Winamp Logo
Jua Haki Zako Cover
Jua Haki Zako Profile

Jua Haki Zako

Swahili, National/National politics/National assembly, 1 temporada, 44 episodios, 0 horas, 0 minutos
Acerca de
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.
Episode Artwork

Haki ya kutali Africa bila vikwazo

Ni vigumu kwa watu wachache kutumia usafiri wa beskeli hapa Africa lakini Yusufu raia wa Morocco kwake kutali Africa kwa kuendesha beskeli ni kama kazi. Benson Wakoli aliketi chini na Yusuf, kuthamini safarizake barani Africa na jinsi gani amekuwa akipokelewa na raia wa mataifa mengine.
21/2/20240 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Valentine : Haki ya wanaume na wanawake

Kila  mwaka Feb 12 dunia huadimisha siku ya wapendanao, raia wengine wakionesha mapenzi kwa wachumba, pamoja na marafiki. Lakini  nini maana ya valentine? kufahamu  zaidi skiza makala haya.
17/2/20240 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Kenya : Viongozi wa dini wapinga ushoga

Kwenye haya tunajadili hatua viongozi wa dini nchini Kenya kulitaka bunge kuanza uchuguzi wa haraka kuhusiana na madai kwamba kuna njama ya makusudi kueneza sera za ushoga nchini Kenya. Viongozi hao wa dini wanadai kwamba kuna mpango wa ambao tayari umepangwa kupinga vita dhidi ya mashoga na wasagaji, na watu wanaodai kutetea haki za mashoga, hulka ambayo inaenda kinyume kabisa na maadili ya jamii za  kiafrica. Kufahamu zaidi skiza makala haya. 
9/2/20240 minutos
Episode Artwork

DRC : Je haki za raia zilikiukwa kipindi cha uchaguzi?

Katika makala haya tunapiga darubini kuangazia haki za raia wa DRC wakati wa kipindi cha kampeini za uchaguzi, na baada ya uchaguzi. Mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu Mapendo Kusudi alifanya mazungumzo kupitia njia ya simu na mwandishi wetu Benson Wakoli. Kufahamu zaidi skiza makala haya.
3/2/20240 minutos
Episode Artwork

Haki ya mtoto kupata elimu ( Fizi)

Katika haya  tunaangazia haki ya watoto kupata elimu ambapo utaskia kwa wadau mbalimbali walioazisha kutuo cha elimu cha Fizi kinatoa elimu ya somo la kifaransa  nchini Kenya  kwa watoto wakimbizi kutoka nchini DRC , Rwanda na Burundi. Kituo hiki  kilianzishwa mwaka 2014 lengo likiwa kuwasaidia watoto wakimbikizi kutoka mataifa ya Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ili kuendelea kujifunza na kuendeleza tamaduni ya lugha ya Kifaransa,hasa ikizingatiwa kwamba nchini Kenya raia wengi huzungumza kingereza  na Kiswahili. 
26/1/20240 minutos
Episode Artwork

Human watch yatahumu jamii ya kimataifa kwa kukosa kusadia Sudan

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Right Watch limetuhumu jamii ya kimataifa kwa kukosa kushughulikia vita vinavyoendelea nchini Sudan. Kwa mjibu wa ripoti ya kila mwaka ya shirika hilo, jamii ya kimataifa haijafanya juhudi za kutosha kushawishi pande hasimu nchini Sudan Kusitsha vita. Ili Kufahamu negi zaidi skiza makala haya.
21/1/20240 minutos
Episode Artwork

Hali ya haki za binadamu nchini Kenya na Tanzania

Visa vya raia kupotea na kisha kuonekana  baada ya siku kadhaa nchini Kenya si vipya tena, hili likishuhudia mara kwa mara nchini Kenya, polisi wakituhumiwa kuhusika kwenye visa hivi lakini je tume ya haki za binadamu nchini Kenya inafahamu hili? na je nchini Tanzania hali ya hali za haki za binadamu ipo je?Maswali haya yanajibiwa ndani ya makala.
9/1/20240 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yakumbwa na uhaba wa fedha

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR, limeonya kuwa mashirika ya misaada yanakabiliwa na uhaba wa fedha, na kwamba yanahitaji dola milioni 400 kufikia mwisho wa mwaka huu. Katika kongamano la siku tatu kuhusu wakimbizi huko Geneva, Wiki iliyopita, Mkuu wa shirika hilo Filippo Grandi, alisema asilimia 75 ya wakimbizi wanaishi katika nchi maskini na zile zinazoendelea.Grandi ameiomba jamii ya kimataifa kutofumbia macho mamilioni ya waliokimbia makazi yao huko Ukraine, Sudan, Syria, Afghanistan, na vile vile DRC.Kuzungumzia haya na pia haki za wakimbizi kwa ujumla, Bi. Faith Kasina, msimamizi wa UNHCR ukanda wa Afrika mashariki alizungumza na George Ajowi.
19/12/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Ipo siku watu wanaoishi na walemavu watapata nafasi sawa katika jamii

