Winamp Logo
Wimbi la Siasa Cover
Wimbi la Siasa Profile

Wimbi la Siasa

Swahili, Political, 1 season, 62 episodes, 10 hours, 17 minutes
About
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Episode Artwork

Niger, Mali na Burkina Faso kujiondoa ndani ya ECOWAS

Mataifa ya Mali, Niger na Burkina Faso, yametangaza kujiondoa kwenye muungano wa ECOWAS, baada ya vikwazo ambayo muungano huu ulitangaza dhidi ya mataifa hayo, kipindi baada ya mapinduzi ya kijeshi. Benson Wakoli pamoja na wachanganuzi wa siasa za kimataifa, dkt Braine Wanyama na Mali Ali, wanatathimini Athari ya Niger, Mali na Burkina Faso kujiondoa ndani ya ECOWAS.Skiza makala haya.
2/3/20249 minutes, 42 seconds
Episode Artwork

Matarajio ya wakongo baada ya kuapishwa kwa rais Félix Tshisekedi

Wimbi la siasa imeangazia fursa iliyopo kidiplomasia kwa rais wa DRC Felix Thisekedi aliyeapishwa Jumamosi iliyopita, kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili.DR Congo, imekuwa kwenye mvutano wa kidiplomasia na Rwanda, kwa madai kuwa Kigali inawaunga mkono waasi wa M23 eneo la mashariki. Ruben Lukumbuka amewaalika Francois Alwende, mtaalamu wa siasa za DRC akiwa jijini Nairobi pia  Guerschome Kahebe pia ni mchambuzi wa siasa akiwa Jijini Washington nchini Marekani.
1/24/202410 minutes, 11 seconds
Episode Artwork

Mvutano kati ya ofisi ya rais nchini Kenya na idara ya mahakama

Rais wa Kenya William Ruto, ameingia kwenye mvutano na idara ya Mahakama. Ruto anasema Mahakama imejawa na Majaji mafisadi, wanaopindisha haki na kukwamisha miradi za serikali. Jaji Mkuu Martha Koome amekanusha madai hayo. Nini hatima ya mvutano huu ?
1/17/202410 minutes, 4 seconds
Episode Artwork

Mkataba kati ya Ethiopia na eneo lililojitenga na Somalia la Somaliland, kizungumkuti

Makala hii imejadili hatua ya rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud kusaini sheria ya kufuta makubaliano kati ya Ethiopia na eneo lililojitenga la Somaliland, hii ikiashiria kutoridhishwa na matumizi ya bandari ya Berbera, uamuzi unaoibua hofu ya kutokea mgogoro baina ya pande hizo mbili.Mwandishi wetu Ruben Lukumbuka ameangazia hili pamoja na mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Washington Marekani, Abdullahi Boru pamoja na profesa Macharia Munene ni mchambuzi wa siasa, na mtaalamu wa maswala ya kidiplomasia akiwa Jijini Nairobi hapa Kenya
1/10/202410 minutes, 1 second
Episode Artwork

Utendakazi wa CENI na mrengo wa upinzani katika uchaguzi wa Disemba 20

Maandamano yaliotishwa na upinzani kupinga utendakazi wa CENI yalizimwa na polisi nchini DRC
1/5/202410 minutes, 1 second
Episode Artwork

Tume ya uchaguzi nchini DRC kumtangaza rais Felix Tshisekedi mshindi uchaguzi wa Disemba 20 2023.

1/3/20249 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Raia wa DRC wapiga kura kumchagua rais na viongozi wengine

Wananchi wa DRC zaidi ya Milioni 40 wanapiga kura kumchagua rais, wabunge na madiwani. Tunachambua kwa kina.
12/23/20238 minutes, 28 seconds
Episode Artwork

Ripoti ya kamati ya maridhiano nchini Kenya

Suala la gharama ya maisha kupunguzwa lilikosa kupewa nafasi kwenye vikao vya jopo la maridhiano
11/30/20239 minutes, 41 seconds
Episode Artwork

Mjadala mkali Tanzania juu ya katiba mpya kwanza au mageuzi ya uchaguzi

Mwishoni mwa wiki jana mjadala umeibuka kati ya wadau wa kisiasa nchini Tanzania kuhusu nini kingekuwa cha kwanza kuwasilishwa bungeni, muswada wa marekebisho ya katiba au sheria za uchaguzi. Ni mjadala ambao umewagawa hata wapinzani, ambapo chama kikuu cha upinzani Chadema chenyewe kinataka katiba mpya kwanza, huku vyama vingine vyenyewe vikisema sheria ya uchaguzi ianze.Wachambuzi ni pamoja na Jawadu Mohammed kutoka Tanzania pia Dr. Nicodemus Minde akiwa nchini Kenya.
11/18/202310 minutes, 1 second
Episode Artwork

