa 2020/21

Tumeshuhudia mambo mengi sana katika ligi kuu Tanzania bara lakini sisi SportsCast tumeamua kukuletea uchambuzi wa mbinu zilizotawala katika msimu huu. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili mbinu mbalimbali za makocha wa vilabu vya soka katika ligi kuu. Tumeangazia ubora wa wachezaji katika kila nafasi tukianza na magoli kipa hadi washambuliaji wa kati. Tumegusia namna timu mbalimbal zinavyoanza mashambulizi kutokea nyuma kupitia kwa mabeki wao wa kati na mapungufu ya namna hiyo ya kuanzisha mashambulizi. Ubora wa Clatous Chama nao hatujaufumbia macho kwani tumechambua mchango wake katika safu ya kiungo ya Simba na namna timu nyingine zinavyotamani kuwa na kiungo kama yeye. Tumeongelea kwanini mfumo wa 4-2-3-1 umetumika sana katika ligi kuu msimu huu huku tukiangazia kwa undani timu zilizotumia mfumo huo. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09 Jiunge nasi katika mtandao wa Clubhouse: https://www.clubhouse.com/club/sportscast
7/24/20211 hour, 1 minute, 14 seconds
Episode Artwork

EURO 2020: Mabadiliko ya kimbinu na athari zake katika mechi ya fainali

Gareth Southgate alianza mechi ya fainali ya EURO 2020 na mfumo wa mabeki watatu lakini katika dakika ya 70 alibadili kwenda mfumo wa mabeki wanne. Tangu michuano hii ianze Southgate ametumia mifumo miwili tu; 3-4-3 na 4-2-3-1huku kila mmoja ukiwa na faida na hasara zake. Lakini mabadiliko ya kimbinu katika mechi ya fainali dhidi ya Italy yalileta madhara gani katika kikosi cha England? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kudadavua mbinu zilizotumika na England na namna zilivyowarudisha nyuma. Kadhalika tunaungana na George Job ambaye anatuelezea namna Italia walivyoweza kuukwepa mtego wa England kupitia viungo wao, Jorginho na Veratti. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09 Jiunge nasi katika mtandao wa Clubhouse: https://www.clubhouse.com/club/sportscast
7/12/202133 minutes, 33 seconds
Episode Artwork

EURO 2020: Namna Viungo walivyoamua mechi za nusu fainali

Kama ulikuwa ukidhani 'Referee' ndiye mwamuzi pekee wa mechi basi alipata wasaidizi katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya EURO 2020. Wasaidizi hao si washika vibendera bali ni viungo wa timu zote nne; Italy, Spain, England na Denmark. Viungo hao walishiriki kwa sehemu kubwa timu zao kupata matokeo katika nusu fainali. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili ufanisi wa safu za viungo katika timu zote nne. Pia tunaungana na Geoffrey Lea kujadili maamuzi ya Southgate juu ya Bukayo Saka na Sancho kadhalika na ubora wa Harry Kane. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09 Jiunge nasi katika mtandao wa Clubhouse: https://www.clubhouse.com/club/sportscast
7/8/202134 minutes, 58 seconds
Episode Artwork

EURO 2020: Kwanini timu nyingi zimetumia upande wa kushoto kufanya mashambulizi?

Hatua ya robo fainali ya michuano hii ya EURO 2020 imekuja na mbinu mpya ambayo baadhi ya timu zimeitumia. Italy, England, Denmark, ni kati ya timu zilizotumia upande wa kushoto kufanya mashambulizi. Ni kwanini timu hizo zimetumia upande huo? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujibu swali hilo. Pia tumeangazia mbinu nyingine zilizotumika katika hatua hii ya robo fainali. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09 Jiunge nasi katika mtandao wa Clubhouse: https://www.clubhouse.com/club/sportscast
7/4/202132 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Namna mabadiliko ya wachezaji yalivyoathiri mifumo ya timu katika raundi ya 16 bora

