Winamp Logo
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii Cover
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii Profile

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Swahili, Political, 1 season, 46 episodes, 15 hours, 27 minutes
About
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Episode Artwork

Watatu wafa katika mlipuko wa gas jijini Nairobi Kenya, M23 waendeleza mapigano DRC

Miongoni ni pamoja na watu watatu wafariki dunia katika mlipuko wa gesi jijini Nairobi nchini Kenya, kundi la waasi wa Uganda wa ADF waendeleza mauaji ya raia wa kawaida nchini DRC,lakini pia yaliyojiri kwenye kanda ya Afrika Mashariki, Afrika magharibi na Mgomo wa wakulima nchini Ufaransa, hali ya Israeli na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.
2/3/202420 minutes, 7 seconds
Episode Artwork

Mvutano kati ya Kigali na Bujumbura, mauaji ya watu zaidi ya 10 Mwesso DRC

Yaliyojiri wiki hii inaangazia kauli ya rais wa Rwanda Paul Kagame kwamba ataitetea nchi yake kwa gharama yoyote ile, upinzani nchini Tanzania uliandamana kupinga mabadiliko ya sheria za uchaguzi, mauaji ya watu zaidi ya kumi mjini Mwesso mashariki mwa DRC, uchaguzi visiwani Komoro hali katika ukanda wa Afrika Magharibi lakini pia uchaguzi mdogo huko Marekani,
1/27/202420 minutes, 9 seconds
Episode Artwork

Kuapishwa kwa rais Felix Tshisekedi jumamosi, Rwana na UK njia panda bado

Makala hii imeangazia kuhusu kuapishwa rais wa DRC Félix Tshisekedi baada Mahakama ya katiba  kuidhinisha ushindi wake katika uchaguzi wa desemba 20, viongozi wa nchi wananchama wa IGAD walikutana jijini Kampala huku wakitoa wito wa kusitishwa mapigano Sudan, waziri mkuu wa Uingereza Richy Sunak na mpango wa kuwasafirisha waomba hifadhi huko Rwanda.
1/20/202420 minutes, 14 seconds
Episode Artwork

Mahakama ya katiba yaidhisha ushindi wa Tshisekedi, Burundi yafunga mpaka na Rwanda

Mahakama ya katiba huko DRC iliidhinisha ushindi wa rais Félix Tshisekedi,rais wa Uganda Yoweri Museveni awatahadharisha waasi wa ADF, Waziri mkuu wa Uingereza Richy Sunak akabiliwa na wakati mgumu kuhusu suala la kuwasafirisha waomba hifadhi huko Rwanda, yaliyojiri katika ukanda wa Afrika Mashariki, Afrika magharibi lakini pia uteuzi wa Gabriel Attal kuwa waziri Mkuu wa kwanza kijana nchini Ufaransa, mashambulio ya jeshi la Israeli yawaathiri raia wa kawaida mjini Gaza, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.
1/13/202420 minutes, 9 seconds
Episode Artwork

Dunia yakaribisha mwaka mpya, mvutano kati ya rais Ruto na idara ya mahakama

Miongoni mwa habari kuu za wiki hii ni pamoja na dunia kuukaribisha mwaka mpya 2024, mvutano kati ya rais wa Kenya William Ruto na idara za mahakama, wapinzani wa DRC waendelea kuonesha kutofurahishwa na ushindi wa rais Felix Tshisekedi kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa desemba 20 mwaka uliopita, yaliyotangazwa na CENI, yaliyojiri katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, Afrika magharibi lakini pia mashambulio mjini Gaza, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.
1/6/202420 minutes, 15 seconds
Episode Artwork

DRC: Rais Felix Tshisekedi ashinda uchaguzi kwa muhula wa pili

Baadhi ya habari ambazo tumeangazia ni matokeo ya uchaguzi nchini DRC ambapo Felix Tshisekedi ameshinda uchaguzi kwa muhula wa pili kwa asilimia 73.34, katika matokeo ya uchaguzi ambayo yametangazwa na Ceni Jumapili jioni. Tutaangazia pia mashambulio ya ADF kule Uganda lakini pia mkutano wa ana kwa ana kati ya majenerali wanaopigana Sudan ambao haukufanikiwa, hali kule Nigeria kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika jimbo la Plateau, Urusi kufungua tena ubalozi wake nchini Burkina Faso na ulimwenguni tutazidi kuangazia hali ya vita vya Gaza
12/31/202320 minutes, 1 second
Episode Artwork

