Winamp Logo
Afrika Ya Mashariki Cover
Afrika Ya Mashariki Profile

Afrika Ya Mashariki

Swahili, Political, 1 season, 47 episodes, 7 hours, 43 minutes
About
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.
Episode Artwork

Harakati mpya za vikosi vya SADC mashariki ya DRC

Vikosi vya SADC vinapelekwa mashariki mwa DRC kusaidia kurejesha amani. Hatua inayokuja baada ya kuondoka kwa vile vya Afrika Mashariki ambavyo vilituhumiwa na serikali ya Kinshasa kushindwa majukumu yao.
1/31/20249 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Muhula wa pili wa rais Felix Tshisekedi nchini DR Congo

Makala ya wiki hii  yanaangazia ahadi za rais Felix Tshisekedi katika muhula wake wa pili kama kiongozi wa DRC.
1/26/20249 minutes, 57 seconds
Episode Artwork

Kufunguliwa kwa shule nchini Tanzania

Wanafunzi wengi katika mataifa ya Afrika Mashariki wamerejea shuleni wiki hii.
1/17/20249 minutes, 16 seconds
Episode Artwork

Hatua Somalia kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa hatua ya Somalia kujiunga na EAC, itaisaidia katika vita dhidi ya makundi ya watu wenye silaha
12/1/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Wanawake katika sanaa ya uchoraji nchini Tanzania

Makala ya wiki hii yanaangazia namna wanawake nchini Tanzania wamegeukia sanaa hii ya uchoraji.
11/9/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Uelewa wa wananchi wa Mwanza kuhusu mvua za El Nino

Baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki yameendelea kufanya maandalizi kuelekea mvua za El Nino.
11/1/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Nishati inachangia asilimia kubwa kwa ukuaji wa Uchumi wa mataifa

Sekta ya Nishati ndiyo mhimili muhimu wa maendeleo ya taifa lolote lile, Mathalan takwimu zinaonesha, mahitaji ya juu ya umeme yameongezeka ambapo serikali ya Tanzania inasema kuwa muelekeo ni kuongeza katika Gridi ya Taifa MW 218.67 na kufikia MW 1,913.22 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2022/23.
10/28/20239 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Biashara ya samaki na dagaa jijini Mwanza nchini Tanzania.

Makala ya wiki yanaangazia namna wanawake waendeleza biashara ya samaki nchini Tanzania
10/18/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Tanzania: Jamii zinavyo shiriki katika utunzaji wa hifadhi ya Ruaha

Jamii zinavyo shiriki katika utunzaji wa hifadhi ya Ruaha
10/11/20239 minutes, 58 seconds
Episode Artwork

Juhudi za kusambaza umeme nchini Tanzania

Zaidi ya watu milioni mia tano kusini mwa jangwa la sahara wanakabiliwa na tatizo la umeme.
9/22/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Nafasi ya muungano wa BRICS kwa mataifa ya Afrika

Viongozi wa kundi la mataifa ya BRICS - Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini hvi karibuni wamekutana mjini Johannesburg nchini Afrika kusini na ajenda muhimu mezani ikiwa ni kukubali ombi la kuongeza wanachama wapya ndani ya muungano huo. Tunaangazia mkutano huu wiki hii.
8/29/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Vijana na ushiriki wa fursa ndani ya Afrika mashariki

Namna Jumuiya ya Afrika Mashariki inawapa vijana nafasi na fursa za kujiendeleza kimandeleo.
8/16/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Juhudi za muungano wa makabila kusaka amani DRC

Ukabila umetajwa kuwa mojawapo ya mambo yanayochangia katika utovu wa usalama nchini DRC
8/10/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Mgogoro wa Kenya na athari kwa uchumi Afrika

Makala ya wiki yanaangazia athari za kiuchumi zinazotokana na maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama ya maisha nchini Kenya kwa bara Afrika
7/29/20239 minutes, 49 seconds
Episode Artwork

Matumizi ya dawa za kulevya yanavyokatiza ndoto za vijana

Idadi ya vijana wamepoteza ajira na hata familia zao kutokana na athari za matumizi ya dawa za kulevya.
7/19/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Bakteria wanao shambulia mpunga nchini Tanzania

Baadhi ya wakulima wa mpunga tayari wanaiipa bakteria hiyo jina la Uviko wa mchele 
7/14/20239 minutes, 58 seconds
Episode Artwork