Raundi ya 16 bora katika michuano ya EURO 2020 tumeshuhudia namna mabadiliko ya wachezaji yalivyoathiri mifumo ya timu mbalimbali. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia mabadiliko hayo pamoja na athari zake katika timu zote kwenye hatua hii. Tumeangazia mbinu zilizotumika katika mechi zote nane za hatua hii huku tukihusisha na takwimu ili kupima ubora wa nafasi zilizotengenezwa. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09 Jiunge nasi katika mtandao wa Clubhouse: https://www.clubhouse.com/club/sportscast
6/30/202141 minutes, 52 seconds
Episode Artwork

EURO 2020: Ubora na ufanisi wa mbinu za Makocha katika raundi ya tatu

Raundi ya tatu ya michuano ya EURO 2020 imekua ya kuvutia kutokana na baadhi ya timu kusaka matokeo ili zifuzu katika hatua inayofuata. Makocha wametumia ufundi na mbinu zao ili kuhakikisha timu zao zinapata matokeo wanayohitaji. Mabeki wa kulia kutumika upande wa kushoto, mabeki wa pembeni kucheza kama mabeki wa kati ni kati ya mbinu zilizotumika katika raundi hii. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili ubora na ufanisi wa mbinu zilizotumika na makocha mbalimbali katika raundi ya tatu ya michuano hii. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09 Jiunge nasi katika mtandao wa Clubhouse: https://www.clubhouse.com/club/sportscast
6/24/202143 minutes, 40 seconds
Episode Artwork

EURO 2020: Mbinu gani zimetawala katika raundi ya pili?

Mbinu mbalimbali za Makocha ndio zimeamua matokeo ya mechi nyingi katika raundi ya pili ya michuano ya EURO 2020. Lakini ubora wa mchezaji mmoja mmoja pia umesaidia kupata matokeo kwa timu fulani kama ambavyo George Job anavyoangazia ubora wa wachezaji katika kikosi cha Italia. Pia tumeungana na Geoffrey Lea kuangazia ubora wa mfumo wa kikosi cha England pamoja na mbinu za mwalimu Southgate. Unapoongelea raundi ya pili huwezi acha kuitaja mechi ya Germany vs Portugal ambayo ilikuwa ikitazamwa sana na hapo tumeungana na George Ambangile kujadili maamuzi ya kocha wa Ureno na ubora wa kikosi cha Ujerumani. Kadhalika hatujaacha takwimu nyuma, Prosper Bartalomew anatupitisha katika takwimu zote za mchezo ili kupima ubora wa nafasi za magoli zilizotengenezwa katika raundi hii. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09 Jiunge nasi katika mtandao wa Clubhouse: https://www.clubhouse.com/club/sportscast
6/20/20211 hour, 9 seconds
Episode Artwork

EURO 2020: Tulichojifunza katika mechi za raundi ya kwanza.

Timu kutumia mfumo wa 3-4-3, mabadiliko ya mifumo, ubora wa Robertson ni kati ya mambo yaliyovutiwa watu wengi katika mechi za ufunguzi wa michuano hii. Lakini si hayo tu ambayo tunaweza kujifunza kutokana na mechi za kwanza kama ambavyo Prosper Bartalomew anavyochambua mechi zote 12 za kwanza. Tumegusia takwimu mbalimbali ili kupima ubora wa nafasi za magoli zilizotengenezwa katia raundi ya kwanza. Pia tumejadili kama uwepo wa mashabiki katika baadhi ya viwanja kumeathiri maamuzi au matokeo ya mechi fulani. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09 Jiunge nasi katika mtandao wa Clubhouse: https://www.clubhouse.com/club/sportscast
6/16/202141 minutes, 49 seconds
Episode Artwork