Raia DRC wasubiri matokeo ya uchaguzi, Rais Biden amsuta Netanyahu kulinda raia

Kwenye makala yaliyojiri wiki hii, tumeangazia uchaguzi kule DRC wakati huu shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea, kikosi cha jumuiya ya Afrika Mashariki chaondoka rasmi nchini DRC, mapigano kule Sudan. Pia tumeangazia uhusiano wa kidiplomasia kati ya Ufaransa na Niger, pia siasa za Afrika Kusini na kwingineko ulimwenguni tumeangazia masaibu yanayomkabili Donald Trump lakini pia hali kule Gaza.
12/24/202320 minutes, 1 second
Episode Artwork

CENI uchaguzi utafanyika desemba 20 DRC, Uingereza kuhamishia wahamiaji Rwanda

Yaliyojiri wiki hii imeangazia hatua ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini DRC CENI kusisitiza kuwa  uchaguzi utafanyika desemba 20 kama ulivyopangwa; wakati huo huo aliyekuwa mwenyekiti wa CENI Corneille Nangaa alizindua chama kipya cha AFC Alliance Fleuve Congo, wabunge wa Uingereza walipiga kura kuunga mkono mpango wa kuwahamishia wahamiaji nchini Rwanda, siasa za Senegal, na huko Niger Mahakama ya ECOWAS yaamuru kuachiwa huru kiongozi aliepinduliwa nchini Niger Muhamed Bazoum, Jeshi la Israel laendeleza  mashambulio mjini Gaza, na pia matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.
12/16/202320 minutes, 15 seconds
Episode Artwork

CENI uchaguzi utafanyika desemba 20 DRC, Uingereza kuhamishia wahamiaji Rwanda

Yaliyojiri wiki hii imeangazia hatua ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini DRC CENI kusisitiza kuwa  uchaguzi utafanyika desemba 20 kama ulivyopangwa; wakati huo huo aliyekuwa mwenyekiti wa CENI Corneille Nangaa alizindua chama kipya cha AFC Alliance Fleuve Congo, wabunge wa Uingereza walipiga kura kuunga mkono mpango wa kuwahamishia wahamiaji nchini Rwanda, siasa za Senegal, na huko Niger Mahakama ya ECOWAS yaamuru kuachiwa huru kiongozi aliepinduliwa nchini Niger Muhamed Bazoum, Jeshi la Israel laendeleza  mashambulio mjini Gaza, na pia matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.
12/16/202320 minutes, 15 seconds
Episode Artwork

Rwanda na Uingereza zasaini mkataba kuhusu wahamiaji, jeshi la EAC laondoka DRC

Makala hii imeangazia hatua ya Rwanda na Uingereza kutiliana saini mkataba mpya kuhusu kuwahamisha wahamiaji kutoka Uingereza kupelekwa Rwanda, makumi ya watu wapoteza maisha katika mafuriko nchini Tanzania, kampeni za uchaguzi mkuu zashika kasi kuelekea desemba 20 huko DRC, Waasi wa M23 wazidisha Mapigano eneo la mashariki mwa DRC, hali ya siasa nchini Kenya, na mataifa mengine ya Afrika magharibi, lakini pia kongamano la Kimataifa kuhusu hali ya hewa waendelea Dubai kwenye Nchi ya Falme za kiarabu, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani...
12/9/202320 minutes, 15 seconds
Episode Artwork

Mkutano wa COP28, EU kuondoa waangalizi wake wa Uchaguzi huko DRC na mengineyo

Makala hii imeangazia mkutano wa kilele wa kimataifa kuhusu hali ya tabia nchi COP28 huko Dubai, kuachiwa kwa baadhi ya mateka waliokuwa wameshikilwia na Hamas huko Gaza, DRC ilisema muda wa Kuwepo kwa vikosi vya Jumuia ya EAC hautaongezwa baada ya desemba 08, Umoja wa Ulaya  waamua kusitisha mpango wa kuwasambaza waangalizi wake wa uchaguzi nchini DRC, siasa za Kenya, Tanzania, na mengine yaliyojiri kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, Afrika magharibi na kwengineko duniani.
12/2/202320 minutes, 14 seconds
Episode Artwork