Uelewa wa wakazi wa Jiji la Mwanza juu ya matumizi ya sarafu moja

Mwandishi wa Martin Nyoni amezungumza na wakazi wa Mwanza nchini Tanzania kuhusu uelewa wa matumizi ya sarafu  Mpango huu wa viongozi wa jumuia hii yenye wanachana saba kwa sasa ulifasiliwa na baadhi ya wachumi kuwa ni sawa na kusukuma tofali kwenye kina kirefu cha bahari bila kuwa na matarajio ya kulifikia tena tofali hiloUmoja wa Fedha wa Afrika Mashariki (EAMU) ni hatua muhimu katika mchakato wa Mtangamano wa Kikanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Itifaki ya EAMU ilipitishwa kwa mujibu wa Mkataba wa EAC na kutiwa saini tarehe 30 Novemba 2013 lakini wananchi wa jumuiya hii wao wanasema kuwaKaribu katika Makala ya Afrika mashariki hii leo tunatuwa nchini Tanzania tukiangaza uelewa wa wakazi wa taifa hii la ukanda wa Afrika mashariki juu ya mchakato wakuwa na matumizi ya sarafu moja sanjali na maoni ya wanazuoni wakati ikiwa ni muongo moja sasa tangu kusainia kwa makubalino yakuwa na sarafu moja.
7/6/20239 minutes, 42 seconds
Episode Artwork

Juhudi za kupambana na uchafuzi wa Ziwa Victoria kaskazini Magharibi mwa Tanzania

Mwandishi wetu Martin Nyoni ameandaa Makala ya haya akiwa mjini Mwanza
6/14/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Ndoa za utotoni zinavyo sababisha fistula Afrika Mashariki

Ndoa za utotoni zinatajwa kusababisha athari kwa watoto wa kike kisaikolojia, kiafya, kiuchumi na hata Kwenda mbali zaidi kusabisha athari za afya Kuzidi kushadidi kwa ndoa za utotoni katika mataifa ya ukanda wa Afrika mashariki utajwa moja ya kisababisha kwa binti kupata ugonjwa wa fistula ya uzazi ambayo upatikana wakati wa kujifungua.Fistula ya uzazi inachangia asilimia 8 ya vifo vya uzazi, na asilimia 90 ya visa vya kujifungua watoto wafu huku wataalamu wakieleza kuwa watoto wa kike waliopo kwenye ndoa za utotoni wapo hatarini zaidi kupata ugonjwa huo.Zubeda Maulidi mwenye umri wa miaka 18 sasa siyo jina lake halisi mkazi wa Meatu mkoani Simiyu,aliolewa akiwa na umri wa miaka 17 kasoro huku mumewe akiwa na umri wa miaka 21 anasema alikatisha masomo mara baada ya kuhitimu darasa la saba na kutumbukia katika ndoa za utotoniInakadiriwa kuwa wanawake na wasichana 500,000 katika nchi zaidi ya 55 za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Asia na Pasifiki, nchi za Kiarabu, Amerika Kusini na Caribbea wanakadiriwa kuishi na fistula, huku maelfu zaidi ya visa vipya hutokea kila mwaka
5/31/20239 minutes, 58 seconds
Episode Artwork

Wafugaji wanavyo changia kuharibu mazingira

Makala ya wiki hii yanaangazia jinsi wafugaji wanavyochangia katika uharibifu wa mazingira mjini Iringa Tanzania
5/24/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Vijana na Ubunifu mkoani Mwanza nchini Tanzania

Vijana wengi huchangia katika nguvu kazi ya kitaifa kama njia moja ya kuboresha na kuimarisha uchumi wa kitaifa.
5/18/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Vijana na muziki wa Injili nchini Tanzania

Katika ukanda wa Afrika mashariki muziki wa kizazi kipya ndio wenye kubamba kutoka pembe mbalimbali nchini Tanzania ukiitwa Bongo fleva ukiwa na maadhi tofauti tofauti kama ilivyo kwa muziki wa genge nchini Kenya
5/12/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Uhuru wa vyombo vya habari

Martin Nyoni anaangazia uhuru wa habari nchini Tanzania
5/3/20239 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Ndondi kwa Wanawake nchini Tanzania