Ubora na Mapungufu ya kila kikosi kuelekea EURO 2020

Vikosi vya timu zinazoshiriki EURO 2020 vimeshathibitishwa na kila kocha ametetea maamuzi yake. Je, unajua ni kwanini makocha wameamua kuita wachezaji fulani na kuwaacha wengine? Tumekuandalia majibu yote hayo. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili ubora wa kila kikosi kuelekea michuano ya EURO 2020. Tumeangazia timu zinazopigiwa upatu kutwaa taji hili kama Ufaransa, Ureno, Ubelgiji, nk. Tumeenda mbali zaidi kwa kuchambua timu ambayo inaweza leta 'Suprise' katika michuano hii kutokana na ubora wa kikosi chao. Pia tumejadili Kukosekana kwa Ramos katika kikosi cha Hispania na sababu ya maamuzi hayo na Thomas Muller na Mats Hummels kujumuishwa katika kikosi cha Ujerumani. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
6/5/202151 minutes, 8 seconds
Episode Artwork

Champions League: Tutarajie nini katika mechi ya fainali?

Ikiwa ligi mbalimbali zimefika tamati barani Ulaya mashabiki na wapenzi wengi wa soka wanaisubiri kwa hamu mechi ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya. Hii ni mara ya tatu kwa Chelsea kutinga katika hatua hii huku Manchester City ikiwa ni mara yao ya kwanza. Lakini tutarajie nini katika mechi hii ya kuvutia? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalome kuchambua timu zote mbili zilizotinga fainali ya UEFA Champions League msimu huu. Tumeangazia kila idara kuanzia ulinzi hadi ushambuliaji huku tukitumia takwimu za soka. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
5/25/202152 minutes, 46 seconds
Episode Artwork

Mambo usiyoyajua katika ligi kuu tano bora barani Ulaya msimu huu (2020/21)

Timu gani imetengeneza nafasi zenye ubora wa hali ya juu msimu huu? Na ubora wa hizo nafasi unapimwaje? Hayo ni kati ya maswali ambayo wadau wengi wa soka wamekuwa wakijiuliza katika kipindi hiki ambacho takwimu mbalimbali zimekuwa zikitumika katika kupima ubora wa timu mbalimbali. Katika msimu huu wa mwaka 2020/21 timu nyingi barani ulaya zimeweza kuonesha ubora katika nyanja mbalimbali kwenye ligi zao. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia timu gani ilikuwa bora msimu huu kwa kutumia takwimu katika ligi kuu tano bora barani Ulaya. Pia tumeelezea takwimu hizo zinamaanisha nn katika soka na namna ambavyo zinaweza kutumika na timu au vitengo vya skauti ili kuweza kufanya maamuzi. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
5/21/202152 minutes, 22 seconds
Episode Artwork

Namna timu iliyopanda daraja inavyoweza kusalia katika ligi kuu (VPL)

Tumeshuhudia timu nyingi zinazopanda daraja katika ligi kuu Tanzania bara (VPL) zikitetereka lakini vipi kuhusu timu ambazo hazitetereki katika msimu wa kwanza VPL? timu nyingi zinazopanda daraja katika ligi kuu Tanzania bara (VPL) zikitetereka lakini vipi kuhusu timu ambazo hazitetereki katika msimu wa kwanza VPL? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew pamoja na Thierry Hitimana aliyewahi kuwa kocha wa Namungo na Mtibwa kujadili namna timu zilizopanda daraja zinavyoweza kusalia ligi kuu. Hitimana anatupa uzoefu wake wa kipindi alipoipandisha daraja klabu ya Namungo pia anatueleza namna klabu iliyopanda daraja inavyoweza kukabiliana na timu kubwa katika mechi za ligi. "Ukitaka kupata sifa ipatie kwa mtu mkubwa" - Thierry Hitimana Tumechambua kwa undani mwendendo wa matokeo wa timu zilizopanda daraja katika misimu mitatu iliyopita. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
5/13/202133 minutes, 47 seconds
Episode Artwork

