Winamp Logo
Habari RFI-Ki Cover
Habari RFI-Ki Profile

Habari RFI-Ki

Swahili, Political, 1 season, 90 episodes, 14 hours, 53 minutes
About
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Episode Artwork

Maoni yako katika mada huru

2/24/20249 minutes, 47 seconds
Episode Artwork

Maoni yako kuhusu kuwepo kwa umri wa lazima wa watu kustaafu

2/23/20249 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya lugha mama

2/21/20249 minutes, 35 seconds
Episode Artwork

Siku ya kimataifa ya haki za kijamii kushinikiza haki na usawa katika jamii.

2/20/20249 minutes, 31 seconds
Episode Artwork

Mkutano wa viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia

2/19/20249 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Mada ya msikilizaji wiki hii

2/19/202410 minutes, 9 seconds
Episode Artwork

Maandamano jijini Kinshasa yaliyolenga ubalozia wa nchi za magharibi

2/16/202410 minutes, 1 second
Episode Artwork

Madagascar yapitisha sheria ya kuhasiwa watuhumiwa wa ubakaji

2/16/202410 minutes, 3 seconds
Episode Artwork

Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Radio

2/13/202410 minutes, 2 seconds
Episode Artwork

Michuano ya AFCON 2024

Ivory Coast walitawazwa washindi wa michuano ya kombe la Afrika AFCON baada ya kuishinda timu ya Super Eagles ya Nigeria kwa mabao 2 -1
2/12/202410 minutes, 16 seconds
Episode Artwork

Maoni ya waskilizaji kuhusu matangazo yetu juma hili

Kila siku ya Ijumaa una uhuru wa kuchangia mada mbalimbali kwenye makala ya Habari Rafiki, ndani ya rfi kiswahili. Haya hapa maoni ya baadhi yenu.
2/9/20249 minutes, 47 seconds
Episode Artwork

Ugumu wa kupata vitambulisho Kenya na DRC

 Makala ya Habari Rafiki leo tunajadili hatua ya raia nchini Kenya kuzidi kulalamikia ugumu wa kupata vitambulisho, huku nchini DRC raia pia wakilalamikia ugumu wa kupata passpoti. Je unafikiri ugumu huu unatokana na nini?Haya hapa baadhi ya maoni yako.
2/8/20249 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

AFCON : Ubashiri wa mashabiki kuhusu mechi za leo

Tunajadili ubashiri wako kwa mechi za leo za  kuwania ubingwa wa kombe la Afrika, Afcon ambazo zitagarazazwa leo, ikiwa NI nusu fainali DRC ikipiga dhidi ya Ivory Coast nayo Nigeria ikichuana na Afrika Kusini.  Nani atatambaa kwenye mechi za leo?Haya hapa baadhi ya maoni yenu?     
2/7/20249 minutes, 39 seconds
Episode Artwork

Kenya : Vipi tunaweza zuia mikasa ya moto ?

Watu sita wamefariki nchini Kenya, kutokana na mkasa wa moto ambao ulitokana na mlipuko kwenye kituo cha gesi kilichokuwa karibu na  makaazi ya watu mtaani Embakasi viungani mwa jiji la Nairobi.  Tunakuliza wewe, nini kifanyike ili kuepusha mikasa kama hii kwenye maakazi ya watu , maana si mara ya kwanza tukio kama hili kutokea katika mataifa ya Africa.Haya hapa baadhi ya maoni yako.
2/6/20249 minutes, 51 seconds
Episode Artwork

Transparency international yasema Afrika yashindwa kupambana na rushwa

Ripoti ya hivi punde ya shirika la Transparency International, ambayo inaonesha kuwa mataifa ya Afrika hayapigi hatua kwenye mapambano dhidi ya rushwa.Tumekuuliza msikilizaji unadhani nini kinasababisha hali hii ? Unafikiri serikali ya nchi yako inafanya vya kutosha kupambana na rushwa?Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kupata maoni ya wasikilizaji wa RFI Kiswahili
2/1/202410 minutes, 1 second
Episode Artwork