Tarehe 3 Disemba mwaka huu, dunia iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya watu wanaoishi na ulemavu. Siku hii iliasisiwa mwaka 1992 na umoja wa mataifa. Nchini Kenya, siku hii ilifana sana huku sherehe ikiandaliwa katika maeneo mbalimbali. Katika eneo la Dagoreti, jijini Nairobi, tulikutana na Grace Wanjiku Maina ambaye alizaliwa na ulimavu lakini amejizatiti na kufanikiwa sana katika Jamii.Licha ya kuishi na Ulemavu Grace ni mshinda wa tuzo ya urembo ya kinadada wanaotumia vitu vya magurudumu, tuzo alioyoishinda 2017 na 2018, vile vile ni mwakilishi wa watu wanaoishi na ulemavu katika eneo la Dagoreti na pia mkurugenzi katika wakfu wa Sweet Aroma foundation, wakfu ambao unawatetea walemavu. Katika makala ya leo nimeanza kwa kumuuliza, nini kimebadilika tangu aliposhinda taji la urembo la miss Wheelchair miaka 6 iliyopita?
11/12/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kushinikiza serikali kutekeleza maamuzi ya mahakama

Mtandao wa Taasisi za Kitaifa za Haki za Kibinadamu za Kiafrika (NHRI)kwa ushirikiano na Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNCHR) pamoja na Taasisi ya Sheria ya Kibinadamu na Haki za Kibinadamu ya Raoul Wallenberg iliyo na makao yake makuu nchini Sweden iliandaa warsha ya kutathmini miradi kuhusu mafunzo ya Haki za Kibinadamu barani Afrika na ufuatiliaji wa jinsi ya Kutekeleza mapendekezo ya Maamuzi. Katika makala haya  Petronila Mukaindo, naibu mkurugenzi wa KNCHR anatoa twasira kamili ya changamoto na hatua za kutetea haki za kibinadamu nchini kenya na katika mataifa mengine.Kwa mengi zaidi skiza makala haya.
4/12/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Siku 16 za mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake

Kila mwaka dunia hutumia  siku 16  kuadhimisha mapambano ya kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto . Umoja wa mataifa huongoza kampeni hii na hufanyika kuanzia tarehe 25 Novemba na kumalizika tarehe 10 Desemba ya kila mwaka kwa ajili ya kupinga ukatili na kutetea haki za wanawake.Siku hiyo ilianza kuadhimishwa rasmi mwaka 1991 na tangu wakati huo zaidi ya asasi 6,000 kwa  zaidi ya nchi 187 hushiriki katika maadhimisho haya. Nchini Kenya katika eneo la Kibra baadhi ya kinadada wamethibitisha kuwa visa vya dhulma bado vipo na kati ya wanawake 5 wawili wamedhulumiwa kisaikologia na hata kingono .Ili kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
1/12/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Manufaa ya mitandao, mwandishi Paul Braine anasimulia

Ujio wa  mitandao umekuja na masaibu mengi tu, licha ya manufaa mengi, katika makala haya Benson Wakoli anakamilisha mahojiano yake na mwandishi wa kitabu cha Parenting in Dijital Era, yaani uzazi kipindi hiki cha kidijiti, bwana Paul Braine kuhusu manufaa na hasara za mitandao. Ili kufahamu mengi skiza makala haya.
28/11/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Haki ya watoto kipindi hiki cha kidigiti

Paul Braine mwandishi wa vitabu nchini Kenya, amechapisha kitabu kinachoangazia haki za watoto kulelewa kipindi hiki cha dijitali na jukumu la wazazi kuwalea watoto kipindi hiki. Benson Wakoli amezungumza naye kuangazia haki za kila pande yaani watoto na wazazi katika makala haya ya Jua Haki Zako. Kwa mengi zaidi skiza makala haya.
7/11/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Kenya : Serikali yaendesha bomoabomoa kwenye ardhi inayodai kuwa yake

Katika makala haya tunajadili hatua ya serikali nchini kenya kubomoa makaazi ya raia wanaodiwa kujenga nyumba zao kwenye ardhi ya serikali, ambayo inamilikiwa na kampuni ya simiti ya East African Portland cement. Kwa mjibu wa kampuni ya simiti ya East African Portland cement, raia waliojenga kwenye ardhi inayodai kuwa yake walikuwa wameonya dhidi ya kujenga kwenye ardhi hiyo.Ili kuelewa mengi zaidi skiza makala haya.
27/10/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