Namna umahiri wa Conte ulivyoipaisha Inter Milan

Mafanikio ambayo klabu ya Inter Milan imeyapata msimu huu yanatokana na mipango ya muda mrefu ya uongozi wa klabu hiyo iliyo chini ya kampuni ya Suning. Kati ya uamuzi bora uliofanywa na klabu hiyo ni kumpa kibarua Antonio Conte cha kukinoa kikosi cha timu hiyo. Conte alianza kibarua hicho huku akipata changamoto mbalimbali za kiufundi kutokana na kukosa wachezaji kadhaa kutoendana na falsafa yake. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew pamoja na Edgar Kibwana kujadili namna Antonio Conte alivyoonyesha umahiri wake kukabiliana na changamoto zote za kiufundi katika Klabu ya Inter Milan. Tumeangazia mfumo wake wa 3-5-2 na wachezaji ambao wameonesha kiwango cha hali ya juu. Pia tumeangazia namna uongozi wa klabu ulivyoshirikiana na kocha licha ya kuwa na mikwaruzano ya hapa na pale. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
5/7/202144 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Champions League: Tutarajie nini katika mechi za marudiano nusu fainali?

Nusu fainali ya UEFA imekua ya kusisimua zaidi katika raundi ya kwanza huku ikiacha maswali mengi ya kimbinu. Je, Zidane atarudi kwenye mfumo wake wa 4-3-3 aliouzoea ama atasalia na 3-5-2 dhidi ya Chelsea? Kikosi cha PSG kitakuwa na sura gani kitakapomkosa kiungo Idrissa Gueye katika mechi ya marudiano? Hayo ni kati ya maswali ambayo tumeyajadili kwa kina huku tukijumuisha mbinu za makocha wote wanne waliopo katika hatua hii ya nusu fainali. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
4/29/202127 minutes, 17 seconds
Episode Artwork

Mbinu anazotumia Solksjaer katika safu yake ya ushambuliaji

"Ubora wa kocha ni pamoja na kujua mapungufu yako"- Geoffrey Lea Solksjaer ameonekana kuwa katika safari ya mafanikio tangu alipopata kibarua cha kuinoa Manchester United. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew pamoja na Geoffrey Lea kujadili ubora na mapungufu ya safu ya ushambuliaji katika kikosi cha Manchester United. Tumeangazia pia mchango wa mabeki wa pembeni kama Luke Shaw na Wan Bissaka katika kufanya mashambulizi. Umaridadi wa Marcus Rashford hatukuufumbia macho, tumeangazia maeneo ambayo mchezaji huyu akicheza anakuwa katika kiwango cha juu. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
4/22/202150 minutes, 35 seconds
Episode Artwork

Siri ya mafanikio ya Simba katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika

Safari ya Simba SC. kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika imekua yenye mafanikio, lakini nini sababu ya mafanikio hayo? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew pamoja na Charles Abel kujadili mbinu zilizotumika na klabu ya Simba Pia tumeangazia mchango wa kimbinu Kocha Didier Da Rosa na namna anavyowatumia wachezaji mbalimbali kikosini. Tumechambua ubora na mapungufu ya safu ya ulinzi ya kikosi cha Simba na nini kifanyike ili kuongeza ubora katika safu hiyo. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
4/14/202128 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Sababu zinazopelekea mshambuliaji kupoteza ufanisi mbele ya goli

"Striker hupimwa kwa magoli" ni msemo uliozoeleka kwa mashabiki wengi wa mpira wa miguu, lakini itakuwaje kama mshambuliaji atapoteza ufanisi mbele ya goli? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew pamoja na Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa na Klabu ya Yanga Ally Mayay Tembele kujadili sababu zinazopelekea kupungua kwa ufanisi wa washambuliaji. Tumeangazia kwa undani mwenendo wa wachezaji kama Timo Werner, Michael Sarpong, Ditram Nchimbi na Mbwana Samatta. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
4/9/202146 minutes, 47 seconds
Episode Artwork

Ni Cristiano Ronaldo ama Andrea Pirlo?

Nani anapaswa kulaumiwa kwa mwenendo wa sasa wa Juventus? Je uamuzi wa kumchagua Andrea Pirlo kukinoa kikosi cha Juve ulikuwa sahihi? Cristiano Ronaldo anafiti kwenye Falsafa za Andrea Pirlo? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew pamoja na Mchambuzi George Job kuangazia kwa kina matatizo yanayoisibu klabu ya Juventus. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
3/30/202137 minutes, 22 seconds
Episode Artwork

Nini suluhu ya matatizo yanayoikumba Yanga?

