Winamp Logo
Jukwaa la Michezo Cover
Jukwaa la Michezo Profile

Jukwaa la Michezo

Swahili, Sports, 1 season, 41 episodes, 16 hours, 15 minutes
About
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Episode Artwork

AFCON 2024: DRC na Nigeria zatinga hatua ya nusu fainali

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na taifa la DR Congo pamoja na Nigeria kufuzu kwa hatua ya nusu fainali katika michuano ya  kuwania taji la soka kwa mataifa ya bara Afrika. Dereva wa magari ya langalanga Lewis Hamilton kuhamia katika timu ya Ferrari kutoka Mercedes mwaka 2025.
2/3/202423 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

AFCON 2024: Michuano ya hatua ya 16 bora kuanza

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na michuano ya hatua ya 16 kuwania taji la soka kwa mataifa ya bara Afrika. Mashindano ya mchezo wa mikono bara Afrika yanayoendelea kule Misri na Aryna Sabalenka  kushinda mashindano ya Australian Open kwa upande wa wanawake.
1/27/202423 minutes, 49 seconds
Episode Artwork

Mataifa ya Afrika yaendelea kupambana kutafuta taji la AFCON

Tunaendelea kukuletea uchambuzi wa michuano ya soka kuwania ubingwa kwa mataifa ya Afrika, inayoendelea nchini Cote Dvoire. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Tanzania, pia zinapambana kuwania taji hilo. Ungana na wachambuzi wetu Jason Sagini, George Ajowi na Jason Sagini akiwa mjini San Pedro.
1/20/202423 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Michuano ya AFCON yaanza nchini Cote Dvoire, nani ataibuka mshindi ?

Michuano ya soka kuwania taji la mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON, inaanza leo nchini Cote Dvoire. Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano haya makubwa kurejea kwenye nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 40. Kuna timu 24 zinazotafuta ubingwa wa taji hili, ikiwemo Taifa Stars ya Tanzania na Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka Afrika Mashariki na Kati. Wachambuzi wetu Paul Nzioki, George Ajowi na Jason Sagini, akiwa  Abidjan, wnachambua.
1/13/202423 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

CAF yaongeza kiwango cha fedha kwa mshindi wa AFCON 2024

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa  Shirikisho la soka barani Afrika CAF kuongeza kiwango cha fedha kwa mshindi wa michuano ya AFCON, itakayoanza Januari 13 nchini Cote Dvoire,  Bondia wa DRC Martin Bakole aomba mchango wa fedha kushiriki mechi za mkanda wa WBA, matokeo ya Mapinduzi Cup na kombe la Amani visiwani Zanzibar na Brazil yamfuta kazi kocha Fernando Diniz.
1/6/202423 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Timu za Afrika zaanza kutangaza vikosi kuelekea AFCON 2024

Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa vikosi vya mwisho vilivyotangazwa na mataifa kadhaa kuelekea AFCON ya mwaka 2023 itakayoanza Januari 13, 2024, raia wa Rwanda Clare Akamanzi ateuliwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa NBA Africa, Guy Bukasa atangazwa kocha mpya wa AS Kigali, rais wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach atangaza mikakati ya kujumuisha michezo ya kielektroniki e-sports kwenye Olimpiki na kocha Carlo Ancelotti atia saini mkataba mpya klabuni Real Madrid.
12/30/202323 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Kenya yaibuka bingwa wa mashindano ya Tong Il Moo Do

Tuliyokuandalia ni pamoja na Kenya kuhifadhi taji lake la Tong Il Moo Do kwa mara ya 11, mkenya Angella Okutoyi ashinda dhahabu mbili kwenye tenisi ya kimataifa ya W25, uchambuzi wa matokeo ya mechi za Klabu bingwa Afrika wiki hii, Man City kutwaa ubingwa wa Kombe la Klabu bingwa Duniani kwa mara ya kwanza na Mahakama ya Ulaya kupinga uamuzi wa FIFA na UEFA kuzuia kuanzishwa kwa Ligi mpya ya Ulaya kuwa kinyume na sheria. 
12/23/202323 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Mashindano ya Kimataifa ya Tong-Il-Moo-Do yafanyika nchini Kenya