Mkutano wa SADC watamatika bila kuzaa matunda

Katika makala wimbi la siasa tunaangazia hisia mseto zinazoenea kwenye eneo la ukanda wa nchi za maziwa makuu, baada ya mwishoni mwa juma lililopita, wakuu wa nchi kutoka Jumuiya ya SADC waliokutana mjini Luanda, Angola, kushindwa kutoa terehe kamili ya vikosi vyake kupelekwa mashariki mwa DRC. Aidha, viongozi wa SADC walikubaliana kumpa muda zaidi rais wa Angola, Joao Lourenco, kuendelea na juhudi za upatanishi kati ya nchi ya DRC na Rwanda. Mwandishi wetu George Ajowi anazungumza na Haji Kaburu akiwa Tanzania na Guershome Kahebe akiwa Marekani..
11/8/20239 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Wanasiasa wa upinzani wa Afrika kuungana hivi karibuni

Makala ya Wimbi la siasa wiki hii inampokea kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Burundi, CNL Bwana Agathon Rwassa katika mahojiano maalum na Idhaa hii ya RFI Kiswahili
11/1/202310 minutes, 9 seconds
Episode Artwork

Bunge la seneta nchini DRC larefusha muda wa dharura kwa siku 15

Siku chache baada ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi kutangaza kulegeza hatua kwa hatua makataa ya hali ya dharura kwenye majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri mashariki mwa nchi hiyo, wiki hii bunge la seneta lilikutana na kuongeza muda wa hali hiyo, Ungana na mwandishi wetu Victor Moturi pamoja na Omari Kavota mtaalamu wa siasa za DRC akiwa mjini Beni, pia Promesse Matofali Yonama, ni mbunge wa bunge la mkowa wa Kivu kaskazini 
10/19/20238 minutes, 47 seconds
Episode Artwork

Mataifa mbalimbali dunia, yamelaani hatua Hamas kuivamia Israel

Mataifa mbalimbali dunia, yamelaani hatua ya kundi la Hamas kutoka Mamlaka ya Palestina kushambulia miji mitatu ya  Kusini mwa Israeli na kurusha maelfu ya maroketi kutokea ukanda wa Gaza. Aidha Urusi imesema kuundwa kwa taifa la Palestina, ndilo suluhu kwa mzozo wa Isreali na Palestina, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov, akisema vita havitaleta suluhu.
10/11/202310 minutes, 10 seconds
Episode Artwork

Baraza la usalama la UN kuidhinisha Kenya kuongoza kikosi cha polisi cha kimataifa nchini Haiti

Kenya ilijitolea kuongoza kikosi hicho ambacho kimepewa mamlaka ya kukabiliana kwa mtutu na makundi yenye silaha nchini humo ambayo kwa muda mrefu yametatiza usalama wa taifa taifa hilo la Karibia.
10/4/202310 minutes, 3 seconds
Episode Artwork

Mwaka mmoja tangu kuapishwa kwa rais wa Kenya William Ruto, Septemba 13 09 2022

9/13/202310 minutes, 1 second
Episode Artwork

Nafasi ya siasa kukabili mabadiliko ya tabia nchi barani Afrika

Wiki hii, wakuu wa nchi za bara Afrika, watunga sera na wanaharakati walikutana jijini Nairobi, kujadili namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Je, utashi wa kisiasa upo kufikia malengo ya azimio lililokubaliwa ? 
9/7/202310 minutes, 8 seconds
Episode Artwork

Kipimo cha Demokrasia nchini Zimbabwe, huku wananchi wakipiga kura

Wananchi wa Zimbabwe, wanapiga kura kumchagua rais na wabunge. Rais Emmerson Dambudzo Mnangagwa 80, anapambana na mgombea wake mkuu Nelson Chamisa, 45. Nini hatima ya demokrasia nchini Zimbabwe ? Tunajadili kipimo cha demokrasia katika taifa hilo la Kusini mwa Afrika.
8/24/202310 minutes, 14 seconds
Episode Artwork

DRC: Viongozi wakutana Kinshasa kutathmini hali ya dharura Kivu Kaskazini na Ituri