DRC : Haki za raia kuelekea uchaguzi mkuu

Nchini DRC raia wanajitarayarisha kushiriki uchaguzi mkuu mwezi disemba ambapo watapata fulsa kuwachagua wabunge pamoja na rais. Katika mantiki haya mwanaharakati ambaye sasa ni mwanasiasa Pascal Mpenda anafafanua ni vipi raia wa DRC wanapaswa kutumia haki yao ya kikatiba kuwachagua viongozi.Kwa mengi zaidi skiza makala haya.
23/10/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Sudan Kusini : Serikali inaminya uhuru wa kujieleza wa wanahabari

Kwenye makala ya juma hili tunaganzia ripoti ya bazara la haki za binadamu la umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, ambayo iliangaizia kwa kina mathila yanayotekelezwa na serikali ya Sudan Kusini dhidi ya wanahabari, wanaharakati pamoja na wanasiasa wa upinzani. Umoja wa mataifa kupitia afiasi yake ya haki za biandamu nchini Sudan Kusini, imeeleza kustitishwa kwake namna waandishi wa habari wanavyonyanyaswa na vyombo vya usalama nchini Sudan Kusini, Lengo likiwa kuuzia taarifa zozote zinazopaka tope serikali, baadhi ya wanahabari wanaokiuka hili wakitishwa, kufungwa jela na hata baadhi kuuawa.Skiza makala haya kwa mengi zaidi.
10/10/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Jamii zisizo na uraia zalilia serikali ya Kenya

Nchini Kenya serikali inalenga kuanza kutoa vitambulisho vya kidijiti ili kuimarisha huduma zake mbali na kuzuia wizi wa mitandao ambao umekuwa ukiteklezwa na wahalifu. Hata hivo mashariki mbalimbali yamejitokeza kupinga kuanza kwa shughuli hiyo hadi pale jamii mbalimbali ambazo zimekuwa zikishuhudia changamoto za kupata vitambulisho kutokana na kukosa uraia zikitaka serikali kushughulikia matatizo hayo kabla ya kuendelea na shughuli ya kuanza usajili.Jamii ni hizo ni pamoja raia kutoka nchini Rwanda, Wapemba, Wanubi na washona. Ili kufahamu mengi skiza makala haya.
3/10/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Kenya : Mashirika ya kirai yaitaka serikali kuzingatia sheria

Nchini Kenya serikali inapanga kuzindua mpango wa kusajili wakenya upya ili kuwapa kitambushi cha kidijiti, ambacho serikali inasema kitasaidia kuimarisha huduma zake. Hata hivyo masharika ya kiraia nchini humo yamepinga mpango huo yakisema haujazingatia sheria kwani serikali haijatoa hakikisho kuhusu usalama wa data ya wakenya. kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
25/9/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Mazingira yaathiri haki za watoto Africa

Wataalamu wa mazingira yameonya kuhusu athari kubwa inayotokana na maingira ambayo moja kwa moja inathiri watoto. Katika makala haya wanamazingira na watetezi wa haki za watoto wanajadili namna gani haki za watoto zinaweze lindwa kipindi hiki dunia inapotafuta mbinu ya kukabiliana na athari ya mabadiliko ya tabia nchi.
21/9/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

DRC : Visa vya ubakaji kambini Nyiragongo

Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka (MSF ) na wanawake wanaoishi  kwenye kambi baada ya kutoroka makaazi yao katika vijiji vya mkowa Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo DRC, wameeleza kuongezeka kwa visa vya ubakaji katika kambi ya Nyiragongo, wanawake hao wakitaka serikali ya DRC kuwashughulikia. Tangu mwezi Julai mwaka 2023 hadi sasa ni  kwamba zaidi ya wanawake elfu moja wamedhulumiwa kingono eneo la  Nyiragongo Mkoani Kivu kaskazini. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
18/9/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Haki ya wanawake kutumia mitandao

Katika makala ya haya tunaangazia haki za wanawake kutumia mitandao na haki za wanawanawake kwa jumla, kwa mengi zaidi skiza makala
6/9/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Changamoto za wachimba madini ya dhahabu nchini Kenya

Mchakato wa kupata madini ya dhahabu huwa ni ngumu sana. Wengi ambao wanajihusisha na kazi hii wanapitia changamoto nyingi ikiwemo kutotumia vifaa bora vya kujikinga, kazi nzito na hatimaye huenda hata kuangamia iwapo maporomoko ya ardhi yanapotokea.George Ajowi amezuru Kaunti ya Migori, Magharibi mwa  nchi ya Kenya. Ameandaa ripoti ifuatayo.
17/8/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Uhalifu wa kivita unafanyika Sudan : Amnesty International