Wabunge wapya waanza vikao vyao nchini DR Congo

Nchini DRC, bunge la awamu ya nne 2024 hadi 2028, lilianza vikao vyake siku ya Jumatatu jijini Kinshasa kwa kuwatambulisha wabunge wapya waliochaguliwa.Wananchi wa DRC watarajie nini kutoka kwa bunge hili ? Unadhani sera ya kususia vikao kwa wabunge wa upinzani ni chaguo bora ?
1/31/20249 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Hali ngumu ya maisha katika nchi za Afrika

1/24/202410 minutes, 6 seconds
Episode Artwork

Hatua ya Sudan Kusitisha uanachama wake na muungano wa IGAD

Sudan kabla kuwasilisha msimamo huo rasmi ,ilisusia kikao cha IGAD jijini Kampala ikisema pia imesitisha uhusiano wowote na IGAD Ni hatua ambayo inakisiwa kuchochewa na IGAD kumwalika kiongozi wa RSF Mohamed Dagla katika kikao chake cha Kampala
1/23/20249 minutes, 51 seconds
Episode Artwork

Maoni yako mskilizaji kuhusu mada tofauti

1/19/20249 minutes, 52 seconds
Episode Artwork

Oxam laonya juu ya kuongezeka kwa pengo kati ya watu matajiri na masikini duniani

1/18/20249 minutes, 31 seconds
Episode Artwork

Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na chanjo ya ugonjwa huo kuanza kutolewa Zambia

1/17/20249 minutes, 49 seconds
Episode Artwork

Nchi za Ukanda kuendelea kukumbwa na ajali za migodi, tukio la punde likitokea nchini Tanzania

1/16/20249 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Maoni yako kuhusu muanza kwa michuano ya AFCON23 nchini Ivory Coast, na timu unayoshabikia

1/15/20249 minutes, 48 seconds
Episode Artwork

Maoni ya waskilizaji kuhusu tuhuma za Burundi kwa Rwanda kuwaunga mkono waasi

Maoni ya waskilizaji kuhusu tuhuma za rais wa Burundi dhidi ya Rwanda kwamba inawaunga mkono waasi wa M23 ambao walitekeleza mauaji hivi karibuni nchini Burundi katika eneo la mpaka wa Burund na DRC na kuwauwa watu 20.
1/10/20249 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Mada ya msikilizaji

1/5/202410 minutes, 1 second
Episode Artwork

Athari za Matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii

Mataifa mengi kama Tanzania, Burundi na DRC yamekabiliwa na athari za matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kuanzia kwa taarifa za uongo hadi jumbe za chuki hasa nyakati za uchaguzi.Na leo kwenye makala yetu tulitaka kujua iwapo unadhani mitandao ya kijamii inatumika kueneza propaganda? na nini kifanyike ili kuzuia matukio kama haya?Sikiliza 
12/19/202310 minutes, 2 seconds
Episode Artwork

Jumuiya ya kimataifa kuongeza shinikizo kwa Israel na Hamas kusitisha mapigano

Kwenye makala yetu ya leo tunajadili kuhusu kuhusu jumuiya ya kimataifa kuongeza shinikizo kwa Israel na Hamas kusitisha mapigano.Unafikiri kwa nini mataifa yanashindwa kuzishinikiza pande hizo kusitisha mapigano? Nini zaidi kifanyike kupata suluhu ya mzozo kati ya pande hizo mbili ? sikiliza 
12/18/20239 minutes, 48 seconds
Episode Artwork

Maoni yako kuhusu taarifa zetu juma hili

Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi kuchangia mada yoyote inayokuhusu au ile umeskia katika taarifa zetu.
12/15/20239 minutes, 46 seconds
Episode Artwork

Maoni yako kuhusu taarifa zetu juma hili

Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi kuchangia mada yoyote inayokuhusu au ile umeskia katika taarifa zetu.
12/15/20239 minutes, 46 seconds
Episode Artwork