Viongozi kutoka kwenye majimbo mawili ya Ituri na Kivu Kaskazini wanazungumza na wale wa Serikali kuu, kuhusu ikiwa makataa ya hali ya dharura iliyotangazwa kwenye majimbo yao iondolewe au la, ingawa wanasiasa wengi kutoka kwenye maeneo hayo wanataka iondolewe.
8/16/202310 minutes, 1 second
Episode Artwork

Mapinduzi ya Niger tumbo joto kwa ECOWAS

Nchini Niger viongozi wa mapinduzi wamekatakata kuonana na ujumbe wa ECOWAS kujadili mchakato wa kurejesha madarakani rais Mohamed Bazoum.  Hii ni licha ya ECOWAS kutishia kutumia nguvu kumrejesha madarakani rais Bazoum, wakati vikwazo wa viongozi wa mapinduzi vikiendelea kutolewa.Katika makala haya Benson Wakoli na wachambuzi wa siasa za kimataifa Mali Ali akiwa katika visiwa vya Mayotte na Jawadu Mohamed akiwa nchini Tanzania, wanadadavua hali nchini Mali.
8/9/20239 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Juhudi za kikanda ili kukabiliana na mapinduzi ya kijeshi Afrika magharibi

Wimbi la siasa imeangazia yaliyojiri nchini Niger baada ya maafisa wa jeshi kumng’atusha madarakani Mohammed Bazoum aliyechaguliwa chini ya misingi ya kidemokrasia, hali inayoendelea kwa sasa pamoja na juhudi za Ecowass kutaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia, na kuachiwa huru kwa rais Bazoum. Kuchambua hili wachambuzi Mali Ali  akiwa kwenye Visiwa vya Mayote, pamoja na Hajji Kaburu akiwa jijini Daresalaam nchini Tanzania.
8/2/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Uchambuzi kuhusu siku mia moja za vitaa vya wenyewe kwa wenyewe Sudan

Katika Makala haya ya leo Ali Bilali anajadili na wachambuzi kuhusu siku mia moja ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan
7/29/202310 minutes, 2 seconds
Episode Artwork

Uchambuzi kuhusu siasa ya Zimbabwe baada ya upinzani kuzuiliwa kufanya kampeni

WImbi la siasa juma hili Ali Bilali na wachambuzi wake wanajadili hali ya kisiasa nchini Zimbabwe kuelekea kwenye uchanguzi mkuu wa rais
7/27/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Maandamano ya upinzani nchini Kenya

Upinzani nchini Kenya umeitisha maandamano ya siku tatu wiki hii kupinga kile wanachosema ni kupanda kwa gharama ya maisha, ukitaka serikali ya rais William Ruto kushugulikia suala hilo kwa dharura.
7/19/20239 minutes, 44 seconds
Episode Artwork

Zimbabwe : Marafuku ya kuanzishwa kwa kampeni za chama cha upinzani

Tunaangazia hatua ya mahakama nchini Zimbabwe kuidhinisha marafuku kuanzishwa kwa kampeni iliyopangwa kufanywa na chama kikuu cha upinzani wakati huu pia kiongozi wake mkuu Nelson Chamisa akikabiliwa na vikwazo.
7/15/20239 minutes, 26 seconds
Episode Artwork

Hatua ya rais wa Senegal kutangaza kutowania muhula mwengine

Hatua hiyo rais Macky Sall, imesifiwa nje na ndani ya taifa lake baada ya kuwepo hofu kuwa angetangaza kuwania tena. Rueben Lukumbuka amezungumza na wachambuzi wa siasa kuhusu suala hili.
7/6/202310 minutes
Episode Artwork

Siku ya Kimataifa ya kuadhimisha lugha ya Kiswahili

Kuelekea siku ya Kimataifa ya kuadhimisha lugha ya Kiswahili, watalaam Wanjohi Mugambi kutoka Kenya, na Pascal Baguez kutoka Ufaransa wanajadili maendeleo ya lugha hiyo.
7/6/202310 minutes, 7 seconds
Episode Artwork

Uasi wa kiongozi wa wapiganaji mamluki wa Wagner Yevgeny Prigozhin, nchini Urusi.