Shirika la kimataifa la ketetea haki za binadamu Amnesty International  katika repoti yake ya hivi punde limesema pande hasimu nchini Sudan, zinatekeleza uhalifu wa kivita na kutaka jamii ya kimataifa kuingilia kati kunusuru hali. Shirika hilo linasema raia wa taifa hilo wanapitia mithila makubwa mikoni mwa wapiganaji wa RSF na jeshi, kwa mengi zaidi skiza makala haya.
9/8/20230 minutos
Episode Artwork

Jamii za mipakani taabani kupata vitambulisho

Kinyume na jamii nyingine nchini Kenya kundelea kupata vitambulisho bila vikwazo, jamii zinazoishi mikapani nchini humo zinaendelea kupitia changamoto za kupata vitambulisho, wengi wakilazimika kufanyiwa ukaguzi kabla ya kupewa stakabadhi hiyo muhimu. Katika makala haya, utaskia kutoka kwa wahusika ambao wametia changamoto si hapa ili kupata vitamblulisho, mashirika ya kiraia kama vile Namati yakiingilia kati kuhakikisha wahusika wanapata haki.kwa mengi zaidi skiza makala haya.
31/7/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Kenya: Polisi watumia nguvu kupita kiasi

Mashirika kadhaa ya kirai nchini yametuhumu polisi kwa kumia nguvu kupita kaisi kuwakabili wandamanaji wa upinzani wambao wamekuwa wakishiriki maandamano kutaka serikali kushughulikia kupanda kwa gharama ya maisha. Mashirika hayo yanatka  polisi wanaohusika kutumia kuchukuliwa  hatua za kisheria, wakati huu serikali ikiwatetea wahusika.
28/7/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Je wanawake wanatetea haki zao?

Katika makala haya tunajadili dhana kuwa wanawake hawapo mstari wa mbele kupigania haki zao, ambapo utaskia kauli ya Allan Ngare kutoka Human Right Watch anayekanusha vikali dhana hiyo, pia utaskia kutoka kwa mratibu wa kina dada wanaotumia miili yao kupata riziki bi Felister Abdalla anayesema wakati umewadia jamii kuwakumbatia. kwa jumla hata hivyo wote wanakiri kuwa hatua zaidi zastahili kuchukuliwa ili kulinda haki za wanawake.
26/7/20230 minutos
Episode Artwork

Hali ya kibinadamu katika mataifa ya Kenya,Burundi na DRC

katika makala haya tunaangazia hali ya Kinadamu ilivyo katika mataifa ya Kenya, Burundi na DRC, hii ni baada ya masharika kadhaa ya kutetea haki za binadamu kungazia hali ilivyo katika mataifa hayo. Watafiti kutoka shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International  wanatoa kauli zao kuhusu hali ya biandamu katika mataifa husika.skiza makala haya kwa mengi zaidi.
11/7/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Haki ya kupata habari za kweli na kuaminika

Taasisi ya Bazara Media Lab nchini Kenya imezindua mpango unalenga kutambua habari za kzeli na uongo, tasisi hi ikisema wamechochewa kuja na mpango huo kutokana na kuongezeka kwa habari ghushi katika mitandao ya kijamii.  Na licha ya taasisi kuwa na makao yake nchini Kenya, inalenga kupanua mabawa yake katika mataifa ya Africa Mashaki ili kuwasaidia wenye kuhumu mengi zaidi kuhusu habari za kweli na uongo.kwa Mengi zaidi skiza makala haya.
6/7/20230 minutos, 1 segundo
Episode Artwork

Watoto wanyanyaswa kigongo nchini DRC

Bunge la watoto wilayani Masisi Mashariki mwa DRC, linashutumu unyanyasaji unaofanyiwa watoto kwa kuhusishwa katika biashara ya ngono. Kulingana na mashairika ya kiraia na wanaharakati wa haki za binadamu huko Masisi, maelfu ya watoto wanatumiwa  kiuchumi na wazazi wao ambao huwalazimisha kufanya kazi  nao katika shughuli zao za vijijini na katika biashara ndogo ndogo za  kingono .Kwa mujibu wa wanaharakati kwa haki  za binadamu, hali  linatokana na vita vya M23 na makundi mengine yenye silaha ambayo yanafanya eneo hili kukosa usalama. Kwa mengi zaidi skiza makala haya.
5/7/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