Rais George Weah akubali kushindwa kwenye duru ya pili ya uchaguzi

Matukio kadhaa wa kadhaa yamefanyika ulimwenguni kukiwemo George Weah kukubali kushindwa katika duru ya pili ya uchaguzi nchini Liberia kwa Joseph Boakai. Hii ina maana atakuwa miongoni mwa marais waliohudumu kwa muhula mmoja.  Tutaangazia pia mafuriko yalivyoathiri nchi nyingi, Hali ya usalama na kisiasa nchini DRC, kadhalika Kenya kuidhinisha polisi kutumwa Haiti, tutaangazia uamuzi wa mahakama ya Uingereza kuhusu sera ya wahamiaji nchini Rwanda, kadhalika usalama Mali na chaguzi nchini Madagascar na hali halisi katika vita vinavyoendelea huko Gaza na pia tutaangazia mkutano kati ya Rais Joe Biden na Xi Jinping.
11/18/202320 minutes, 3 seconds
Episode Artwork

Burundi kuondoa wanajeshi wake DRC, Ufaransa na mkutano kuhusu Gaza

Makala ya Yaliyojiri wiki Hii, imeangazia hatua ya kikosi cha wanajeshi wa Burundi chini ya Jumuia ya Afrika Mashariki, EAC kujiondoa maeneo ya mashariki mwa DRC, mapigano kati ya jeshi la serikali ya DR Congo FARDC na waasi wa M23 mkowani Kivu kaskazini, hotuba ya rais wa Kenya wiki hii yazua hisia mseto, hali ya kibinadamu nchini Sudan yausikitisha Umoja wa mataifa, kongamano la Kimataifa kuhusu Gaza lafunguliwa nchini Ufaransa na mengine mengi duniani.
11/11/202320 minutes, 15 seconds
Episode Artwork

Zaiara ya mfalme wa tatu wa Uingereza, kukamatwa kwa muasi wa ADF Uganda

Makala ya wiki hii imeangazia matukio kadhaa yaliyojitokeza wiki hii kote ulimwenguni, miongoni ni pamoja na ziara ya mfalme Charles wa tatu wa Uingereza nchini Kenya, ambapo pia rais wa shirikisho la Ujerumani Frank-Walter Steinmeier kule Tanzania, hali ya kisiasa na kiusalama nchini DRC, mkutano kuhusu utalii barani Afrika ulitamatika jijini Kigali, nchini Rwanda, na matukio mengine yaliyoshuhudiwa kwenye ukanda huu na kwengineko duniani.
11/4/202320 minutes, 18 seconds
Episode Artwork

Ziara ya rais E. Macron huko Israel, mapigano mashari mwa DRC, siasa za Kenya

Makala hii imeangazia ziara ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron  huko Israeli, maombi kutaka bunge liidhinishe mpango wa kutumwa kwa askari wake elfu 1 nchini Haiti, hali ya kisiasa na usalama huko DRC, nchini Sudan, lakini pia hali tete ya kiafya ya kinara wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani. Ungana na mwanahabari wetu Ruben Lukumbuka kupata mengi zaidi
10/28/202320 minutes, 10 seconds
Episode Artwork

Mashambulio ya Gaza huko Israeli, siasa za DRC, Kenya na Burundi na mengineyo

Makala hii imeangazia ziara ya rais wa Marekani Joe Biden huko Israeli, kuuawa kwa watalii huko Uganda mpakani na DRC, siasa za Kenya na siku ya mashujaa iliyoadhimishwa oktoba 20, hali ya kisiasa na usalama huko DRC, Burundi na nchini Sudan lakini pia ziara ya rais wa Chad nchini Ufaransa, na matukio mengine mengi ya wiki hii duniani.
10/21/202320 minutes, 12 seconds
Episode Artwork