Juma hili msikilizaji tunatupia jicho matukio ya mwishoni mwa juma lililopita nchini Urusi, ambapo kiongozi wa kundi la wapiganaji, mamluki wa Wagner, Yevgeny Prigozhin, alitekeleza kitendo kilichotajwa kama uasi, baada yake kuongoza wapiganaji wake kuuteka mji wa Rostov-on-Don kusini, na kisha kusonga mbele kabla ya kusitisha mpango wao wa kufika Moscow.
6/28/202310 minutes
Episode Artwork

Usalama nchini Uganda na ukanda baada ya mashambulio ya ADF

Kundi la waasi la ADF Lenye asili nchini Uganda ila limekuwa likitikileza  mashambulio mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ,limewauwa watu 42 nchini Uganda baada ya kushambulia shule ya sekondari eneo la Kasese ADF linaonekana kuwa tishio baada ya ripoti ya umoja wa mataifa kuonesha ADF imekuwa ikifadhiliwa na kundi la Kijihadi la Islamic State tangu mwaka 2019. Kuna hofu mtandao wake ADF unaweza kusambaaa zaidi baada ya ripoti hiyo kusema Islamic State imekuwa ikiwatumia watu kutoka mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini.
6/22/202310 minutes, 4 seconds
Episode Artwork

Kamatakamata ya wapinzani kwenye mataifa ya Afrika nini hatma yake?

Makala ya wimbi la siasa hii leo inaangazia hali ya kamata kamata inayotekelezwa na vyombo vya usalama dhidi ya wapinzani kwenye mataifa kadhaa ya Afrika mfano huko DRC Salomon Idi Kalonda mshauri wa kisiasa wake Moise Katumbi, hali kama hiyo inashuhudiwa pia huko Burundi katika chama cha upinzani cha CNL, Nchini Senegal huko na Kinara wa Upinzani Ousmane Sonko alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kufuatia tuhuma za ubakaji. Mwandishi wetu Reuben Lukumbuka amewaalika Mali Ali ni mchambuzi wa siasa za Nchi za maziwa makuu akiwa Visiwani Mayotte na pia Francois Alwende ni mchambuzi na mataalamu wa siasa za DRC akiwa Jijini Nairobi nchini Kenya
6/14/202310 minutes, 1 second
Episode Artwork

Hatima ya mswada wa fedha nchini Kenya

Kwanini mswada wa fedha unazua gumzo na mjadala nchini Kenya ? Tunajadili hili kwenye Makala ya Wimbi la Siasa
6/7/202310 minutes, 2 seconds
Episode Artwork

Ziara ya rais Tshisekedi wa DRC huko CHINA,pia mchakato wa uchaguzi wa 2023

Makala ya wimbi la siasa wiki hii imeangazia ziara ya rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi nchini China, na pia maendeleo ya mchakato wa uchaguzi kwenye nchi hiyo.Waalikwa wetu katika kuzungumzia hili ni Kashando Mukanisa Yvon mchambuzi huru na mtaalamu wa siasa za DRC, wakili Moise Bashwira wa chama cha UNC moja ya vyama madarakani vya Sacred Union, na pia Muhindo Safari Akayezu wa chama cha upinzani cha Ensemble pour la République chake Moise Katumbi. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kupata mengi zaidi
5/31/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Hali inavyoendelea nchini Sudan

Makala ya wiki hii yanaangazia hali inavyoendelea nchini Sudan wakati huu kukiwepo na mkataba wa kusitisha mapigano
5/24/20239 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Kukutana kwa kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga na rais Ruto kwenye hafla ya hadhara

Hii ni baada ya rais Ruto na  Odinga mwishoni mwa wiki iliyopita, kuonekana hadharani pamoja, mwanzo katika mazishi ya mke wa mpiganiaji uhuru Dedan kimathi, Mukami Kimathi na baadaye katika mashindano ya riadha na mchezo wa soka Jumapili iliyopita.
5/17/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

SADC kutuma kikosi nchini DRC, Tshisekedi akosoa kikosi cha EAC

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi amelishtumu jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kutofanya vya kutosha kudhibiti utovu wa usalama Mashariki mwa nchi yake.Mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC, wamesema watatuma kikosi chake Mashariki mwa DRC, huku Umoja wa Mataifa ukita juhudi zaidi kusaidia kupatikana kwa amani. Tunachambua kwa kina.
5/10/202310 minutes, 17 seconds
Episode Artwork