Matatizo ya umaliziaji na Timu kukosa muunganiko ni kati ya matatizo makubwa yanayoikumba klabu ya Yanga chini ya kocha Cedric Kaze. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili kwa kina matatizo hayo na namna ya kuyatatua. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
3/5/202140 minutes, 47 seconds
Episode Artwork

Namna Mbappé na Haaland wanavyojitengenezea ulimwengu wao wa soka

Wengi wamehusishwa kurithi ufalme wa Lionel Messi na Christiano Ronaldo lakini hawakuweza kufikia kiwango chao. Je, Kylian Mbappé na Erling Braut Haaland wataweza kufikia kiwango cha Messi na Ronaldo? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili namna makinda hawa wanavyotengeneza ulimwengu wao wa soka. Tunaangazia zaidi takwimu za mchezo na namna wanavyosaidia timu zao kuweza kupata matokeo. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
2/26/202128 minutes, 10 seconds
Episode Artwork

Je, Diego Simeone amebadili falsafa yake?

Diego Simeone amezoeleka kwa aina ya soka la kukaba na kufanya mashambulizi ya kushtukiza ila kwa sasa hali ni tofauti. Ongezeko la asilimia za umiliki wa mpira (Ball Possession) na mabadiliko ya 'formation' ni kati ya vitu vinavyowashangaza wengi kuhusu Atletico Madrid iliyo chini ya Diego Someone. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili kama kocha Diego Simeone amebadili falsafa yake. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
2/19/202135 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Matatizo ya kimbinu yanayoikumba Liverpool

Kukosekana kwa Van Djik kumemfanya Jurgen Klopp kubadili mbinu mbalimbali ili kuweza kukabiliana na pengo hilo. Mabadiliko hayo ya mbinu yamepelekea matatizo mengi kuanzia safu ya ulinzi, viungo na washambuliaji. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalome kujadili matatizo mbalimbali ya kimbinu yanayoikumba Liverpool chini ya Klopp. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
2/11/202132 minutes, 14 seconds
Episode Artwork

Guardiola amefanya mabadiliko gani baada ya kuanza msimu vibaya?

"Tulikua hatuchezi vizuri kwa sababu tulikua tunakimbia sana, kwenye mpira unabidi ukimbie kwa kiasi na kwa muda maalum" - Pep Guardiola. Manchester City ya sasa ni tofauti na ile ya mwanzo wa msimu huu wa 2020/21, mengi yamefanywa ili kuweza kupata ubora wa kikosi hicho kwa sasa. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia mabadiliko ambayo Pep Guardiola ameyafanya ili kuirudisha timu hiyo katika kuwania ubingwa msimu huu. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
2/2/202131 minutes, 23 seconds
Episode Artwork

Namna Stefano Pioli alivyoibadili AC Milan

Stephano Pioli ameifanya AC Milan kutoa ushindani katika ligi kuu nchini Italia maarufu kama 'Serie A' Uzoefu wake katika ligi hiyo umemuwezesha kuiongoza AC Milan kucheza mechi 29 bila kupoteza mchezo wowote. Tumeangazia mbinu alizotumia kuifanya AC Milan kucheza soka la kasi na lenye kuvutia zaidi. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
1/26/202136 minutes, 41 seconds
Episode Artwork

Kufeli na kufaulu kwa safu ya viungo wa Chelsea chini ya Lampard

Chelsea mara nyingi imekua ikipata magoli kwa kutegemea mipira ya krosi ambazo hupigwa na mawinga au mabeki wa pembeni. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew na Barnabas Gwakisa (Mr. Darajani) kujadili kufaulu na kufeli kwa safu ya viungo wa Chelsea chini ya Kocha Frank Lampard. Mfumo wa 4-3-3, nafasi anayopaswa kucheza Ngolo Kante, umuhimu wa Jorginho na ubora wa Kai Havertz ni kati ya mambo yaliyojadiliwa kwa kina katika Episode hii. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
1/12/202150 minutes, 12 seconds
Episode Artwork

Nini kinamfanya Meddie Kagere kuwa hatari zaidi mbele ya goli?