COP28: Dunia yaidhinisha wito wa kuachana na nishati ya mafuta na gesi

Dunia kwa mara ya kwanza imeidhinisha wito wa kuachana na nishati ya mafuta na gesi katika juhudi zakukabiliana na madiliko ya hali ya hewa.Na hii ni baada ya mkutano wa COP28 kule Dubai.Kwenye makala utakayosikiliza tulimuuliza msikilizaji wetu anafikiri mambo gani yatabadilika baada ya siku 13 za mazungumzo? na pengine alitarajia nini kutoka kwa mkutano huo
12/14/20239 minutes, 42 seconds
Episode Artwork

Marekani yatangaza usitishwaji vita wa saa 72 kati ya waasi wa M23 na jeshi la FARDC nchini DRC

Marekani imetangaza usitishwaji vita wa saa 72, uliokubaliwa na pande zinazopigana mashariki mwa DRC.Ukumbuke kuwa Novemba mwaka jana makubaliano mengine ya kusitisha mapigano yalipitishwa kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa FARDC.Wasikilizaji wetu wanawaza nini kuhusu usitishaji wa vita hivi punde,je  utadumu? Hebu sikiliza 
12/13/20239 minutes, 49 seconds
Episode Artwork

Mkutano wa wanachama wa Ecowas wafanyika jijini Abuja nchini Nigeria

Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi, wametoa masharti kwa nchi ya Niger kumuachia huru Rais Bazoum na kuindolea vikwazo nchi hiyo baada ya kukutana jijini Abiuja nchini Nigeria.Na kwenye makala yetu ya leo tulikuuliza iwapo Unadhani ECOWAS iko sahihi kuendelea kuweka vikwazo dhidi ya Niger, Mali na Burkina Faso?Sikiliza maoni ya baadhi ya wasiikilizaji wetu 
12/12/202310 minutes, 1 second
Episode Artwork

Umoja wa mataifa washindwa kuafikiana kuhusu mapigano kwenye eneo la Gaza

Msikilizaji kwenye makala yetu hii leo tunazungumza kuhusu, baraza la usalama katika Umoja wa Mataifa kushindwa kuafikiana kuhusu usitishwaji wa mapigano kwenye eneo la Gaza baada ya kura ya turufu ya Marekani.Hebu sikiliza maoni ya raia kutoka mataifa mbalimbali.
12/11/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Jumuiya ya Afrika mashariki kukutana jijini Arsuha juma lijalo

Wakati huu wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakitazamiwa kukutana juma lijalo, Jumuiya hiyo imeonekana kuendelea kushindwa kutatua mizozo inayoikumba nchi wanachama.Na kwenye makala yetu tumejadili mengi ikiwemo nini cha ziada kifanyike kuboresha utendakazi jumuiya hiyo.Sikiliza.
11/16/20239 minutes, 40 seconds
Episode Artwork

Nchi za Kenya na Rwanda zinafikiria kuondoa hitaji la viza kwa raia wa Afrika

11/14/20239 minutes, 36 seconds
Episode Artwork

Mali: Mapigano yaendelea kushuhudiwa huku vikosi vya umoja wa Mataifa vikiondoka

Mapigano yameendelea kuripotiwa kati ya jeshi la Mali, wapiganaji wa Tuareg na makundi mengine ya waasi kaskazini mwa taifa hilo wakati huu vikosi vya UN vinapoendelea kuondoka katika eneo hilo. Unadhani  kuondoka kwa vikosi hivyo kumechangia kuongezeka kwa mapigano?
11/13/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Maoni yako kuhusu taarifa zetu juma hili

Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi kuchangia mada yoyote inayokuhusu au ile umeskia katika taarifa zetu. Haya hapa maoni yako kuhusu matangazo yetu juma hili.
11/3/202310 minutes
Episode Artwork

Kenya : Mfalme Charles III akosa kuomba msamaha licha ya matarajio

Katika makala haya tunajadili  hatua ya mfalme wa Uingereza Charlers wa III, kujutia vitendo vya kikoloni vilivyotekelezwa nchini Kenya bila kuomba radhi kama alivyotarajiwa, huku rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, akikiri makosa ya kikoloni yaliofanyika nchini Tanzania, na kuomba msamaha Unazungumziaje matamshi ya viongozi hawa wawili ?Haya hapa baadhi ya maoni yako.
11/2/20239 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Uganda : Raia wabugia pombe kupita kiasi