Je serikali ya Kenya ianze kudhibiti makanisa

Karibu katika makala wimbi la siasa. Tunaangazia swala la mhubiria Paul Mackenzie Nthenge ambaye aliwashawishi wafuasi wa kanisa lake wafunge bila kula ili wakutane na Mungu katika kijiji cha Shakahola karibu na mji wa Malindi, Pwani ya Kenya. Nchini Kenya, idadi ya watu wanaohusishwa na imani potofu ya kutokula chakula hadi kufa ili kumwona Mungu, imeongezeka na kufikia 98 baada ya miili mingine kufukuliwa katika kijiji cha Shakahola karibu na mji wa Pwani, Malindi.Tukio hilo limezua hasira miongoni mwa viongozi, wananchi na wenyeji huku mchungaji anayedaiwa kuwashawishi wauamini wake kufunga mpaka kufa Paul Mackenzie Nthenge akiendelea kuzuiwa.Kuzungumzia swala hili naungana studioni na Askofu mkuu wa kanisa la anglikana nchini Kenya Jackson Ole Sapit pamoja na afisa wa sheria katika shirika la kutetea haki za binadamu nchini Kenya Haki Afrika Walid Seketi.
4/27/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Sudan: Majenerali waendelea kupimana nguvu licha ya juhudi za kidiplomasia

Wiki hii kwenye Makala wimbi la siasa, Jupiter Mayaka anafanya mwendelezo wa mzozo unaoendelea nchini Sudan, wakati huu hali ya kibinadamu ikizidi kuwa mbaya, kutokana na raia kuuawa na misaada kutowafikia waathiriwa. Juhudi za kidiplomasia zinaendelea kutoka ukanda na kimataifa, ili kuwapatanisha mkuu wa jeshi la Sudan, jenerali Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake, Mohammed Hamdan Daglo maarufu Hemedti ambaye ni kiongozi wa kikosi cha RSF.
4/19/202310 minutes
Episode Artwork

Kucheleweshwa kwa kusainiwa kwa mkataba wa kisiasa nchini Sudan

Kwenye Wimbi la Siasa wiki hii, Ali Bilali anaangazia kucheleweshwa kwa kusainiwa kwa mkataba wa kisiasa nchini Sudan, utakaoruhusu kuundwa kwa serikali ya kiraia baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 2021.   Mara mbili mapema mwezi huu, mwezi huu, wawakilishi kutoka uongozi wa kijeshi na wale wa kiraia waliahirisha tukio hilo la kihistoria baada ya kuripotiwa kuwepô kwa mvutano kuhusu namna ya kujumuishwa kwenye jeshi la taifa kwa kikosi maalum Rapid Support Forces (RSF). 
4/12/20239 minutes, 48 seconds
Episode Artwork

Mchakato wa maridhiano kati ya serikali na upinzani nchini Kenya baada ya maandamano

Rais William Ruto na kinara wa upinzani Raila Odinga watoa nafasi ya kuzungumza kumaliza mzozo wa kisiasa Baada ya majuma kadhaa ya kupinga madai ya upinzani, hatimaye, serikali ilikubali kuketi kwenye meza ya majadiliano kupitia bunge kuyatafutia ufumbuzi masuala yaliyoibuliwa.
4/6/202310 minutes, 6 seconds
Episode Artwork

Je, suluhu ya kisiasa itazaa matunda kuhusu mzozo wa DRC

Suluhu ya kudumu kuhusu mzozo wa usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, haijapatikana mpaka sasa. Waasi wa M 23, wameendelea kupambana na wanajeshi wa serikali. Jumuiya ya Kimataifa, inasema suluhu ni ya kisiasa. Je, itawezekana ? Tunajadili hili na wachambuzi, Price Mugasalusha na Edwin Kegolu, kutoka kwenye ukumbi wa Alliance Francais jijini Nairobi. 
3/29/202310 minutes, 1 second
Episode Artwork

Nini hatima ya mvutano wa kisiasa nchini Kenya ?

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, ameitisha maandamano kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha na kuipinga serikali ya rais William Ruto kwa kile anachosema hakushinda uchaguzi wa urais wa mwaka uliopita. Nini suluhu ?
3/24/202310 minutes, 15 seconds
Episode Artwork