Mashambulio ya Hamas nchini Israel, siasa za DRC na ukanda wa Afrika mashariki

Miongoni mwa mengi yaliyoangaziwa katika makala ya juma hili ni pamoja na mashambulio yaliyofanywa na kundi la Hamas huko Israeli, siasa za Kenya, Uganda na Tanzania, kulegezwa kwa hali ya dharura iliyowekwa kwenye majimbo mawili ya Kivu kaskazini na Ituri huko DRC, hali ya Sudan na kuondoka kwa awamu ya kwanza ya wanajeshi wa Ufaransa nchini Niger, na mengineyo duniani.
10/14/202320 minutes, 14 seconds
Episode Artwork

Mwanasiasa wa upinzani Uganda Bobi Wine akamatwa, mauaji ya Sondu Kenya

Makala ya wiki hii imeangazia baadhi ya habari kuu za dunia matukio makubwa kama vile kukamatwa na kuwekwa katika kizuizi cha nyumbani kwa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine, ziara ya rais wa Kenya William Ruto magharibi mwa Nchi na kuwasilishwa kwa faili za wanasiasa wanaogombea urais katika ofisi za Tume ya uchaguzi nchini DRC, CENI, siasa na hali ya ukanda wa Afrika magharibi na kaskazini na kwengineko duniani.
10/7/202320 minutes, 8 seconds
Episode Artwork

Kenya, Uganda na Tanzania kuandaa Afcon 2027, Tshisekedi asema uchaguzi utafanyika tu

Katika makala hii tumeangazia baadhi ya habari kuu za dunia za wiki hii na miongoni ni pamoja na  Kenya, Uganda na Tanzania ziliteuliwa na shirikisho la soka Afrika CAF kuwa wenyeji wa mashindano ya kombe la Afrika mwaka 2027, DRC na Rwanda ziligubika mkutano wa Baraza la Umoja wa mataifa, balozi wa Ufaransa nchini Niger Sylvain Itté aliongea kwa mara ya kwanza kuhusu namna alivyofurushwa Niamey, Siasa za Marekani Israeli na kwengineko duniani ni miongoni mwa mengi tumekuandalia
9/30/202320 minutes, 13 seconds
Episode Artwork

Mkutano wa 78 wa umoja wa mataifa, rais wa DRC aitaka Monusco kuondoka DRC

Makala hii imeangazia hotuba za viongozi wa Afrika katika baraza la Umoja wa mataifa huko Newyork Marekani,rais wa zamani wa jamhuri ya Afrika ya kati ahukumiwa kifungo cha maisha jela, Ecowass na hali ya nchini Niger, ziara ya Mfalme wa 3 wa Uingereza nchini Ufaransa lakini kiongozi wa Kanisa katoliki Papa Francis kule Marseilla Ufaransa, na mengine mengi.
9/23/202320 minutes, 11 seconds
Episode Artwork

Mafuriko nchini Libya tetemeko la ardhi nchini Morocco, na siasa za DRC

Makala hii inaangazia hali inavyoendelea huko Libya baada ya mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu idadi ya vifo kutokana na Tetemeko la ardhi huko Morocco yaendelea kuongezeka, aliyekuwa mshirika wa karibu wake rais wa DRC Félix Tshisekedi na naibu spika wa bunge Jean Marc Kabund ahukumiwa kifungo cha miaka 7, tutaangazia hali ya kisiasa na kijamii nchini Kenya, Tanzania lakini pia ziara ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UN huko Urusi pamoja na mambo mengine.
9/16/202320 minutes, 18 seconds
Episode Artwork

Zaidi ya watu 600 wamefariki kutokana na tetemeko la ardhi nchini Morocco

Tetemeko kubwa la ardhi siku ya Ijumaa usiku limeitikisa nchi ya Morocco wakati huu zaidi ya watu 600 wakiafriki, kwa mujibu wa takwimu za wizara ya mambo ya ndani, idadi hii ikihofiwa kuendelea kuongezeka. Tetemeko hilo la ukubwa wa 6.8 lilipiga kilomita 72 kusini magharibi mwa eneo la watalii la Marrakesh, Utafiti wa Jiolojia wa Marekani umeripoti.Tetemeko pia ilisikika katika miji ya pwani ya Rabat, Casablanca na Essaouira.
9/9/202320 minutes, 1 second
Episode Artwork