DRC yatunga sheria kudhibiti kiwango cha mahari

Nchini DRC wabunge wametunga sheria kudhibiti kiwango cha mahari kinachostahili kutolewa, hii ni baada ya wanaume wingi kudaiwa kususia ndoa kutokana na kiwango cha juu cha mahari kinachoitishwa na familia ya wasichana. Je kuna haja ya kiwango cha mahari kuthibitiwa hasa ikizingatiwa jamii mbalimbali za kiafrica zina tamaduni zake?Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi
20/6/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Matumizi ya nguvu kupitia kiasi na polisi wakati wa maandamano

Mashirika ya kutetea haki za binadamu Human Right Watch na Amnesty International, yametuhumu polisi  nchini Kenya kwa matumizi ya nguvu kupita kiasi wakati wa kuwakabili wandamanaji wakati wa maandamano yaliokuwa yameitishwa na upinzani mwezi Machi. Katika ripoti yao mashirika hayo mawili, pia yametuhumu serikali ya Kenya kwa kukosa kuwachukulia hatua polisi wanaotuhumiwa kuhusika na visa vya ukiukaji wa haki za binadamu ikiwemo mauwaji ya raia 16.Ili kufahamu mengi zaidi sikiza makala haya.
16/6/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Kenya :Watoto wanaoishi na ulemavu vijijini wakosa mahitaji ya kimsingi