Umri ni namba, shughuli dimbani na Meddie Kagere tangu ametua katika ardhi ya Tanzania ameweza kuonesha shughuli nzito awapo uwanjani. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalome pamoja na Michael Mwebe kuchambua kwa kina aina ya soka ambalo Kagere hucheza pamoja na uwezo na mapungfu yake. Tumeenda mbali zaidi kwa kuangazia historia yake, umuhimu wake katika kikosi cha Simba na kulinganisha uwezo wake pamoja na washambuliaji wengine katika ligi kuu Tanzania Bara. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
1/5/202137 minutes, 57 seconds
Episode Artwork

Wachezaji wanaofanya vizuri ligi kuu Tanzania Bara

Katika mzunguko wa kwanza wa VPL wachezaji mbalimbali wameonesha umaridadi wao katika nafasi mbalimbali wanazocheza uwanjani. SportsCast imekuandalia orodha ya wachezaji watano (5) ambao kwa nafasi zao wameweza kuonyeshe ubora wa kimbinu na kuweza kusaidia katika falsafa za makocha wao. Orodha hii inahusisha wachezaji kama; Prince Dube, Edward Manyama, Adam Adam, Mukoko Tonombe na Clatous Chama. Sikiliza zaidi ili kuweza kujua ubora wa wachezaji hao huku tukiangazia mbinu Zaidi. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
12/26/202032 minutes, 27 seconds
Episode Artwork

Mabadiliko ambayo Koeman anayafanya ndani ya Barcelona

Kila kocha huja na mbinu na falsafa yake, Barcelona chini ya Ronald Koeman ni tofauti na ya makocha waliopita hususani katika namna wanavyocheza. SportsCast imeangazia mabadiliko ya kimbinu ambayo kocha huyo ameyaleta katika klabu ya Barcelona. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
12/19/202022 minutes, 37 seconds
Episode Artwork

Kwanini Arsenal imetengeneza nafasi chache za kufunga?

Arsenal ya msimu huu imekua ikitegemea krosi zaidi ili kufikisha mpira kwenye box la timu pinzani. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew ambaye anachambua kwa kina mbinu za Arsenal kwa msimu huu na kutoa ufafanuzi juu ya uhaba wa nafasi za kutengeneza magoli katika kikosi cha Mikel Arteta. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
12/13/202027 minutes, 57 seconds
Episode Artwork

Umuhimu wa Viungo katika mfumo wa Sven

Pira biriani la simba linachagizwa na umahiri wa viungo walio chini ya kocha Sven Vandenbroeck ambaye kupitia mfumo wake timu imeweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga na kumiliki mpira kwa asilimia kubwa. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia kwa kina umuhimu wa kila kiungo wa Simba ndani ya mfumo wa Sven. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
12/3/202026 minutes, 27 seconds
Episode Artwork

Nafasi ambayo Paul Pogba anapaswa kucheza

Je Bruno Fernandes amechukua nafasi ya Pogba uwanjani?, Inawezekana Pogba na Bruno wakafiti kwenye timu moja?. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujibu maswali hayo na kuangazia zaidi uwezo wa Paul Pogba katika nafasi mbalimbali pindi awapo uwanjani. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
11/23/202026 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Kuna haja ya kurejesha sub 5 EPL?

Utaratibu wa kufanya mabadiliko uwanjani kwenye ligi kuu Uingereza umehusishwa kuleta madhara mbalimbali kwa wachezaji. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili kwa kina madhara hayo kwa wachezaji na mapendekezo ya makocha mbalimbali. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
11/14/202017 minutes, 2 seconds
Episode Artwork

Mipango ya Cedric Kaze & Tatizo Sugu la Waamuzi

Je Kocha Cedric Kaze ameleta mabadiliko yoyote kwenye kikosi cha Yanga? Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuichambua kwa kina mipango Kaze ndani ya Yanga kadhalika pia tunaangazia kwa undani zaidi tatizo la waamuzi kushindwa kuhimili michezo katika Ligi Kuu Bara. Tufuate katika mtandao wa Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1s7jr9p0pao5 Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09
11/10/202028 minutes, 22 seconds
Episode Artwork