Mapinduzi Gabon, moto Afrika Kusini, siasa na usalama DRC na masaibu ya Trump

Mambo ambayo yamegonga vichwa vya habari ni pamoja na mapinduzi ya Gabon na kiongozi kuteuliwa amabye anatarajiwa kuapishwa Jumatatu ya Septemba 4, pia tuaangalia mapinduzi katika nchi jirani ya Niger, vilevile kisa cha kusikitisha cha moto nchini Afrika Kusini uliogharimu maisha ya zaidi ya watu 70. Kadhalika tutaangalia kuteuliwa kwa rais wa DRC Felix Tschisekedi kupeperusha bendera ya cha UPDS katika uchaguzi wa Disemba na tunavuka Tanzania ambapo rais Samia Suluhu alifanya mabadiliko katika baraza lake na kusema kuwa hatua hiyo si adhabu.
9/2/202320 minutes
Episode Artwork

Matukio ya wiki hii, kifo cha kiongozi wa wagner, siasa za DRC, Kenya, na kwengineko

Makala ya Yaliyojiri wiki hii,imeangazia kuenea kwa taarifa ya kifo cha mtu anayedaiwa kuwa kiongozi wa kundi la mamluki wa Wagner Yevgeny Prigozhin, mkutano wa Brics huko Johannesburg Afrika kusini, siasa za Kenya, DRC, matukio ya kule Uganda, uchaguzi wa Gabon, pia hali inavyoendelea Niger na kwengineko duniani
8/26/202319 minutes, 58 seconds
Episode Artwork

Hali ya dharura mashariki ya DRC, siasa za Kenya, Niger na kwengineko

Tathmini juu ya hali ya dharura iliyotangazwa na rais wa DRC Felix Tshisekedi kwenye mikowa ya Kivu kaskazini na Ituri, Siasa za Kenya, kukamatwa kwa Dokta Slaa mwanasiasa mkongwe wa nchini Tanzania, Hali ya huko Sudan, Niger na kwengineko duniani. Kupata mengi zaidi, ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka
8/19/202320 minutes, 3 seconds
Episode Artwork

Taasisi za kimataifa zasikitikia mazingira anayozuiliwa Mohamed Bazoum

Tumekuandalia mengi tu ikiwemo mazungumzo kati ya serikali na upinzani yalioaanza kule nchini Kenya, siasa na maandalizi ya uchaguzi mkuu huko nchini DRC na mengine mengi tu.
8/12/202320 minutes, 2 seconds
Episode Artwork

Juhudi za kimataifa na za kikanda zaendelea kurejesha Bazoum Niger

Makala hii imeangazia juhudi za kikanda na za kimataifa kuendelea ili kulaani mapinduzi ya kijeshi nchini Niger na kutaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia, Umoja wa mataifa ulikaribisha hatua ya Kenya kukubali kuongoza kikosi cha ulinzi huko Haiti, Siasa za DRC kuelekea Uchaguzi wa desemba 20, Sudan na kwengineko duniani, kwa hayo na mengine mengi ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka
8/5/202320 minutes, 9 seconds
Episode Artwork

Mapinduzi ya kijeshi nchini Niger, mkutano wa Wakuu wa Afrika na Urusi

Makala hii imeangazia mkutano wa viongozi wa Afrika na Urusi huko St Petersburg, Urusi, mapinduzi ya Niger, mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kule Daresalaam nchini Tanzania, upinzani wa Kenya ulitangaza kusitisha maandamano, Siasa za DRC na ufunguzi wa michezo ya Francophonie, hali ya Sudan na matukio mengine duniani.
7/29/202320 minutes, 5 seconds
Episode Artwork

Maandamano ya upinzani nchini Kenya, DRC mauaji ya Okende yalipangwa asema Ambongo

Makala hii imeangazia kuhusu maandamano yaliyoitishwa na wapinzani nchini Kenya, ziara ya rais wa Hungary nchini Tanzania, lakini pia uchunguzi kuhusu mauaji ya Cherubin Okende, mwanasiasa mshirika wa karibu wake Moise Katumbi, aliyeuawa katika mazingira tatanishi katika mji mkuu wa Kinshasa, nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo lakini pia siasa za kikanda, na mambo mengine duniani..
7/22/202320 minutes, 11 seconds
Episode Artwork