Kweny makala haya tunajadili hatua ya Wizara ya afya nchini Uganda kusema raia wake zaidi ya milioni 1.2 wamezama kwenye unywaji wa pombe kupita kiasi, hili likitia serikali wasiwasi. Serikali zetu zinaweza kufanya nini kudhibiti unywaji wa pombe kupita kiasi ?Haya hapa baadhi ya maoni yako.
11/1/20239 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Kenya: Mfalme wa Uingereza azuru Kenya

Mfalme wa Uingereza yko nchini Kenya wakati huu masharika ya kiraia yakitaka aombe msamaha kwa vitendo vya kikoloni nchini Kenya vilivyotekelezwa na nchi yake. Je unadhani hili ni sawa ?Skiza baadhi ya maoni yako.
11/1/20239 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Ukataji wa miti kuzungu mkuti kwa mataifa ya Africa na dunia

Nchi ambazo ni makazi ya misitu mikuu mitatu ya mvua duniani mwishoni mwa wiki iliyopita, zilibaliana kushirikiana ili kumaliza ukataji miti na kulinda bayoanuwai lakini zikashindwa kufikia makubaliano dhabiti ya kulinda udhibiti wa kaboni. Katika mahaya haya tumekuuliza iwapo unadhani wakati umewadia nchi zetu kuchukuwa hatua kuzia ukataji wa miti.Haya hapa baadhi ya maoni yako.
10/30/20239 minutes, 48 seconds
Episode Artwork

Makala ya habari rafiki kila Ijumaa, mada huru

10/27/20239 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Mazungumzo ya kutatua mzozo wa sudan yarejelewa mjini Jedah, Saudi Arabia

Mazungumzo ya kutatua mzozo wa sudan yarejelewa mjini Jedah, Saudi Arabia, baada ya mazugumzo ya awali kukosa kuzaa matunda.
10/27/20239 minutes, 45 seconds
Episode Artwork

Rais wa Uganda avitaka vyombo vya usalama kuwashirikisha polisi na raia kuwasaka waasi wa ADF

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa wito kwa vyombo vya usalama kuwashirikisha raia katika maswala ya usalama na kuwawinda waasi wa ADF wanaochangia usalama mdogo nchini na mashariki mwa DRC
10/25/202310 minutes, 11 seconds
Episode Artwork

Kudorora kwa sarafu y anchi za Afrika mashariki dhidi ya dola

Kenya imerekodi sarafu yake kushuka maradufu dhidi ya dola, katika historia ya nchi hiyo, hali ambayo pia inashuhudiwa katika mataifa ya Afrika Mashariki, na kutishia kulemaza zaidi chumi za mataifa haya ya kikanda.
10/25/20239 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Sheria ya afya nchini Kenya kusaidia raia wake

Ijumaa iliyopita nchi ya Kenya ilizindua mswada wake wenye utata unaosemekana kusaidia kuimarisha huduma za afya kwa wananchi wake. Mpango huo wa Afya ukionekana kuwa mzigo zaidi kwa Wakenya wenye mishahara ambao sasa watatozwa 2.75% ya mishahara yao, kugharamia hazina hiyo ya Afya.Tumemuuliza msikilizaji kuwa ana maoni gani kuhusu hatua hii, nchini Kenya?Na je serikali yako imefanya nini kuafikia huduma za afya kwa wote?
10/23/202310 minutes, 8 seconds
Episode Artwork

Wasikilizaji wa RFI Kiswahili watoa mada huru

Ni mada huru ambapo wasikilizaji wetu kutoka kila kona ya dunia wamezungumzia kuhusu habari mbali mbali walizosikia katika matangazo yetu ya juma hili.
10/20/202310 minutes, 13 seconds
Episode Artwork

Ziara ya rais wa Marekani Joe Biden nchini Israeli ina tija yoyote?