Wakati mchezo wa masumbwi ukizidi kukua kwa kasi katika nchi za afrika mashariki, nchini Tanzania kufanya vizuri kwa mabondia kadhaa wakizazi kipya kama vile Hassan Mwakinyo,Kkarim Mandonga, Twaha Kiduku na wengine kadhalika kumezidi kusisimua wasichana na wanawake kuanza kujikita katika mchezo huu…
4/20/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Utunzaji wa vyanzo vya maji

Leo katika makala ya Afrika Mashariki tunajikita kuangazia namna ambavyo utunzi wa vyanzo vya maji ni muhimu katika jamii haswa kuzuia uharibifu wa mazingirza na uchafuzi wa bahari.
3/29/20239 minutes, 58 seconds
Episode Artwork

Wavumbuzi wa sayansi Afrika Mashariki

Ndoto za wavumbuzi waki sayansi kutoka nchini Tanzania kama walivyo wengine kutoka nchini za ukanda wa Afrika mashari kwa ujumla ni kuhakikisha kuwa wanazalisha au kuvumbua vifaa ambavyo vinautambulisho wa mataifa yao karibu katika makala ya Afrika mashariki hii leo tupata simulizi ya vijana walio acha kazi na kuaumua kujiajili wenyewe katika uvumbuzi wakisayansi na Teknolojia na kisha kuwafundisha wanafunzi wa iliwaweze kupata mafunzo kwa vitendo pindi wawapo shuleni au majumbani.
3/15/20239 minutes, 41 seconds
Episode Artwork

Vijana na Ufundi wa vyombo vya moto

Makala ya Afrika mashariki wiki hii yanaangazia vijana walio jitupa katika kazi ya ufundi wakutengeneza vyombo vya moto nchini Tanzania ni nini sababu ya wao kuingia katika kazi hii ya yapi matarajio yao kwa siku za usoni .
3/10/20239 minutes, 27 seconds
Episode Artwork

Rais Samia aruhusu vyama vya upinzani kufanya mikutano ya siasa

Karibu katika Makala ya Afrika mashariki hii leo tuna tuama nchini Tanzania kuangaza na kulika kuanza tena kwa mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa nchini humo nini matarajio na mapokeo ya wafuatilizi wa maswala ya siasa katika taifa hili lililo shuhudia ukimya wa miaka saba yakutofanyika kwa mikutano ya hadhara mwandalizi na msimulizi wa makala haya naitwa Martin Nyoni nasema karibu jamvini tuwe sote hadi tamati .
2/22/20239 minutes, 52 seconds
Episode Artwork

Nini hatima ya mzozo wa utovu wa usalama Mashariki mwa DRC ?

Tunaangaza na kumulika kuzidi kushadidi kwa mgogoro katika eneo la Mashariki mwa DRC nini kifanyike ili kupatikana kwa suluhu ya kudumu katika taifa hilo ambalo linaifanya Jumuiya ya Afrika mashariki kuwa soko kumbwa la huduma na bidhaa Mwandalizi na msimulizi wa makala ni Martin Nyoni
1/18/20239 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Changamoto za wagonjwa wa ukoma nchini Tanzania

Tunaangazia juu ya kituo cha wagonjwa wa ukoma na vikongwe kilichoko Kolandoto, mkoani Shinyanga, Tanzania. RFI imefika kituo cha Kolandoto ambapo kituo hicho kilichojengwa mwaka 1914 maalumu kwa wagonjwa wa Ukoma, leo hii kituo hicho kimegeuka kimbilio la vikongwe wanaotuhumiwa kwa uchawi ili wasiuawe na jamii inayowazunguka.  
1/25/20229 minutes, 44 seconds
Episode Artwork

Changamoto za usalama barabarani nchini Tanzania

Leo tunaangazia juu ya  changamoto za usalama barabarani nchini Tanzania. Kwa namna ya pekee utawasikia wadau mbalimbali wa vyombo vya moto huko mkoani kagera wakiangazia changamoto walizonazo ikiwezo ukosefu wa mafunzo ya utambuzi wa alama za barabarani lakini pia kutojua sheria za barabarani kwa madereva na abiria. 
1/18/20229 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Kupambana na ulanguzi wa binadamu Afrika Mashariki