Wapinzani nchini DRC watoa tamko kuhusu kifo cha Okende, maandamano nchini Kenya

Makala hii imeangazia ripoti mbali mbali za waandishi wetu lakini kubwa ni kuhusu mauaji ya kuvizia dhidi ya mwanasiasa wa upinzani na mshirika wa karibu wake Moise Katumbi kule DRC pamoja na kauli ya Upinzani nchini Kenya kuhusu maandamano kuendelea juma lijalo, kule Sudan mapigano bado yaendelea, ICC yasema inafuatilia visa vya uhalifu dhidi ya binadamu, nchini Senegeal, mpinzani Ousmane Sonko ateuliwa na chame chake kuwa mgombea wa urais, na mambo mengine mbali mbali
7/15/202320 minutes, 4 seconds
Episode Artwork

Polisi wa Kenya watawanya maandamano ya upinzani, M23 na ripoti ya EU DRC

Makala hii imeangazia maandamano yaliyofanyika jijini Nairobi na maeneo mengine nchini Kenya, siku ya Kiswahili duniani, lakini pia ripoti ya umoja wa Ulaya kuhusu vita ya M23 mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, mapigano ya Sudan na matukio mengine kwengineko duniani ..Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kupata mengi zaidi.
7/8/202320 minutes, 2 seconds
Episode Artwork

Waombahifadhi kutumwa Rwanda, kinyume cha sheria: Mahakama, miaka 63 uhuru wa DRC

Makala hii imeangazia hatua ya mahakama ya London Uingereza kuhusu waomba hifadhi kwamba ni kinyume cha sheria na kwamba Rwanda si salama huku Rwanda ikisema itakata rufaa  wahamiaji walioko nchini humo. Maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa DRC na mkutano wa Luanda Angola kuhusu amani ya mashariki ya Nchi hiyo, imeangazia pia yaliyojiri nchini Kenya, Uganda, Sudan an Ethiopia na kwengineko duniani.
7/1/202320 minutes, 4 seconds
Episode Artwork

Mkutano kuhusu madeni na mabadiliko ya tabianchi watamatika Paris Ufaransa, usalama DRC

Makala hii imeangazia mkutano wa kimataifa unaolenga kutafuta mwafaka kuhusu namna ya kubadili mfumo wa ufadhili wa kifedha na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwenye mataifa yote ya dunia. Shambulio liliotekelezwa na waasi wa Uganda ADF dhidi ya shule moja laua 42, na mkataba wa kibiashara kati ya Kenya na Umoja wau laya, mchakato wa uchaguzi nchini DRC na pia yaliyojiri kwenye mataifa mengine duniani..
6/24/202320 minutes, 20 seconds
Episode Artwork

Ziara ya marais wanne wa Afrika huko Urusi na Ukraine, mauaji ya wakimbizi 46 DRC

Makala hi imeangazia ziara ya ujumbe wa viongozi wa Afrika huko Ukraine na Urusi, Nchi za Jumuia ya Afrika mashariki wiki hii zilisoma Badgeti zao za mwaka wa 2023/2024, Ripoti ya Shirika ya kimataifa la haki za binadamu kuhusu kundi la waasi wa M23 mashariki mwa DRC mauaji ya katika kambi ya wakimbizi huko Ituri, tumeangazia pia yaliyojiri kule Khartoum Sudan, kwengineko Afrika na duniani
6/17/202320 minutes, 6 seconds
Episode Artwork

Wizara ya mambo ya ndani yasitisha shughuli za CNL Burundi, msako makazi ya Katumbi DRC

Hatua ya rais wa Rwanda Paul Kagame kufanya mabadiliko katika vyombo vya usalama na jeshi nchini mwake, viongozi wa COMESA wakutana jijini Lusaka nchini Zambia, msako mkali ulifanyika katika makazi ya Moise Katumbi na mshauri wake nchini DRC, tumeangazia yaliyojiri nchini Kenya, Uganda, na hali ya mapigano kule Sudan Khartoum, na pia Afrika magharibi na kwengineko duniani! Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kusikiliza mengi zaidi
6/10/202320 minutes, 14 seconds
Episode Artwork