Rais wa Marekani Joe Biden amesema nchi yake itashirikiana kwa karibu na Israeli na ameunga mkono kwamba wapiganaji wa kipalestina ndio waliohusika na shambulio la roketi katika hospitali ya Gaza. Tumekuuliza unadhani ziara yake nchini Israeli itabadilisha chochote? Nini kifanyike ilie kuepuka janga la kibinadamu huko Gaza?
10/19/202310 minutes, 4 seconds
Episode Artwork

DRC yaitaka Monusco kuondoka mwishoni mwa mwaka huu wa 2023

Mamlaka ya DRC imeiomba tume ya Umoja wa Mataifa MONUSCO kuwaondoa wanajeshi wake elfu kumi na nne kabla ya mwisho wa mwaka huu. Kwa upande wake katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres yeyé anaamini kuwa hali nchini DRC inazidi kuzorota. Tumekuuliza unadhani ni wakati mwafaka kwa MONUSCO kuondoka nchini DRC?Jeshi la Congo FARDC linaweza kurejesha usalama na amani nchini humo? Kukuletea makala hii naitwa Ruben Lukumbuka
10/18/202310 minutes, 9 seconds
Episode Artwork

Rais wa DRC alegeza makataa ya hali ya dharura kwenye majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri

Makala ya habari rafiki imeangazia hatua ya serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kutangaza kuwa italegeza hatua kwa hatua hali ya dharura kwenye majimb ya Kivu kaskazini na Ituri, miaka miwili baada ya kuwekwa kwenye maeneo hayo kufuatia utovu wa usalama
10/16/202310 minutes, 6 seconds
Episode Artwork

Maoni ya waskilizaji kuhusu mzozo mpya baina ya Israel na Palestina

Mapigano yanaendelea kati ya wapiganaji wa Hamas na wanajeshi wa Israel, baada ya kundi la Palestina, kufanya mashambulio ya kushtukiza dhidi ya Israel kutoka Gaza, katika ongezeko kubwa la mzozo kati ya Israel na Palestina.Unazungumziaje mzozo huu?Unadhani jumuiya ya kimataifa imeshindwa kuzisaidia pande hizo mbili kupata suluhu?
10/9/202310 minutes, 1 second
Episode Artwork

Maoni yako kuhusu taarifa zetu juma hili

Kila siku ya Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi kuchangia mada yoyote unayopenda kuhusu taarifa zetu au kile kinaendelea pale ulipo. Juma hili tumekuwa na maoni chanya hasi kuhusu maswala mbali ya yale yanayoendelea duniani.Skiza makala haya.
10/7/202310 minutes
Episode Artwork

Uganda na Kenya zapiga marufuku za safari za ngambo

Serikali za Uganda na Kenya zimepiga  marufuku safari za ngambo za afisa wa serikali zisizo kuwa za lazima, lengo likiwa kubana matumizi ya pesa za umma.  Ni hatua inayotokana kile zile hizo zimesema baadhi ya safari hizo ahazina manufaa kwa taifa. Haya hapa baaadhi ya maoni yako.
10/5/202310 minutes, 1 second
Episode Artwork

Wanawake wachukuwa majukumu muhimu katika familia

Utafiti wa hivi punde nchini Kenya, umeonesha kuwa idadi kubwa ya wanawake wamechukuwa majukumu ya wanaume nyumbani, hasa katika maeneo ya mijini.  Wengi wakionekana kusimamia majukumu muhimu kwa familia Je unakubaliana na utafiti huu kwamba wanaume wameacha kuteleza majukumu yao kwa jamii?  Haya hapa baadhi ya maoni yako.
10/4/20239 minutes, 39 seconds
Episode Artwork

Kinyanganyiro cha urais DRC chapamba moto

Nchini DRC   muungano wa kisiasa wa chama tawala Sacred Union umemteua rais Felix Tshisekedi , kuwania tena kiti cha urais kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba, ambapo atapambana tena  na  mpinzani Martin Fayulu, Moise Katumbi na mshindi wa tunzo ya mani ya Nobele  daktari Denis Mukwege miongoni mwa wagombea wengine. Unazungumziaje hatua Denis Mukwege kuwania Urais.Je unafikiri DRC imejitarisha vilivyo kwa uchaguzi huu ?Haya hapa baadhi ya maoni yako.
10/3/20239 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Matayarisho ya mvua za el Nino Africa Mashariki

Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati zimeanza kuchukua mikakati ya kujiweka tayari kwa ajili ya kudhibiti athari zinazotokana na mvua ya El Nino inayotarajiwa kuaanza kunyesha mwezi huu. Mamlaka ya hali ya hewa zimeonya kuhusu athari zinazoweza kujitokeza.Nchi yako imejiandaa vya kutosha? Haya hapa baadhi maoni yako. 
10/2/20239 minutes, 46 seconds
Episode Artwork

Vijana wengi wa Afrika wahatarisha maisha yao kwa kujaribu kwenda Ulaya

9/28/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Maoni ya waskilizaji kuhusu hatuwa ya Somalia kuomba ARTMIS kuchelewa kuondoka

Haya ni maoni ya waskilizaji wa RFI KIswahili kuomba Umoja wa Afrika kuchelewesha kuondoa vikosi vyake nchini Somalia
9/28/20239 minutes, 32 seconds
Episode Artwork

Upinzani kuzuiliwa kufanya mikutano Africa

Serikali nyingi za Afrika zinazodai kuheshimu demokrasia zimeendelea kuminya uhuru wa vyama vya upinzani kufanya mikutano ya kisiasa, hivi punde tukishuhudia chama cha upinzani nchini Uganda NUP chake Bobi Wine, kikizuiwa kufanya mikutano yake ya kisiasa. Hali ikoje nchini mwako ? Haya hapa baadi ya maoni yako
9/20/20239 minutes, 58 seconds
Episode Artwork

Kupanda kwa bei za mafuta katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki

Nchi za Kenya, Burundi na DRC, zimetangaza bei mpya za mafuta, wakati huu nauli za usafiri na bei ya vyakula ikiongezeka.Nchini mwako hali ikoje?Mataifa ya Afrika Mashariki yanapaswa kufanya nini ilikudhibiti bei za bidhaa?
9/19/20239 minutes, 37 seconds
Episode Artwork

Utawala wa kijeshi nchini Mali, Niger na Burkina Faso wasaini mkataba wa kushirikiana kijeshi,

Utawala wa kijeshi nchini Mali, Niger na Burkina Faso umesaini mkataba wa ushirikiano wa kijeshi, mataifa haya yakiahidi kufanya kazi kwa pamoja kuzuia uvamizi wowote kutoka nje.Na kwenye makala yetu utaskia maoni tofauti tofauti ya iwapo hatua hii ya kushirikiana kijeshi kati ya mataifa haya inaweza zuia tishio la kijeshi kutoka nje na iwapo mpango huo utafanikisha vita dhidi ya makundi ya kijihadi.
9/18/202310 minutes, 8 seconds
Episode Artwork

Mada ya msikilizaji

Katika makala haya tunaangazia maoni ya msikilizaji kuhusu matukio ya juma lote yakiwemo Mafuriko Libya na tetemeko la ardhi Morocco
9/15/202310 minutes, 18 seconds
Episode Artwork

Umoja wa Afika wajumuishwa kwenye muungano wa G20

Umoja wa Africa umejumuishwa kuwa mwanachama wa kudumu katika muungano wa G20 katika mkutano uliokamilika nchini India na sasa una nafasi sawa na Umoja wa Ulaya EU. Nini mtazamo wako kuhusiana na hatua hii?Unadhani AU sasa utakuwa na ushawishi katika maswala ya ulimwengu. Kwenye makala haya utaskia maoni tofauti ya wasikilizaji kuhusiana na swala hili.
9/13/20239 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Tetemeko la ardhi nchini Morocco: Mamlaka zakubali msaada kutoka Hispania, UAE na sio Ufransa

Karibu watu elfu tatu wamepoteza maisha kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Jumamosi iliyopita nchini Morocco. Mamlaka zinakubali msaada wa kibinadamu wa dharura kutoka Uingereza, nchi za Kiarabu, na Hispania lakini sio Ufaransa, ambayo ina wakazi wapatao milioni 2 kutoka Morocco.TumekuulizaJe, siasa zinapaswa kupewa kipao mbele badala ya misaada ya dharura kwa wananchi? Kwenye makala haya utaskia maoni tofauti ya wasikilizaji kuhusiana na swala hili.
9/13/202310 minutes, 7 seconds
Episode Artwork