Leo tunaangazia juu ya mapambano dhidi ya biashara, unyonywaji na usafirishaji binadamu kwenye ukanda wa afrika ya mashariki. Kwa mjibu wa mtaalamu wetu Bi. Winnie Mtevu kutoka Nairobi Kenya, vitendo hivo viovu dhidi ya binadamu vinafanywa ndani na hata nje ya mipaka ya nchi husika,  ikiwa  ni kinyume kabisa na haki za binadamu. 
1/11/20229 minutes, 29 seconds
Episode Artwork

Matukio makubwa yaliyotokea mwaka 2021 Afrika Mashariki na Kati

Leo tunaangazia sehemu ya pili na ya mwisho ya baadhi ya makala zilizoletwa kwako mwaka uliopita wa 2021. Baadhi yake ni pamoja na utengenezaji wa nishati mbadala nchini Tanzania,  uhusiano baina ya Burundi na Rwanda, wanafunzi kuagizwa kuni shule za msingi Tanzania, pia pendekezo la kuundaa mkoa mpya wa Chato nchini Tanzania.
1/5/20229 minutes, 52 seconds
Episode Artwork

Mkusanyiko wa baadhi ya matukio ya mwaka 2021

Tunaangazia sehemu tu ya baadhi ya makala zilizoletwa kwako mwaka huu wa 2021. Baadhi yake ni pamoja na uhusiano baina ya jamii ya wakimbizi na wenyeji Tanzania, Uhusiano baina ya wenyeji na raia wa Burundi na Tanzania, wasomi wa Afrika ya Mashariki kusaka ajira nje ya nchi zao, pamoja na Rushwa nchini Burundi.
12/28/20219 minutes, 52 seconds
Episode Artwork

Changamoto za mimba za watoto wa kike nchini Tanzania

Leo tunaangazia juu ya  tatizo la mimba kwa watoto wa kike nchini Tanzania hususan nyakati hizi wanafunzi wawapo likizo. Baadhi ya wadau wakiwemo wazazi na viongozi wa kiroho wanaangaziatatizo hilo lilalotatiza ndoto za mtoto wa kike nchini Tanzania.
12/22/20219 minutes, 51 seconds
Episode Artwork

Changamoto za waendesha vyombo vya moto nchini Tanzania

Leo tunaangazia juu ya  changamoto zinazowakumba waendesha vyombo vya moto nchini Tanzania. Kwa namna ya pekee tutajikita kuongea na wadau wa magari na pikipiki huko mkoani Kagera nchini Tanzania akiangazia kuwa baadhi ya changamoto ni pamoja na ukosefu wa mafunzo ya sheria zabarabarani. Waendesha vyombo vya motona baadhi ya abiria wanaeleza uhitaji mkubwa wa elimu juu ya alama za barabarani
12/14/20219 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Burundi - Wafuasi wa upinzani kukamatwa

Julian Rubavu anaangazia  siasa za Burundi hususan taarifa za kupotea na kukamatwa wafuasi wa vyama vya upinzani kikilengwa zaidi chama cha CNL kinachoongozwa na Agathon Rwassa.
12/8/20219 minutes, 58 seconds
Episode Artwork

Kiwanda cha kutengeneza mkaa mbadala nchini Tanzania

Tunaangazia juu ya uhifadhi na utunzaji mazingira nchini Tanzania. Kwa namna ya pekee, RFI imetembelea kiwanda cha kutengeneza mkaa mbadala tofauti na uchomaji miti. Shirika lisilo la kiserikali ya REDESO (relief for development society) ndio linajishughulisha na upatikanaji wa nishati mbadala kwa ajili ya kuhudumia wakimbizi wasio jiweza kambini Nyarugusu, mkoani Kigoma,
11/30/20219 minutes, 58 seconds
Episode Artwork

Uhusiano wa raia wanaoishi mpakani mwa taifa la Burundi na Tanzania

 Kwenya makala haya mwandishi wetu, Juliani Rubavu, anaangazia  uhusiano baina ya raia wa Tanzania wanaoishi kwenye mpaka wa Manyovu wilayani Buhigwe mkoani Kigoma, na jirani zao wa tarafa ya Mabanda  mkoani Makamba, nchini Burundi. Wenyeji wa pande zote wanaeleza kuwa uhusiano wao ni mzuri na wanashirikiana kwa kila jambo.   __________________________
11/24/20219 minutes, 57 seconds
Episode Artwork