Kikosi cha EAC chaongezewa muda wa kuhudumu DRC, mapigano yaendelea Sudan

Makala hii imeangazia hatua ya viongozi wa Jumuia ya Afrika mashariki kukiongezea muda wa miezi sita kikosi cha Jumuia hiyo kuhudumu kwa ajili ya kupatikana kwa amani ya mashriki mwa DRC, nchi za magharibi na Marekani zasikitikia hatua ya Uganda kupinga Ushoga, ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Urusi Lavrov jijini Bujumbura Burundi, hali ya mapigano kule Sudan Khartoum, lakini pia yaliyojiri katika eneo la Afrika magharibi na mkutano wa Moldova na mapigano ya Ukraine. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi
6/3/202320 minutes, 12 seconds
Episode Artwork

Ziara ya rais wa DRC Félix Tshisekedi China, mradi wa umeme wa Uganda na Tanzania

Katika makala ya yaliyojiri wiki hii, tunaangazia habari kuu za dunia, matukio ya wiki hii ikiwa ni pamoja na  ziara ya rais wa DRC Felix Tshisekedi huko China, Uganda na Tanzania zilizindua bwawa la pamoja la kuzalisha umeme wa megawati 16, katika mto Kagera eneo la Kikagati, miaka 60 tangu kuundwa kwa Umoja wa Afrika AU, hali ya mapigano kule Sudan Khartoum, lakini pia eneo la Afrika magharibi na mapigano ya Ukraine ni miongoni mwa mengi yaliyomo
5/27/202320 minutes, 8 seconds
Episode Artwork

Wafanyabiashara wa Kariakoo Tanzania wakutana na waziri mkuu, hali Sudan yatisha

Katika makala ya Yaliyojiri wiki Hii, tunaangazia baadhi ya habari kuu za dunia matukio ya wiki hii katika miongoni ikiwa ni pamoja na  mgomo wa wafanyabiashara katika soko la kimataifa la Kariakoo jijini Daresalaam nchini Tanzania, DRC na Rwanda zilikubaliana kutengeneza mazingira kwa wakimbizi wa pande zote kurejea makwao, Hali ya kisiasa na nchini Sudan, lakini pia yaliyojiri katika eneo la Afrika magharibi na Mkutano wa G7 huko Japani ni miongoni mwa mengi utayasikia
5/20/202320 minutes, 14 seconds
Episode Artwork

SADC kupeleka wanajeshi DRC, miili 150 yafukuliwa nchini Kenya na mengineyo

Makala hii imeangazia kuhusu maafa yaliyosababishwa na mafuriko wilayani Kalehe DRC, pia hatua ya jumuia ya SADC kusaidia juhudi za upatikanaji wa amani ya mashariki mwa DRC, miili zaidi yafukuliwa nchini Kenya, hali ya nchini Sudan,pamoja na mambo mengine yaliyojiri katika eneo la Afrika magharibi na kwengineko duniani.
5/13/202320 minutes, 16 seconds
Episode Artwork

Mafuriko yasababisha maafa mengi nchini Rwanda na maeneo mengine ya Afrika

Makala hii imeangazia matukio mengi ya wiki hii lakini kubwa ni kuhusu maafa yaliyoripotiwa huko Rwanda na nchini DRC katika mafuriko yaliyosababisha maporomoko ya ardhi baada ya mvua kubwa kunyesha maeneo kadhaa, maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari tukiangazia kwa namna ya pekee mazingira ya wanahabari wa mashariki ya DRC hali nchini Sudan, yaliyojiri katika eneo la Afrika magharibi, kutawazwa kwa mfalme Charles wa 3 na mambo mengine kwengineko duniani.
5/6/202320 minutes, 15 seconds
Episode Artwork

Hali ya usalama nchini Sudan yaboreka, mkuu wa jeshi la EAC DRC forces arejea Nairobi