Nafasi ya wanawake kwenye siasa za bara Afrika

Leo tunatupia jicho nafasi ya wanawake kwenye siasa za bara Afrika.  Wiki hii siku ya Jumapili tarehe 19  rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, anatimiza miaka mitatu madarakani, baada ya kuapishwa kuongoza nchi hiyo kama rais wa sita, na kuwa rais wa kwanza mwanamke.    Samia alichukua hatamu za uongozi baada ya kifo cha mtangulizi wake John Magufuli.  Huku nchini Namibia, chama tawala SWAPO, kimemteua mwanamke mwingine Netumbo Nandi-Ndaitwah kuwa mgombea wake wakati wa uchaguzi huu mwaka ujao.  Je, nyota ya wanawake barani Afrika, kwenye medani ya kisiasa imeanza kungaa? Kujadili hili, tunaungana nayeAnna  Henga Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu akiwa Dar es salaam nchini  Tanzania na Maimuna Mwidau akiwa Mombasa akiwa Kenya. 
3/15/20239 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Siku ya kimataifa ya wanawake duniani

Kauli mbiu ya sherehe za mwaka huu wa 2023 imekuwa ni matumizi ya kidigitali kwa usawa wa kijinsia na namna wanawake wanaweza kutumia teknolojia kuaangazia na kutafuta suluhu ya changamoto zao.
3/10/202311 minutes, 24 seconds
Episode Artwork

Harakati za chama cha upinzani nchini Kenya

Makala haya ya Wimbi la siasa, juma hili  tunapigia darubini siasa za upinzani zinazoendelezwa nchini Kenya.  Juma lililopita, kinara wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, alitangaza kuitisha maandamano ya nchi nzima ndani ya siku 14 zijazo, ikiwa matakwa ya muungano wao wa Azimio hayatatekelezwa ikiwemo kushusha gharama ya maisha kwa raia. 
3/1/20239 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Viongozi wa EAC wataka M23 kuachilia maeneo, viongozi wa AU wapinga mapinduzi Afrika

Makala ya Wimbi la siasa imeaangazia kauli ya viongozi wa EAC waliokutana huko Addis Ababa Ethiopia  walithibitisha kuunga mkono michakato ya Luanda na Nairobi ambayo inawataka waasi wa M23 Huko DRC kusitisha mapigano na kuondoka katika maeneo wanayoyashikilia, katika sehemu ya pili viongozi wa Afrika walisisitiza msimamo wao wa kutovumilia njia zisizo za kidemokrasia, kuchukua madaraka wakijadili hali ya mapinduzi ya kijeshi kule Burkina Faso, Guinea, Mali na Sudan..Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka akiwa na wageni wake: Francois Alwende, mchambuzi wa siasa akiwa Nairobi nchini Kenya, pia Hajji Kaburu mchambuzi akiwa Dar Es Salaam Nchini Tanzania
2/22/202310 minutes, 8 seconds
Episode Artwork

Hatima ya usalama wa eneo la maziwa makuu na ule wa mashariki mwa DRC mashakani

Makala hii imeangazia hali inayoendelea huko mashariki mwa DRC ambapo hivi karibuni maelfu ya raia kwenye mji wa Goma, waliandamana kupinga uwepo wa vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki, wanavyosema vimeshindwa kuwadhibiti waasi wa M23, ni maandamano ambayo yalifanyika siku chache baada ya viongozi wa Jumuia ya EAC kukutana jijini Bujumbura Burundi ambapo waliwataka waasi kusitisha mapigano, kuheshimisha mkataba wa Luanda unaowataka kuondoka katika maeneo wanayoyashikilia, wakati huu kundi hilo likiripotiwa kuchukua miji zaidi.   
2/8/202310 minutes, 6 seconds
Episode Artwork

Joto la kisiasa limeanza kupanda nchini Kenya

Nchini Kenya siasa zimeanza tena miezi tano tu baada ya uchuguzi mkuu, siasa hizo zikichochewa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kukataa kutambua serikali ya rais William Ruto. Je hili lina maana gani ?Benson Wakoli, amezungumza na mchambuzi wa siasa za Kenya Brain Mutie katika makala haya ya wimbi la siasa.
2/1/202310 minutes
Episode Artwork

UHUSIANO WA UFARANSA NA NCHI ZA BURKINA FASO NA MALI

Msikilizaji katika miaka ya hivi karibuni, nchi ya Ufaransa, imeendelea kujikuta matatani na mataifa ambayo wakati mmoja iliwahi kuyatawala wakati wa ukoloni. Hata hivyo hivi karibuni uhusiano kati ya baadhi ya nchi hizo na utawala wa Paris, umekuwa ukizorota kuanzia Mali na sasa Burkina Faso.   Makala ya wimbi la siasa juma hili, inaangazia hatua hizi za nchi ya Mali na Burkina Faso, zinaashiria nini kwa mustakabali wa uwepo wa Ufaransa kwenye nchi za Afrika Magharibi, na kuzungumzia hili , Mwandishi wetu Carol Korir amezungumza na Hamduni Marcel mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Mwanza Tanzania, pamoja na Mali Ali, akiwa katika visiwa vya Mayotte.
1/25/20239 minutes, 51 seconds
Episode Artwork