Umuhimu wa michezo kwa wanafunzi nchini Tanzania

Leo tunaangazia umuhimu  wa Michezo kwa Mwanafunzi kwa Afya ya mwili na akili. Kwenye kipindi hiki utawasikia baadhi ya wadau wakiwakilishaa makundi mbali mbali ya watoto, walezi, wazazi, na wataalamu nchini Tanzania wakiangazia umhimu wa michezo.  
10/27/20219 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Uhuru wa kujieleza kupitia mitandao ya kijamii nchini Tanzania

Leo tunaangazia kuhusu uhuru wa kujieleza na kutoa maoni pamoja na athari za sheria ya mitandao nchini Tanzania. Kwa miaka ya hivi karibuni nchini Tanzania kumekuwepo na minong’ono ya hapa na pale ndani ya jamii kuhusu misingi ya kidemokrasia, uhuru wa kikatiba,  na sheria za mitandao.
10/13/20219 minutes, 42 seconds
Episode Artwork

Changamoto za walemavu nchini Tanzania

Tunaangazia juu ya changamoto za ujasiriamali kwenye vikundi vya walemavu nchini Tanzania. Kwa namna ya pekee tutawasikia baadhi ya walemavu na wadau wengine wanaohusika kuhakikisha mlemavu anajiwezesha kiuchumi huko mjini Bukoba, mkoani Kagera, Magharibi mwa Tanzania.
10/5/20219 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Fursa za vijana kujiajiri katika nchi za Afrika Mashariki

Juhudi za vijana wa ukanda wa Afrika ya Mashariki na kati ambapo licha ya changamoto za hapa na pale kiuchumi na kijamii, lakini kwa namna ya pekee baadhi ya vijana wa ukanda huu wanajibidisha  kuhakikisha wanajiajiri au kuajiriwa huku wakitaja nidhamu na uaminifu kwenye jamii inayowazunguka ndio siri ya mafanikio yao. 
9/29/20219 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Uhusiano kati ya Rwanda na Burundi

Leo tunaangazia juu ya Uhusiano baina ya Burundi na Rwanda. Kwa zaidi ya miaka mitano sasa hali ya uhusiano baina ya nchi hizo mbili umezorota. Baadhi ya sababu zilizotajwa na kila upande, Rwanda inataja Burundi kuhifadhi baadhi ya wahusika wa uhalifu wa kibinadamu waliokimbilia Kongo, na kwa upande mwingine Burndi inataja kwanda kuhifadhi walifanya jaribio la mapinduzi mwaka 2015.
8/31/20219 minutes, 49 seconds
Episode Artwork

Hatua ya serikali ya Burundi kuwaadhibu maafisa wake

Leo tunaangazia juu ya hatua ya serikali ya Burundi kusimamisha baadhi ya viongozi na maafisa waandamizi wa serikali iliyoko madarakani wengi wao wakiwa watumishi wa ikulu.  Serikali ya Burundi ilifahamisha kwamba waliosimamishwa kazi akiwemo aliyewahi kuwa msemaji wa serikali Willy Nyamitwe na wengine, wamesimamishwa kupisha uchunguzi kwa tuhuma za kuchelewa kazini.
8/25/20219 minutes, 57 seconds
Episode Artwork

Unywaji wa pombe haramu nchini Kenya na Tanzania

Leo tunaangazia juu ya Kinywaji haramu cha ‘Gongo’ nchiniTanzania na ‘Chang’aa’ nchini Kenya.  Baadhi ya wanywaji wa pande zote walioongea na RFI wanaomba serikali za nchi zao kuhalalisha kinywaji hicho cha Gondo ambapo kwa Kenya wao huiita Chang’aa, na kwa upande wa Tanzania huiita Gongo au Supu ya Mawe au Machozi ya Simba na kadhalika.
8/17/20219 minutes, 29 seconds
Episode Artwork

Maadili ya viongozi wa umma nchini Tanzania

Leo tunaangazia juu ya Maadili ya Viongozi wa Umma nchini Tanzania. Tutakuwa na baadhi ya wachambuzi ambao ni Ndugu Mjungu akiwa Karagwe mkoani Kagera, pamoja na Dokta. Peter Bujari mchambuzi wa kisiasa, kiuchumi na mshauri wa sera akiwa jijini  Dar es Salaam.
8/10/20219 minutes, 31 seconds