Makala imeangazia hali inavyoendelea nchini Sudan baada ya usitishwaji wa mapigano uliokubaliwa na pande zinazokinzana, ziara ya rais wa Rwanda Paul Kagame nchini Tanzania,hali ya usalama wa mashariki kule DRC, na tukio la moto kwenye gereza  la Bukavu, mkoani Kivu kaskazini, nchini Kenya Kulifukuliwa miili kadhaa ya wakristo waliokufa wakifunga baada ya mchungaji wao kuwaaminisha kufunga hadi kufa ili waonane na YESU,Tumeangazia yaliyojiri pia katika eneo la afrika magharibi na kwengineko duniani,
4/29/202320 minutes, 14 seconds
Episode Artwork

Hali ya usalama yazidi kuzorota Sudan, sheria dhidi ya ushoga bungeni Uganda

Makala hii imeangazia mapigano na hali inavyoendelea nchini Sudan, na miito ya kusitishwa mapigano, muswada wa sheria unaopinga ushoga ulirejeshwa bungeni wiki hii, na kuanza kwa mazungumzo kati ya wajumbe wa muungano wa Upinzani wa Azimio nchini Kenya na wajumbe wa rais wa Kenya William Ruto nchini, tumeangazia yaliyojiri katika eneo la Afrika magharibi na kwengineko duniani
4/22/202320 minutes, 13 seconds
Episode Artwork

Watu 60 wauawa DRC, chanjo ya Malaria yaidhinishwa Ghana, nyaraka za siri za Marekani zavuja

Kwenye makala haya, tutakayoangazia wiki hii ni pamoja na upinzani nchini Kenya kusema utaendelea na maandamano huku wafanyakazi wa umma wakikosa kulipwa, tutaangazia usalama nchini DRC na uchaguzi unaotarajiwa mwishoni mwa mwaka huu. Chad na Ujerumani kuwafukuza mabalozi wake, kadhalika kuvuja kwa nyaraka za siri nchini Marekani na Korea kaskazini kutishia usalama wa kikanda. Zaidi ya raia 60 wameuawa katika mashambulizi mapya ya vijiji vitano mkoani Ituri, waasi wa CODECO na makundi ya kikabila ya Zaire wakituhumiwa kuhusika na mauaji hayo. Kwa mengi zaidi, sikiliza makala haya.
4/15/202320 minutes, 1 second
Episode Artwork

Siasa za Kenya, DRC na Uganda zaungana dhidi ya ADF, miaka 29 baada ya mauaji ya Rwanda

Makala hii imeangazia mpango wa kufanyika mazungumzo kati ya upinzani na serikali nchini Kenya kusuasua, ziara ya rais wa Kenya William Ruto nchini Rwanda, wakuu wa majeshi ya DRC na Uganda wapongeza operesheni Shujaa huko Beni, raia wa Senegal, waliadhimisha miaka 63 tangu wapate uhuru wao kutoka kwa Ufaransa, kwengineko aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump, alifikishwa mahakamani jijini New York, ziara ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron nchini China kuishawishi Urusi kuachana na vita vya Ukraine, na mambo mengine.
4/8/202320 minutes, 3 seconds
Episode Artwork

Maandamano ya upinzani nchini Kenya yashika kasi, Uganda yatuma wanajeshi wake DRC

Kubwa katika makala hii ni kuhusu maandamano ya upinzani nchini Kenya, ziara ya makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris nchini Tanzania, wiki hii wanajeshi wa Uganda waliwasili kwenye mji wa Bunagana mashariki mwa DRC, lakini pia muswada wa sharia unaohusu uraia kwa mtu anayetakiwa kuwa kwenye wadhifa wa rais  kuzua hisia mseto. Hukumu dhidi ya kiongozi wa upinzani nchini Senegal; Ziara ya mfalme Charles wa 3 wa Uingereza huko Ujerumani, na mambo mengine...
4/1/202320 minutes, 7 seconds
Episode Artwork

Rais Tshisekedi awateua Bemba na Kamerhe kuwa Mawaziri

Miongoni mwa yale utakayosikia, ni hatua ya rais wa DRC Felix Tshisekedi kumteua Jean Pierre Bemba kuwa Waziri mpya wa Ulinzi na Vital Kamerhe kuwa Waziri wa Uchumi, maandamano ya upinzani nchini Kenya na makabiliano ya waandamanaji na polisi nchini Ufaransa kupinga mageuzi ya mfumo wa pensheni.
3/25/202320 minutes, 12 seconds