Tanzania: Tundu Lissu atangaza kurejea nyumbani

Mwanasiasa wa Tanzania, Tundu Lissu, baada ya kuishi uhamishoni kwa karibu miaka saba, ametangaza kuwa anarejea nyumbani Januari 25 2023, kuendeleza harakati za kisiasa, baada ya rais Samia Suluhu Hassan, kutangaza kuondoa marufuku ya vyama vya siasa, kufanya mikutano ya kisiasa. 
1/18/202310 minutes, 4 seconds
Episode Artwork

M23 bado inashikilia baadhi ya maeneo mashiriki mwa DRC

Licha ya tetesi za kundi la M23 kudai kuchilia baadhi ya maeneo mashariki mwa DRC, taarifa sinasema waasi hao bado wanashikilia maeneo mengi mashariki mwa DRC. Skiza makala haya ufahamu mengi.
1/16/202310 minutes
Episode Artwork

Kufutwa kwa kesi zinazowahusu wandani wa rais William Ruto

Tangu mwaka jana ,idara ya mahakama nchini Kenya imefuta baadhi ya kesi dhidi ya watu walio karibu na rais William Ruto Mahakama nchini Kenya imefuta kesi nyingi zinazowahusu wandani wake rais William Ruto ,kwa msingi wa kukosa ushahidi.Baadhi ya waliofutiwa mashtaka ni naibu rais Rigathi Gachagua,waziri  Aisha Jumwa na Minthika Linturi. Katika makala haya Eric Theuri ,rais wa chama cha mawakili nchini Kenya ,LSK na Daktari Brian Wanyama mhadhiri  katika chuo kikuu cha Kibabii ,Bungoma nchini Kenya ,ambaye pia ni mchambuzi wa siasa ,wanazungumzia hatua hii ambayo imetafsiriwa na wengi kuwa ya kisiasa
1/5/202310 minutes, 5 seconds
Episode Artwork

Siku mia moja za rais wa Kenya William Ruto ofisini na ahadi alizoahidi kutimiza ndani ya siku hizo

Disemba 22, rais wa Kenya William Ruto alitamatisha siku 100 ofisini, huku baadhi ya watu wakihoji kuhusu ahadi alizotoa kwa wakenya wakati wa kipindi cha kampeni na hata siku ya kuapishwa kwake. Moja ya aahdi alizotoa inayomgusa mwananchi wa kawaida moja kwa moja, ni kupunguza gharama ya maisha kutokana na kupanda kwa bei ya vyakula.
12/30/202210 minutes
Episode Artwork

Matukio ya kisiasa tuliyoyapa uzito mwaka 2022

Nchi mbalimbali, zikiongozwa na Ufaransa pamoja na Kenya, ziliandaa uchaguzi wake mwaka huu. Tulijadili matukio hayo kwa kina, na leo tunakukumbusha baadhi ya matukio hayo, japo kwa kifupi.
12/21/202210 minutes, 14 seconds
Episode Artwork

Mazungumzo ya amani kuhusu Mashariki mwa DRC yanafanyika jijini Nairobi

Makundi ya waasi, serikali ya DRC, mashirika ya kiraia na wadau wengine, wapo jijini Nairobi kwa ajili ya mazungumzo ya tatu ya amani, ili kuleta amani Mashariki mwa nchi hiyo. Je, suluhu itapatikana ?
11/30/20229 minutes, 47 seconds
Episode Artwork

Mkataba wa kuanzishwa mfuko wa fedha kushughulikia athari za mabadiliko ya tabianchi COP27

Katika mkutano wa kimataifa wa mazingira COP27, nchini Misri, mataifa karibu mia mbili yaliafikia makubaliano ya kuanzishwa kwa mfuko wa fedha wa kushughulikia hasara na uharibifu, fedha hizi zikitarajiwa kuzisaidia nchi masikini na zilizo katika hatari ya kuathirika zaidi na athari za mabadiliko ya tabianchi.
11/25/202210 minutes, 1 second
Episode Artwork

Juhudi za kidiplomasia kusaka amani Mashariki mwa DRC

Rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, anaongoza jitihada za kidiplomasia kusaidia kuleta amani Mashariki mwa DRC, kuelekea awamu nyingine ya mazungumzo ya amani jijini Nairobi. Juhudi hizi zinaendelea wakati huu waasi wa M 23 yakiendelea kati ya jeshi la serikali, FARDC. Je, suluhu itapatikana ?
11/16/20229 minutes, 7 seconds
Episode Artwork

Mapigano mashariki mwa DRC.