EAC kuongezewa mda mashariki mwa DRC hadi Disemba

Jumuiya ya Afrika mashariki imeamua kuongeza mda wa jeshi la EAC mashariki mwa DRC hadi Disemba.Mei mwaka jana Rais Felix Tchisekedi alikosoa vikali jeshi hili lakikanda kwa kutokua na ufanisi katika kupambana na waasi wa M23.Kwenye makala haya utaskia maoni tofauti ya wasikilizaji kuhusiana na swala hili.
9/13/202310 minutes
Episode Artwork

Jeshi nchini Gabon lamtangaza Brice Nguema kuwa rais wa mpito

Mwishoni mwa juma Gabon ilifanya uchaguzi  na kutangaza matokeo yake  siku ya jumatano  kabla tuu ya mapinduzi kufanyika na yaliyomuondoa Ali Bongo madarakani.Na tumemuuliiza msikilizaji  nini maoni yake kuhusiana na mapinduzi hayo ya kijeshi.
8/31/20239 minutes, 58 seconds
Episode Artwork

Je, uchaguzi nchini Zimbabwe ulikuwa huru na haki ?

Tunaangazia uchaguzi ambao umekamilika wiki iliyopita nchini Zimbabwe ambapo Rais Emmerson Mnangagwa alitangazwa mshindi wa uchaguzi nchini humo kwa asilimia 53 ya kura wakati mpinzani wake mkuu Nelson Chamisa akikataa matokeo hayo na kudai kuibiwa kura.
8/29/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Kiongozi wa Wagner Yevgeny Prigozhin azikwa

Tunaangazia Kifo cha kiongozi wa Wagner Yevgeny Prigozhin kutokana na ajali ya ndege ambacho kimezua maswali mengi likiwemo suala la ulipizaji kisasi kutoka kwa rais wa Urusi Vladmir Putin miezi miwili tu baada ya uasi wa muda mfupi.Tumemuuliza msikilizaji ikiwa anafikiri kifo chake kilikuwa ajali ya kawaida ama uhalifu ?Kifo chake kinaathiri vipi shughuli za Wagner barani Afrika ?
8/29/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Siku ya kimataifa ya kukumbuka Biashara ya Utumwa na ilivyotokomezwa

Juma hili dunia imeadhimisha kumbukizi ya kumalizika biashara ya utumwa, wakati huu biashara ya binadamu ikishamiri, maelfu ya raia hasa kutoka Afrika wakisafiri na kusafirishwa kwenda Ulaya kutafuta maisha.Pamoja na wasikilizaji wetu tunaangazia nini kifanyike kukomesha biashara ya binadamu? Ungana na mwandishi wetu kupata mengi zaidi
8/24/202310 minutes, 1 second
Episode Artwork

Vita dhidi ya kundi la Al-Shabaab nchini Somalia

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud na serikali yake wameimarisha vita vikali dhidi ya kundi hilo ambalo kwa muda sasa limekuwa likitekeleza mashambulio katika baadhi ya maeneo kwenye taifa hilo pamoja na nchi jirani.
8/22/20239 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Umoja wa Mataifa wataka hatua za haraka kuchukuliwa kutatua mzozo wa Sudan

8/17/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Sarafu za kidijitali zaanza kupata umaarufu barani Afrika

8/16/20239 minutes, 58 seconds
Episode Artwork

DRC: Viongozi wakutana Kinshasa kutathmini hali ya dharura Kivu Kaskazini na Ituri

8/15/202310 minutes
Episode Artwork

Afrika mbioni kutafuta suluhu ya changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana

Mwishoni mwa juma lililopita, dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya vijana, maadhimisho yaliofanyika wakati huu idadi kubwa ya vijana katika nchi za Afrika wakisalia bila ajira. Unafikiri nchi za Ukanda wa Afrika zifanye nini kuongeza nafasi za ajira kwa vijana? Bonyeza sauti ili usikilize maoni ya wasikilizaji.
8/14/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Mada Huru: Msikilizaji kuzungumzia habari alizoziskia wiki nzima