Kenya yaandaa makala ya 11 ya michuano ya kimataifa ya mchezo wa Tong-Il-Moo-Do jijini Mombasa. Uganda ndio washindi wa CECAFA katika mechi za kufuzu kwa michuano ya CAF ya Shule za Afrika. Al Ahly waishinda Al-Ittihad kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu Kisha Paris Saint - Germain yatinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa.
12/16/202321 minutes, 1 second
Episode Artwork

Messi ashinda tuzo ya Ballon d'Or tena

Miongoni mwa yale tunayojadili ni pamoja na tuzo za wachezaji bora barani Afrika mwaka huu katika mchezo wa soka, timu ya taifa ya Uganda Cranes kupata kocha mpya, mechi za soka kufuzu michezo ya Olimpiki Paris 2024 miongoni mwa wanawake, Lionel Messi kushinda tuzo ya nane la Ballon d'Or, miongoni mwa mengine.
11/4/202323 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Uchaguzi wa viongozi wa mchezo wa Tennis barani Afrika

Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na Afrika kupata viongozi wapya wa Shirikisho la mchezo wa Tenisi, uchambuzi wa fainali ya kombe la dunia la raga, pigano la ndondi kati ya Tyson Fury na Francis Ngannou, mechi za kufuzu olimpiki ya mwaka kesho kwa kina dada, Ligi Kuu ya soka Afrika, debi la Manchester na El Clasico na mchezaji wa Newcastle Sandro Tonali kupigwa marufuku ya miezi kumi kwa kujihusisha na masuala ya michezo ya bahati nasibu.
10/28/202323 minutes, 39 seconds
Episode Artwork

Raga: Afrika Kusini na New Zealand kuchuana fainali ya kombe la dunia

Tumekuandalia uchambuzi kuhusu fainali inayotarajiwa kati ya Afrika Kusini na New Zealand, kuwania taji la kombe la dunia katika mchezo wa raga lakini pia kuendelea kwa michuano mipya ya soka ya ligi ya Afrika.
10/22/202323 minutes, 52 seconds
Episode Artwork

CAF yatangaza droo ya hatua ya makundi, michuano ya klabu bingwa na Shirikisho

Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa droo ya hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Afrika, Gor Mahia yaibuka na ushindi kwenye debi la mashemeji, uchambuzi wa matokeo ya mechi za klabu bingwa ulaya, Kombe la Dunia la mwaka 2030 kuandaliwa kati ya mataifa sita na Pogba kupatikana ametumia dawa za kusisimua misuli katika kipimo cha pili.
10/7/202323 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Afrika Mashariki kuwa wenyeji wa AFCON 2024

Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na Afrika Mashariki kuteuliwa kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2027, hatua ya mwisho ya kufuzu Kombe la Mataifa ya wanawake mwaka 2024, raundi ya mwisho kufuzu hatua ya makundi michuano ya klabu bingwa barani Afrika na Kombe la dunia la raga, linaloendelea nchini Ufaransa.
9/30/202323 minutes, 32 seconds
Episode Artwork

Mkenya Eliud Kipchoge ashinda tena taji la Berlin Marathon

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na mwanariadha kutoka Kenya, Eliud Kipchoge kushinda mashindano ya riadha ya Berlin Marathon kwa mara ya tano, Kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya Rwanda, asimamishwa kazi ni  miongoni mwa mengine mengi yanayotokea viwanjani.
9/24/202323 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Klabu za Afrika zachuana kunyakuwa taji la klabu bingwa

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na mahojiano kuhusu kongamano la kibiashara la soka barani Afrika, lililofanyika wiki hii jijini Nairobi. Misri waibuka washindi wa kombe la mataifa ya Afrika voliboli ya wanaume, APR ya Rwanda yashinda ubingwa wa ligi kuu ya basketboli, uchambuzi wa mechi za kufuzu klabu bingwa barani Afrika na kombe la dunia la raga. 
9/16/202323 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Kombe la dunia la mchezo wa raga, laanza nchini Ufaransa