Makala hii imeangazia hali ya usalama inayojiri huko mashariki ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, ambako Kundi la waasi wa M23 likiungwa mkono na Rwanda lilifanikiwa kuyateka miji miwili muhimu ya Rutshuru na Kiwanja mashariki ya DRC na kuendelea na mapigano kwenye viunga vya mliji hiyo, huku serikali ya Kinshasa ikichukua uamuzi wa kumfurusha Balozi wa Rwanda nchini humo, Vincent Karega huku Juhudi za kimataifa zikiendelea kuzipatanisha nchi hizo mbili. Kuangazia hili tumewaalika profesa Pacifique Malonga, ni mtaalamu wa sias aza Rwanda akiwa jijini Kigali nchini Rwanda naye Guerschom Kahebe ni mchambuzi na mtaalamu wa siasa za DRC akiwa Calfornia nchini Marekani.
11/2/20229 minutes, 58 seconds
Episode Artwork

Ongezeko la mapinduzi ya kijeshi Barani Afrika

Msikilizaji utaskia mengi kuhusu chanzo cha ongezeko la mapinduzi ya kijeshi barani Afrika.Mapinduzi kama haya yameshafanyika kwenye nchi za Guinea na Mali, huku majaribio mengine kadhaa yakishindikana kwenye ukanda huo. Mwaka 2021 ulishuhudia idadi kubwa ya mapinduzu barani Afrika ukilinganisha na miaka iliyopita. Leo tunaangazia kwa kina yanayotokea na pengine kutafuta suluhu
10/26/202210 minutes, 1 second
Episode Artwork

Mjadala kuhusu utovu wa usalama Mashariki mwa DRC

Mapigano yaendelea kushuhudiwa nchini DRC, kati ya jeshi la serikali FARDC na waasi wa M23, serikali ya Kinshasa ikiendelea kushtumu nchi jirani ya Rwanda kuwaunga mkono waasi. Juhudi za mazungumzo hadi sasa hazijafua dafu.
10/26/202210 minutes
Episode Artwork

Mjadala kuhusu mchango wa vyama vya upinzani barani Afrika katika kukuza demokrasia

Demokrasia ya kweli, wataalamu wanasema inajengwa na kuwa na mifumo mizuri ya kiutawala na kuruhusu uwepo wa vyama vingi, ambavyo hutumika kujenga utawala bora, na uwepo wa vyama vingi ni pamoja na kuwa na vyama vya upinzani vyenye ushawishi, vyenye uwezo wa kukosoa na kuishauri serikali pale ambapo inaonekana kwenda kinyume na matakwa ya demokrasia na utawala bora.
10/21/202210 minutes, 2 seconds
Episode Artwork

Mjadala kuhusu kuondolewa kwa mipaka ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki

Karibu katika Makala yetu leo wimbi la siasa, kwenye usukani uko nami Ali Bilali ambapo tunajadili kuhusu maendeleo ya jumuiya ya Afrika Mashariki hususan kuhusu kauli ya hivi karibuni ya rais mpya wa Kenya William Ruto, ambae amemuomba Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akiwa kama mkongwe miongoni mwa Viongozi wa Afrika Mashariki kupambana ili kuhakikisha mipaka inayotenganisha Nchi inaondolewa na kuondoa vikwazo vingine vyote.
10/12/20229 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Rais Macron anaweza kuwapatanisha, Kagame na Tshisekedi

Pembezoni mwa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikutana na wenzake wa Rwanda, Paul Kagame na Felix Tshisekedi, kuona uwezekano wa wawili hao kufikia mkataba wa amani kuhusu utovu wa usalama, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
9/28/202210 minutes, 9 seconds
Episode Artwork

Antonio Guterres : M23 ni tishio kwa MONUSCO

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amedai kwamba waasi wa M23 wana silaha nzito kushinda wanajeshi wa Umoja wa mataifa wanaohudumu nchini DRC, MONUSCO, akisema sharti mbinu tofauti itumike kuwashinda waasi hao . Katika makala haya tunathimini kauli hii ya Guterres.
9/21/20229 minutes, 49 seconds