Namna Liverpool inavyokabiliana na pengo la Virgil Van Djik

Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kuangazia Liverpool iliyo chini ya Jurgen Klopp inavyokabiliana na pengo la Van Djik. Pia tumeangazia kwa kina mabeki ambao Liverpool inaweza kuwasajili ili kuziba pengo la Van Djik na Mfumo mpya ambao Klopp anautumia kwa sasa. Tufuate katika mtandao wa Twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09 Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=x07qr4cy41js
10/26/202023 minutes, 29 seconds
Episode Artwork

Champions League: Rashford ang'ara tena Paris & Madrid yaendeleza rekodi mbaya UEFA

UEFA Champions League imerejea tena kwa kishindo. Safu ya Ulinzi ya Manchester ikiwatia kibindoni Mbappe na Neymar, Frank Lampard aweka rekodi mpya Chelsea, Makinda wa Barcelona wang'ara mbele ya Messi, Mbinu za Simeone zagonga mwamba, Klopp afanya maamuzi magumu Amsterdam na Madrid msimu mpya mambo yaleyale. Uchambuzi wa kina wa yaliyojiri kwenye Champions League unaletwa kwenu na Clifford anayeungana na Prosper Bartalomew. Tufuate katika mtandao wa twitter: https://twitter.com/SportsCastTz?s=09, Instagram: https://instagram.com/sportscasttz?igshid=1x2gpz7tfqvsp
10/22/202022 minutes, 4 seconds
Episode Artwork

Namna gani Mikel Arteta ni tofauti na Pep Guardiola?

Arteta na Pep wanafanana katika nyanja mbalimbali lakini soka ndio limewaleta pamoja. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili historia za makocha hawa wawili kadhalika pia na utofauti wa mbinu wanazotumia katika timu wanazoziongoza.
10/19/202024 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Dirisha la Usajili: Man Utd, Arsenal, Liverpool, Everton, Barcelona & Bayern Munich.

Dirisha la usajili barani ulaya limekua la kuvutia sana, likihusisha wachezaji mbalimbali kujiunga na vilabu vikubwa barani Ulaya. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew kujadili namna vilabu barani ulaya vimetumia dirisha hili la usajili ili kuimarisha vikosi vyao na kuleta ushindani katika ligi zao. Tumeangazia dili la Cavani kwenda Manchester United, Partey kwenda Arsenal na Douglas Costa kwenda Bayern. Tufuate katika mtandao wa twitter @SportsCastTz
10/9/202044 minutes
Episode Artwork

Kwa namna gani Krmpotic alifeli kuiunganisha timu ya Yanga?

Krmpotic hana historia ya kukaa kwenye klabu kwa zaidi ya mwaka mmoja na amekua akilalamikiwa kwa namna anavyopanga kikosi chake. Clifford Sangai anaungana na Prosper Bartalomew ambaye anachambua kwa kina namna Krmpotic alivyofeli kuiunganisha timu ya Yanga.
10/4/202030 minutes
Episode Artwork

Manchester City; Msimu mpya mambo yaleyale & Sintofahamu ya Penati za 'Handball' EPL.

Hadi sasa  Manchester City imetumia kiasi cha Pauni milioni 400 kwa ajili ya safu ya ulinzi tangu kocha Pep Guardiola atue klabuni hapo lakini bado hakuna utofauti na wamekua wakiruhusu magoli ya aina ileile.  Sheria mpya ya 'Handball' imeleta sintofahamu nyingi hususani kwa mashabiki na makocha katika ligi kuu ya uingereza.  Clifford Sangai anaungana na mchambuzi Prosper Bartalomew kujadili maswala hayo.
10/1/202029 minutes, 3 seconds
Episode Artwork

SportsCast-Trailer

Ungana nasi mara mbili kwa wiki tukikuchambulia soka kwa namna ya kipekee kabisa.
9/30/20201 minute, 29 seconds