Nchini Kenya Watoto walio na ulemavu nchini kenya hasa maeneo ya mashinani wanazidi kupitia changamoto si haba ukilinganisha na wenzao wa mijini.Hii ni kutokana na ufukara unaozidi kuongezeka mashinani.-Takwimu kutoka shirika la afya duniani zinaonyesha kuwa takriban watoto milioni 2.5 wanaishi na ulemavu nchini Kenya huku asilimia 72 ya watoto walemavu wanaishi mashinani na asilimia 27.4 wanaishi mijini.Mwandishi wetu, Victor Moturi, alitembelea kaunti ya Kisii na Nyamira Ni msimu wa mvua na  katika shule hii spesheli ya Mwata  iliyoko Kaunti ya Kisii nchini Kenya,wanafunzi wasiokuwa na uwezo wa kuongea wamekongamana darasani kupokea mafunzo;Japo wanafunzi hawa wamo darasani,wamekosa vifaa muhimu vya mafunzo pamoja na chakula,Diana Metobo mmoja wa mwanafunzi  anasema wao wamekuwa wakipitia changamoto si haba..‘’’Tuna  changamoto nyingi, tunakosa chakula, nguo, soksi, viatu, hatuna bweni zuri, maji hayapo. Nyumbani kwetu hatuna chakula na hata vitabu vya kusoma hakuna. Tunayo nyumba lakini ni ya zamani sana,’’Amesema Metobo. John Oigara  ni mwanafunzi mwingine asiye na uwezo wa kuongea ,Oigara anadokeza kuwa,.yeye pamoja na wanafunzi wengine, hutegemea msaada kutoka kwa majirani pamoja na wahisani wengine ,ili kujiendeleza kimasomo vile vile kupata mahitaji mengine.‘’Wakati wageni walipokuja shuleni kwetu, walinunua chakula, blanketi, tangi la maji, sabuni, walituletea viatu, soksi na nguo.’’  Kilomita 40 kutoka mji wa kisii,shule ya msingi ya Riang’ombe DOK iliyoko Borabu ,kaunti ya Nyamira ni moja wapo ya shule zilizochaguliwa ili kutenga madarasa maalum kwa minajili ya watoto wanaoishi na ulemavu,lakini kulingana na mwalimu mkuu wa shule hii,George Onditi ,kwa muda sasa,wanafunzi hawajafika shuleni kwa sababu ya ukosefu wa waalimu pamoja na vifaa maalum vya masomo.‘’,,,,Watoto walikuwa wengi,takriban ishiriki lakini kwa sababu nimekosa mwalimu,wengine wamefichwa,wengine hawakuji shuleni,wengine wakiingia wakiona mwalimu wao hayuko basi wanarudi kwa sababu sisi hawatuoni kama waalimu wao.Serikali tafadhali wanisaidie ,watusaidie kama jamii tuweze kupata waalimu,tuweze kupata vifaa,ndiposa tuwashughulikie haa watoto hawa watoto ambao ni walemavu,’’ Amesema George Onditi ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Riang’ombe,,,,Kwa majina naitwa Stella Masaki,hili ni darasala la gredi 5,sasa wajua sisi hatujasomea taaluma hii,kwa hivyo tukiwachanganya hivi ,inatuchukuwa muda kuwafunza hawa badala ya kuwafunza wale ambao tumefunzwa jinsi ya kuwafundisha,kwa hivyo tunahitaji mwalimu ambaye atawashughulikia,wengine walichukuliwa na wazazi wao kwa sababu hatukuwa na uwezo wa kuwachunga,tukaona wale ambao wanaweza kuongea tukaona wabaki hapa tukae nao.Idadi ya wanafunzi walio na ulemavu wanaojiunga na shule  vijijini ni chache mno ukilinganisha na wenzao wanaoishi mijini.Hali hii imesababishwa na gharama ya juu ya vifaa vinavyohitajika kuwapa watoto hao mafunzo,ukosefu wa madarasa maalumu,na ukosefu wa usafiri .Agasa Maroko ni mwalimu maalum katika shule ya msingi magombo,kaunti ya Nyamira..’’.mimi nashughulikia wanafunzi ambao wana shida ya kiakili na wako wanafunzi kumi na watatu lakini kwa kijiji hiki kuna wale amabao hawajaingia shuleni kwa sababu hawana vifaa vya kuwaleta shuleni kama vile viti vya magurudumu.Hapa shuleni kuna mwingine akiona wenzake wanacheza nje anatoka darasani bila kuitisha ruhusa ,sasa mimi kama mwalimu ,lazima nitafute mbinu zote ambazo zitafanya huyo mtoto aingie darasani,na hata hawa walimu wengine kwa vile wana mapenzi kwa hao watoto,pia huwa wananisaidia sana’’Amedokeza mwalimu Maroko Wengi wa wanafunzi wanaoishi na ulemavu katika kaunti za kisii na nyamira ,hufichwa na wazazi ,hatua ambayo huwanyima haki zao za kimsingi pamoja huduma maalumu.‘’kwa mfano unakuta shule zimejengwa ambazo watoto hawawezi pita kuingia darasani,vyoo vya kujisaidia hawawezi tumia na watoto wengine,sasa inabidi tunawafungia hawa watoto nyumbani,kama mimi ninaye mmoja aliyekuwa katika shule ya msingi ya Riang’ombe D.O.K,ikawa sasa hatangamani na watoto wengine kwa sababu ni mlemavu,na hawezi ingia darasani ,na lazima abebwe,hivyo ikabidi tumuweke nyumbani’’Amesema Shujaa Mathias Maina ambaye ni mzazi wa  mtoto anayeishi na Ulemavu. Licha ya vizuizi hivi,Mashirika binafsi, kwa kushirikiana na utawala wa mitaa, wameanzisha mikakati na mipango ya kuongeza idadi ya wanafunzi wenye ulemavu wanaohudhuria shule nchini Kenya.Kama anavyoeleza Anthony Nyabera kutoka shirika la Progressive Africa, Ushirikiano huo una lengo la kutoa msaada muhimu kwa watoto wenye mahitaji maalum, kama vile vifaa vya masomo, sare za shule, viti vya magurudumu, na maelekezo ya kihisia.,’’,Haswa tunawasaidia wale watoto walemavu,pia tunawasaidia wale wenye ni wagonjwa,pengine wanataka kuenda kliniki,tunawapeleka,kama Kijabe ,Kisii,na wakati mwengine madaktari wanawatembelea nyumbani,tulianza kuwafundisha watoto wale wako na shida ya uti wa mgongo,vile vile tukawalipia huduma ya NHIF na ndio huwa wanatumia kwa sasa,pia tunawasaidia na viti vya magurudumu ili viwasaidie kuenda shuleni,vile vile tunawapa vitanda maalum walio na shida za uti wa mgongo,wenye hawawezi kusimama au kutembea,pia kuna vile tunawasaidia’’Amedokeza NyaberaKupitia juhudi hizi, idadi kubwa ya watoto tayari wamenufaika. Zaidi ya watoto 3000 wamepokea msaada unaohitajika ili kuendelea na elimu yao, hivyo kuwawezesha  kuafikia malengo ya elimu.Esther Nyaribari,ni mkurugenzi mkuu katika shirika la Touching souls initiative nchini Kenya‘’Mara ya kwanza tuligundua hawa watoto wako na changamoto za kupata chakula,na watoto hawawezi enda darasani na hawajakula,hivyo huwa tunatafuta wafadhili ambao husaidia hawa watoto kuwapa chakula kama vile mahindi maharagwe nakadhalika,halafu pia unapata watoto wamekuja shuleni wamevalia mavazi ya nyumbani,tunahakikisha tumewatafutia sare za shule angalau pia wafanane na wanafunzi wengine,pia kuna wale wanafunzi wenye umri mkubwa hasa wale walio na matatizo ya kiakili,pia hao tunawafikia manyumbani mwao na kuhakikisha maslahi yao yameshughulikiwa’’ Kulingana na takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani, inakadiriwa kuwa watoto milioni 2.5 wanaishi na ulemavu nchini Kenya. Katika idadi hii, takribani asilimia 72 wanaishi katika maeneo ya vijijini, wakati asilimia 27.4 wanapatikana  mijini.Kwa mujibu wa Nyaribari, Takwimu hizi zinaonyesha hitaji la haraka la kushughulikia changamoto maalum zinazowakabili  watoto wenye ulemavu katika maeneo ya vijijini.‘’Wito wangu kwa wazazi ni kuwa,wasifiche watoto na labda wasione wamepata watoto walemavu ni pigo wamepata,la hasha ,wawachukulie kama watoto wengine,wawatoe nje na wasiwafiche kwa sababu pia hao watoto wanahitaji masomo,wanahitaji matibabu na mambo mengine,kwa hivyo wawaweke wazi ndio sasa tuweze kuwasaidia kwa sababu wakiwaficha hatutaweza kujua kuna watoto wanahitaji msaada,’’Ameongeza NyaribariHuku idadi ya watoto wanaoishi na ulemavu ikizidi kuongezeka nchini Kenya,wazazi pamoja na mashirika ya kijamii ,wanaiomba serikali kuhakikisha uwepo wa vifaa vinavyohitajika kuwapa watoto hao masomo,kuongeza madarasa maalum vile vile kuajiri waalimu zaidi ili kupiga jeki masomo ya watoto wanaoishi na ulemavu.
13/6/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Haki ya raia wa wafaarika kuabudu