Tuliyokuandalia ni pamoja na kuanza kwa  Kombe la Dunia katika  mchezo wa raga nchini Ufaransa, Tanzania kufuzu Kombe la mataifa ya Afrika mchezo wa soka mwaka 2023 na Rwanda yaondolewa  kwenye mashindano ya voliboli barani Afrika.
9/9/202323 minutes, 49 seconds
Episode Artwork

Matukio makubwa yaliyotokea duniani wiki hii

Tuliyokuandalia ni pamoja kifo cha mshindi wa kwanza tuzo la Ballon D'Or  la Afrika Selif Keita, ushirikiano wa Azam  na FKF kupeperusha ligi kuu ya Kenya, rais wa FERWAFA kujiuzulu, Uganda yashinda medali yao ya kwanza kwenye mashindano ya Pentathlon, mlinda lango Andre Onana arejea kwenye kikosi cha Cameroon na uchambuzi wa Droo ya michuano ya klabu bingwa Ulaya na siku ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji ulaya.
9/2/202323 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Faith Kipyegon aweka historia mashindano ya riadha ya dunia 2023

Faith Kipyegon ameishindia Kenya medali mbili za dhahabu katika mbio za mitaa 1500 na 5000 katika mashindano ya riadha ya dunia, katika jiji la Budapest nchini Hungary. Tunajadli hili na mengine mengi yanayotokea viwanjani wiki hii.
8/27/202323 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Mashindano ya riadha ya dunia yaanza nchini Hungary

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na kuanza kwa mashindano ya riadha ya dunia, jijini Budapest. Kocha wa mchezo wa soka nchini Uganda, Sam Timbe ameaga dunia. Mechi za kufuzu hatua ya makundi michuano ya CAF, LALIGA kuweka mipango ya vilabu vyake kuzuru Afrika Mashariki pamoja na Luciano Spalletti kutajwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Italia.
8/19/202323 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Msimu mpya wa ligi kuu ya soka barani Ulaya waanza

Tuliyokuandalia leo ni pamoja na kuanza kwa ligi kuu ya soka nchini Uingereza na mataifa kadhaa ya Ulaya,  uchambuzi wa Kombe la dunia la wanawake katika mchezo wa soka, fainali za ngao ya jamii  katika mchezo wa soka Afrika Mashariki na mashindano ya shule za Sekondari nchini Kenya na michuano ya kufuzu kushiriki taji la klabu bingwa barani Afrika kwa upande wa wanawake, miongoni mwa mengine.
8/12/202324 minutes
Episode Artwork

Kombe la dunia la Wanawake: Timu za Afrika zafika hatua ya 16 bora

Tuliyokuandalia Jumamosi hii, ni pamoja na uchambuzi wa timu za Afrika kwenye raundi ya mtoano Kombe la Dunia la wanawake katika mchezo wa soka. Kombe la dunia la netiboli kwa kina dada na mechi ya ngao ya jamii ya Uingereza kati ya Manchester  City na Arsenal. Pia matokeo ya mashindano ya La Francophonie inayokamilika Jumapili nchini DRC, miongoni mwa mengine. 
8/5/202323 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Michezo ya Francophonie yaanza jijini Kinshasa

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na kuanza kwa  mashindano ya La Francophonie nchini DRC, maandalizi kuelekea Olimpiki ya mwaka 2024? Uchambuzi wa mechi za Kombe la Dunia soka la kina dada droo ya klabu bingwa barani Afrika na michuano ya Kombe la Dunia mchezo wa netiboli.
7/29/202323 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Vingegaard bingwa wa mashindano ya Tour de France mwaka 2023

Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na Jonas Vingegaard ndio bingwa wa mashindano ya kukimbiza baiskeli ya Tour de France ya mwaka 2023 , uchambuzi wa mechi za Kombe la Dunia la wanawake, mashindano ya  riadha Monaco Diamond League, tetesi za uhamisho barani Afrika na Ulaya pamoja na maandalizi ya mashindano ya La Francophonie nchini DRC.
7/22/202323 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Tennis: Vondrousova amshinda Ons Jabeur kunyakua taji la Wimbeledon 2023