Habari zilizoangaziwa ni pamoja na msimamo aliouchukua rais wa Uganda Yoweri Museveni, baada ya benki ya dunia kusitisha ufadhili kwa taifa hilo kutokana na kuweka sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.
8/14/202310 minutes
Episode Artwork

Kenya: Serikali na upinzani waanza kutafuta suluhu ya kisiasa

8/10/20239 minutes, 47 seconds
Episode Artwork

Nchi za Afrika kuwa na katiba kuruhusu marais wastaafu kushtakiwa kwa makosa wakati wa utawala wao

8/9/20239 minutes, 49 seconds
Episode Artwork

Ajali za boti zaendelea kuripotiwa Afrika Mashariki

8/8/20239 minutes, 49 seconds
Episode Artwork

Upinzani nchini DRC walalamikia kuhangaishwa na serikali kuelekea uchaguzi wa mwezi Disemba

8/7/20239 minutes, 42 seconds
Episode Artwork

Mada huru kama alivyochagua msikilizaji

8/4/202310 minutes, 1 second
Episode Artwork

Mataifa ya Afrika yameahidi kudhibiti kelele kutoka kumbi za burudani na uraibu wa pombe

8/3/202310 minutes, 9 seconds
Episode Artwork

Kikosi cha umoja wa Afrika nchini Somalia ATMIS kinaendelea kupunguza idadi ya wanajeshi wake

8/3/202310 minutes, 2 seconds
Episode Artwork

ECOWAS imeutaka utawala wa kijeshi nchini Niger kurejesha utawala wa kiraia ndani ya wiki moja

ECOWAS imetishia kutumia nguvu na kutangaza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Niger ,iwapo utawala wa kijeshi uliofanya mapinduzi ,hautarejesha utawala wa kiraia ndani ya wiki moja
8/1/202310 minutes, 1 second
Episode Artwork

Rais wa zamani wa Nigeria Olesegun Obasanja anatazamiwa kuwa mpatanishi Kenya

7/31/20239 minutes, 57 seconds
Episode Artwork

Mada ya msikilizaji

7/29/202310 minutes, 13 seconds
Episode Artwork

Mkutano wa siku mbili kati ya Urusi na Afrika umeanza rasmi,Saint Petersburg.

Kongamano kati ya Urusi na nchi za Afrika limeanza wakati huu Moscow ikizituhumu nchi za Magharibi haswa Marekani kwa hujuma kwa kushinikiza nchi za Afrika kutohudhuria.Rais wa Urusi Vladmir Putin hii leo amewapokea viongozi hao katika mji wa Saint Petersburg.
7/27/202310 minutes
Episode Artwork

Upinzani umetishia kuishtaki serikali ya Kenya kwa ukatili wa polisi wakati wa maandamano

Kenya imeshtumiwa kwa kosa la polisi kutumia nguvu kupitiliza kuwadhibiti waandamanaji waliokuwa wakiandamana kupinga kupanda gharama ya maisha
7/26/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Siku 100 zimekamilika tangu kuanza kwa mapigano nchini Sudan

Maelfu ya raia wamekimbilia nchi zingine ili kuepuka vita vya pande mbili nchini Sudan wakati huu mazungumzo ya kutafta suluhu yakikosa kufua dafu
7/25/202310 minutes
Episode Artwork

Mali yaidhinisha katiba mpya baada ya kura ya maoni ya mwezi uliopita

Nchi ya Mali kupitia kiongozi wake wa kijeshi Kanali Assimi Goita imetangaza katiba mpya ya nchi hiyo na ambayo upinzani imepinga na hivyo kutishia maandamano.Uchaguzi wa nchi hiyo ulitarajiwa kufanywa mnamo Februari 2022, lakini ukaahirishwa hadi Februari 2024.
7/24/202310 minutes
Episode Artwork

Makala habari rafiki, Mada huru

7/22/20239 minutes, 54 seconds