Katika makala haya  tunaangazia haki ya kuadubudu ambapo nchini Kenya uhuru huo umesbabisha vifo vya zaidi ya watu 200 kupoteza maisha yao kutokana na mafunzo potovu ya mchangaji Paul Mackenzi.  Mackenzi anadaiwa kuwashawishi wafuasi wake kufunga, yaani kukaa bila kula chakula hadi kufa ili kuonana na Masi Yesu Kristo mwana wa Mungu.Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
30/5/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Mashoga na wasagaji wakimbizi walilia haki nchini Kenya

Shirika la kimataifa la kutetea haki za biandamu Amnesty International limechapisha ripoti kuhusu kudhulumiwa kwa haki za mashago na wasagaji nchini Kenya, ripoti hiyo hasa ikijikiita zaidi  kwa wakimbizi na watafuta hifadhi katika kimbi kubwa ziadi nchini Kenya ya Kakuma;  Kambi ya kakuma ni nyumbani kwa zaidi ya watafuta hifadhi na wakimbizi 200,000  ikiwemo familia ya  mashoga na wasagaji.Ili kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
23/5/20230 minutos
Episode Artwork

Hali ya haki za binadamu nchini Tanzania

Shirika la kimataifa la kutetea haki za bindamu Amnesty Internatonal limeeleza wasiwasi wake kuhusu namna serikali ya Tanzania inavyotumia nguvu kupita kiasi kufurusha jamii ya Maasai ambayo inaishi eneo la Ngorongoro na Loliondo. Amnesty linasema serikali ya Tanzania haikushauriana na jamii hiyo kabla ya kuanza zoezi la kuwaondoa wenyeji hao katika ardhi zao asilia.Kwa mengi zaidi skiza makala haya.
15/5/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Je haki za wanawake zinaheshimiwa

Kwa kipindi kirefu wanawake wametazamwa kama viungo daifu kwa jamii hadi baadhi ya jamii bado zina dhana kwamba hawana haki ya kumiliki ardhi, je haki hizi zinaweza kuheshimiwa? Katika makala haya utaskia maswali yakiekelezwa kwa wanaharakati Sara Metei mtetezi wa haki za wanawake kumiliki ardhi kaunti ya Kajiado nchini Kenya, pamoja na Irene Maina kutoka Kituo cha haki cha Dandora.
11/5/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Haki ya wanawake kumiliki ardhi

Katika jamii nyingi za kiafrica si rahisi wanawake kuruhusiwa kumiliki ardhi, ni swala wengi sasa wanaliona kama limepitwa na wakati. Ni kutokana na hatua hiyo ndio maana wanaharakati kama vile Sarah Metei na Irene Maina wamejitokeza kupigania haki za wanawake kumiliki ardhi nchini Kenya.Wanaharakati hawa wanasema wakati umewadia katiba za mataifa ya Africa kuruhusu wanawake kumiliki ardhi, kwa mengi zaidi skiza makala haya.
1/5/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Haki ya watoto kupata elimu barani Africa

Changamoto za kupata elimu bora barani Africa zinazidi kuongezeka kadri watoto wanavyojiunga na shule, hili linatokana na ukosefu wa miundo bora pamoja na waalimu wa kutosha .  Hali hii imechangia watoto wengi kutojua kusoma na kuandika licha ya kuwa kwenye madarasa ya juu.Mfano nchini ,utafiti uliofanywa na shirika la uweza waonyesha kuwa asilimia 60 ya wanafunzi wa gredi ya nne nchini humo hawawezi kusoma masomo ya wale wa gredi ya tatu, ili kufahamu zaidi skiza makala haya.
10/4/20230 minutos
Episode Artwork