Miongoni mwa matukio hayo ni pamoja na uhamisho wa wachezaji wa klabu za soka kutoka nchi za Afrika Mashariki kuelekea kuanza kwa msimu mpya.Droo ya hatua ya makundi kwa mataifa ya Afrika kufuzu kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2026 katika mchezo wa soka nchini Marekani, Mexico na Canada.Katika mchezo wa Tennis, kuwania taji la Wimbeledon, Marketa Vondrousova ndio bingwa kwa upande wa wanawake….miongoni mwa mengine mengi
7/15/202323 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Morocco mabingwa wa taji la vijana wasiozidi miaka 23 Afrika

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na Morocco kushinda ubingwa wa kombe la Mataifa ya Afrika U23, timu ya soka ya wanawake ya Afrika Kusini Banyana Banyana yafanya  uamuzi wa kuelekea Newzealand kwa ajili ya michuano ya Kombe la dunia baada ya kusuluhisha mzozo wa malipo. 
7/9/202323 minutes, 37 seconds
Episode Artwork

Michuano ya soka kutafuta ubingwa vijana chini ya miaka 23 yashika kasi Morocco

Miongoni mwa yale  tuliyokuandalia ni pamoja na  klabu ya Kakamega Homeboyz kutoka Kenya, kufuzu kwenye michuano ya Shirikisho barani Afrika msimu ujao, mashindano ya Fatshi Cup kuanza leo nchini DRC, uchambuzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika U23, matokeo ya michezo ya Ufukweni barani Afrika na riadha za Diamond League naye Mbappe aongoza wachezaji wa timu za ufaransa kukomesha vurugu kufuatia maandamano.
7/1/202323 minutes, 57 seconds
Episode Artwork

Mashindano ya Safari Rally yaendelea kutifua vumbi nchini Kenya

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na mashindano ya Kimataifa ya kukimbiza magari nchini Kenya, Safari Rally, klabu ya soka ya Yanga nchini Tanzania, yampata kocha mpya na matukio yanayojiri viwanjani kote duniani.
6/24/202324 minutes, 40 seconds
Episode Artwork

Tennis: Morocco mabingwa wa taji la Billie Jean King

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia Jumamosi hii, ni pamja na Morocco yashinda  taji la tenisi Billie Jean King  barani Afrika , uchambuzi wa mechi za kufuzu Kombe la EURO na Kombe la mataifa ya Afrika mwaka ujao, kocha Nabi kuondoka Yanga na matokeo ya riadha Oslo Diamond League.
6/17/202323 minutes, 32 seconds
Episode Artwork

Faith Kipyegon avunja rekodi ya dunia kwenye mbio za Mita 5,000

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na Mkenya Faith Kipyegon kuvunja rekodi ya dunia katika  mbio za Mita 5,000 katika mashindano ya riadha ya Diamond League jijini Paris, Iga Swiatek ashinda tena taji la French Open kwenye mashindano ya Tennis na fainali ya klabu bingwa barani Ulaya, kati ya Manchester City na Inter Milan.
6/12/202323 minutes, 52 seconds
Episode Artwork

Manchester City mabingwa wa taji la FA nchini Uingereza

Kocha wa klabu ya Manchester City nchini Uingereza, Pep Guardiola ameiongoza klabu yake kuishinda Manchester United mabao 2-1 katika fainali ya FA. Fainali ya pili ya shirikisho barani Afrika kati ya USM Algier na Yanga kutoka Tanzania, matukio ya riadha na Tennis ni miongoni mwa yale tuliyokuadalia kwenye Makala ya leo.
6/3/202323 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Bayern Munich mabingwa wa ligi mara ya 11

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na maandalizi ya fainali ya kwanza kuwania taji la Shirikisho barani Afrika kati ya Yanga SC ya Tanzania na USM Alger, ya Algeria. Vituo vya kukuza soka nchini Rwanda, vinavyofadhiliwa na klabu ya Ufaransa ya Paris Saint-Germain na Bayern Munich yashinda taji lake ya 11 katika ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani.
5/27/202323 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Dondoo ya taarifa za michezo, ikiwemo Senegal U-17 kuwa mabingwa wa Afrika.

Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na ligi ya mpira wa vikapu barani Afrika kuanza leo nchini Rwanda, Yanga yatinga fainali ya kombe la shirikisho wakati Senegal watawazwa washindi wa kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 17, CAF yatangaza mfumo mpya wa kufuzu kombe la dunia mwaka 2026 na orodha ya mwisho ya wachezaji watakaowania tuzo la Marc-Vivien Foe yatangazwa na RFI/France 24.
5/20/202324 minutes
Episode Artwork

Omanyala awika mashindano ya riadha ya Kip Keino Classic jijini Nairobi

Mkenya Ferdinand Omanyala ameshinda mbio za Mita 100 katika mashindano ya riadha ya Kip Keino Classic yaliyofanyika jijini Nairobi, huku Mmarekani Sha'Carri Richardson naye akiibuka bingwa katika Mita 200 kwa upande wa wanawake.Tunachambua pia ligi ya soka nchini Rwanda,  kufukuzia ubingwa na mchuano wa watani wa jadi nchini Kenya, kati ya Gor Mahia na AFC Leopards.
5/13/202323 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Wanariadha wajipima nguvu katika mashindano ya Diamond League

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na matokeo na uchambuzi mashindano ya riadha ya Diamond League, kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 17 na maendeleo ya ligi kuu za soka katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.
5/6/202323 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Simba SC yaondolewa kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na  kuanza kwa kombe la mataifa ya Afrika CHAN kwa vijana wasiozidi miaka 17, Simba kuondolewa kwenye mashindano ya CAF, Kenya yashinda Kombe la dunia katika mchezo wa wavu na uchambuzi wa mataifa ya  Kenya, Uganda na Tanzania kuomba kuwa wenyeji wa michuano ya AFCON 2027.
4/29/202323 minutes, 51 seconds
Episode Artwork

Mechi za robo fainali klabu bingwa Afrika zashika kasi

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja  na shirikisho la soka nchini Kenya FKF limeitaka bunge la Kenya kutunga  sheria dhidi ya wapangaji mechi, uchambuzi wa mechi za robo fainali mashindano ya vilabu bingwa barani Afrika, matokeo ya riadha wiki hii na tuzo ya RFI na France 24 kuhusu mchezaji wa zamani wa Cameroon Marc Vivien Foe.
4/22/202323 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Ligi kuu Tanzania bara: Nani ataibuka mshindi kati ya Simba na Yanga ?

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa mechi ya watani wa jadi kati ya Yanga dhidi ya Simba kuwania taji la soka Tanzania bara, sakata la wachezaji Sadio Mane na Achraf Hakimi, CAF yampiga marufuku refarii wa Botswana na kocha wa Ethiopia ameacha kuifunza Ethiopia.
4/15/202323 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Droo ya robo fainali kuwania taji la klabu bingwa Afrika

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa hatua ya droo ya robo fainali ya mashindano ya klabu bingwa Afrika. Shirikisho la mchezo wa Raga nchini Kenya limepata viongozi wapya na Mo Farah ashindwa kwenye mbio fupi nchini Gabon. 
4/8/202323 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Ripoti kuhusu hali ya wanamichezo wanaotumia dawa zilizozuiwa, yatolewa Kenya

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na Kenya kutoa ripoti ya kupambana na visa vya dawa zilizopigwa marufuku  za kusisimua misuli kwa wanamichezo na hali ya michuano ya soka, kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika na ile ya kufuzu kwa AFCON 2024.
4/1/202323 minutes, 24 seconds
Episode Artwork

Mataifa ya Afrika yaendelea kusaka nafasi ya kushiriki AFCON 2024

Jumamosi hii, miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na mwanamasombwi kutoka Tanzania, Karim Mandonga kupambana na mpinzani wake kutoka nchini Uganda jijini Nairobi, matokeo, matukio na uchambuzi wa mashindano ya kufuzu Kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu na Kombe la EURO mwaka ujao huko barani Ulaya.
3/25/202323 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Gianni Infantino achaguliwa tena kuwa rais wa FIFA

Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na kongamano la Shirikisho la soka duniani  FIFA lililofanyika jijini Kigali nchini Rwanda, timu za taifa za Afrika Mashariki zajiandaa kwenye mechi za kimataifa na uchambuzi wa mashindano ya ligi ya mabingwa Afrika na droo ya UEFA.
3/18/202323 minutes, 38 seconds