Mchango wa vijana kwa uchaguzi wa DRC

Taifa la DRC, linajianda kwa uchaguzi baadaye mwaka huu, lakini je vijana nchini humo wanafahamu mchango wao katika kufanikisha uchaguzi huo na kuhakikisha vijana wanapata haki yao ya kimsingi ya kuwachagua viongozi wanaofaa?katika makala haya tunaangazi hilo kwa kina.
3/4/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Mchango wa sanaa kupigania haki za binadamu

Mbali na wanaharakati kutumia sheria kuhakikisha maswala ya haki za binadamu zinaheshimiwa, wanaharakati pia wanatumia njia za Sanaa kama vile uingizaji, kuhakikisha kwamba ujumbe unawafikia wahusika. Katika makala haya,wanaharakati Domic Mutemi na Irene Maina, wote walijibu maswali kutoka kwa hadhira katika ukumbi wa Alliance Française, jijini Nairobi katika makala haya ya Jua Haki zako.
1/4/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Matumizi ya sanaa kupigania haki za binadamu Africa

Sanaa ni moja wapo ya nguzo muhimu katika kupigania haki za binadamu, katika makala haya mwanahabari wetu Benson Wakoli kwa undani anajadili na wanaharakati waagizaji Irene Kamau kutoka kituo cha haki cha Dandora, nchini Kenya pamoja na Domic Mutemi kutoka kituo cha haki cha Githurai. Bi Irene na  bwana Mutemi anasema kutokana na sanaa wamafikia mengi tu, katika kutetea haki za binadamu.
21/3/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Hedhi pasua kichwa kwa wasichana na wanawake

Nchini Kenya, Seneta Gloria Orwoba, anaendeleza kampeini ya kuhakikisha watoto wakike wanapata visodo ( taolo za kike) kampeni ambayo imepata hisia mseto kutoka kwa wakenya. Serikali ya Kenya, kwa muda imekuwa ikiahidi kuanza kutoa visodo bila malipo kwa wasichana wa shule lakini hili  limebakia tu ahadi.Katika makala haya Benson Wakoli, anajadili kwa kina na mwanaharati wa haki za wanawake bi Lucy Opondo, kufahamu ni vipi kampeini ya seneta Opondo itafaulu.
6/3/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Mchango wa vyombo vya habari kutetea haki za watoto

Runinga pamoja na redio ni baadhi ya vyombo vya habari ambayo vimetanjwa kuchangia kuimarika kwa ukuwaji wa watoto, hata hivyo baadhi ya vyombo hivi vya habari vinatuhumiwa kwa kukiuka haki za watoto ambapo  vinapeperusha vipindi vinavyoenda kinyume na maandili ya watoto. Katika Makala haya Benson Wakoli, anazungumza na bi Ann Sato, mratibu wa vipindi katika taasisi ya kuzalisha vipindi vya watoto ya Akili Kids, kujadili kile wanachozingatia katika kuzalisha vipindi hivi, ambapo pia utapata nafasi ya kuskia kutoka kwa bwana Peter Martin afisa kutoka mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya.
24/2/20230 minutos, 0 segundos
Episode Artwork

Serikali ya Uganda yasitisha huduma za afisi ya haki za bindamu ya umoja wa mataifa

Uamuzi wa Serikali ya Uganda wa kutoongeza kibali cha afisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu umewaacha wadau wengi wa masuala ya haki za binadamu na wanasiasa wa upinzani wakiwa wamekata tamaa na kutaka uamuzi huo ubadilishwe.  Hatua inatokana na kukamilika kwa leseni iliotolewa na serikali ya uganda kwa afisi hiyo kuendelea kuhudumu nchini Uganda.Serikali ya Uganda inasisitiza kuwa si lazima kila taifa liwe na afisi za umoja wa mataifa zinazoshugulikia haki za binadamu na kwamba tume ya kitaifa ya Uganda inayoshughulikia haki za binadamu ina nguvu zaidi za kuendelea kutekeleza wajibu uliokuwa unatekeleza na afisi hiyo ya umoja wa mataifa.Raia wengi wa Uganda hata hivyo wamelaini hatua hiyo ya serikali na kudai kuwa tume ya kutetea haki za biandamu nchini Uganda haina nguvu na kwamba mara nyingi huegemea upande wa serikali.Kwa ufahamu zaidi skiza makala haya. 
14/2/20230 minutos, 0 segundos